Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mheshimiwa Farida Mgomi amewataka wananchi kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama wilayani humo kwa kubaini wahalifu na uhalifu ili hatua zichukuliwe mapema.
Mheshimiwa Mgomi amesema hayo Januari 15, 2024 wakati akizungumza na watumishi wa kada mbalimbali wakiwepo uhamiaji, jeshi la polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania wilaya ya Ileje (TRA), afya, kilimo, na mifugo katika boda ya Isongole ambayo ni mpaka wa Tanzania ma Malawi huku akiwakumbusha majukumu yao ikiwepo kutoruhusu kuvushwa kwa magendo.
Mheshimiwa Mgomi amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kila mtu kusimamia majukumu yake kwa kusaidia mwingiliano huu ambao pia inasaidia kuimarisha uchumi.
Mheshimiwa Mgomi amesema mpaka huu wa boda ya Isongole wilayani hapa uwe chachu ya kuwasaidia wanaileje kunufaika kiuchumi kupitia ninyi wataalamu mliopewa dhamana ya kuhakikisha mnadhibiti viashiria vya magendo ambavyo vinasababisha kupiteza mapato ya serikali.
“Kila mtumishi kwa nafasi yake hapa mpakani awajibike ipasavyo na kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi waishio mpakani kutumia fursa ya mpaka huo kujiingizia kipato kwani asilimia kubwa wananchi wa Malawi wanatumia mpaka huo kufuata bidhaa Tanzania ikiwepo Isongole na Tunduma hivyo serikali kupata mapato na wafanyabiashara kujiongezea kipato. Ni jukumu letu kila mmoja tujipange vizuri kuhakikisha kwamba nchi zetu mbili zinabaki kuwa salama” amesema Mheshimiwa Mgomi.
Aidha DC Mgomi amesema kutokana na wilaya ya Ileje kupakana na nchi jirani ya Malawi, amewataka watumishi hao, kuimarisha usalama ,mahusiano ya ujirani mwema, kukusanya mapato ya serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara ili biashara zao ziweze kuwa na tija na hatimaye kusaidia ongezeko la mapato ya serikali.
Habari Picha na Ally Thabati
No comments:
Post a Comment