Thursday, 19 July 2018

WAZIRI JAFO AIBUA MAZITO KWA WASHIKAMKIA

Waziri wa tamisemi mh Jafo Selemani Jafo  amesema chanzo cha shule ya sekondari ya Jangwani kushika nafasi ya mwisho kwenye matokeo kidato cha sita ni walimu kutotimiza majukumu yao ikiwemo kuto andika notsi kwa  wanafunzi kutofundisha kwa uweledi na wengine kwenda kufundisha shule binafsi hivyo amemuagiza mkuu wa wilaya ya ilala mama Sofia Mjema kutoa walimu hao na kuwaleta walimu wapya amesema haya alivyotembelea shule ya sekondari ya Jangwani jijini Dar es salaam
wanafunzi wa shule ya Jagwani wakimsikiliza mh Jafo

SERA YA MAADILI NDO MWAROBAINI KABAMBE KWA WATUMISHI

Mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh Ali Hapi amesema sasa ni wakati muafaka kuanzishwa na kuwepo kwa sera ya taifa inayohusu maadili ili tupate sheria ambayo itawabana na kuhukumu viongozi na watumishi wa serikali  ambao wanakiuka misingi ya maadili kwenye kazi zao amesema haya kwenye mkutano ulioandaliwa na tume ya maadili kwa viongozi wa umma katika ukumbi wa Anatogo jijini Dar es salaam

MAGIZO YA WAZIRI WA ELIMU ,SAYANSI NA TEKNOROJIA YA VUTA HISIA NZITO

Naibu makamu mkuu wa chuo cha SUA(utawala wa fedha) prof,  Yonika Ngaja amesema maagizo yaliotolewa na waziri wa elimu wa sayansi na teknolojia prof Joyce Ndalichako ya vyuo vyote vifanye tafiti zenye kutatua matatizo ya jamii wamepokea na watatekeleza kwa vitendo pia vyuo ambavyo havijakidhi viwango na vigezo suala la kufutwa hatua vitachukuliwa kwa vyuo hivyo ilikupata wanafunzi bora  na elimu bora kwa lengo la kuelekea Tanzania ya viwanda lifanikiwe kwa kiasi kikubwa kuweza kupata wataalam wengi na wenye ujuzi amesema hayo wakati wakutoa neno la shukrani kwa waziri wa elimu,sayansi na teknolojia prof Joyce Ndalichako  wakatiwa kufungua maonyesho ya 13 ya vyuo vikuu ya siku nne kuanzia 18/07/2018 mpaka 20/07/2018 mnazi mmoja jijini Dar es salaam, habari picha na Ali Thabit
 

WADAU WA ASASI ZA KIRAIA, KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU WAKISHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE SERA MPYA

Wadau mbalimbali wakutana kwenye hoteli ya Wanyama iliyoko Sinza jijini Dar Es Salaam kwaajili ya kujadili sera mpya kwa asasi za kiraia kupitia kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu LHRC ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani ya Tanzania


ASASI ZA KIRAIA WATAKIWA KUUNGA MKONO SERA MPYA

Ismail Abdunuru Sulemani katibu mkuu wa asasi za kiraia nchini Tanzania zisizo za kiserikali amezitaka asasi zote nchini kuunga mkono jitihada na juhudi za serikali katika kubadilisha sera za asasi za kiraia kwa kushiriki katika utoaji wa maoni kwa lengo la kuondoa sera ya mwaka 2001 kwa kuleta sera mpya kwaajili ya kuendana na wakati wa sasa amesema haya kwenye mkutano ulioandaliwa na kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu LHRC uliofanyika sinza mori katika Wanyama hoteli jijini Dar es salaam.habari picha na Ali Thabit

WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO WAIPATANO SIDO

viongozi wa sido sabasaba
mjasiriamali Danius akiongea
Mjasiriamali Dainus Zabron Kaindi amesema amenufaika na elimu ya usindikaji wa mbogamboga za majani kupitia sido hivyo amewataka watanzania waweze kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na sido kwakuwa fursa hizo zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa watanzania katika wimbi la umasikini
mjasiriamali Lucia akiongea
Pia Lucia Cosmas amesema sido imemsaidia kwa kiasi kikubwa katika kutangaza bidhaa zake za furnituch kitaifa na kimataifa na amekiri waziwazi kuwa sido inaunga mkono adhima ya rais Magufuli kwa vitendo kuelekea Tanzania ya viwanda kwa kuwaibua na kuwainua watu wa viwanda vidogovidogo kwa kuwapa elimu,kuwatia moyo pamoja na masoko 




  wamesema hayo katika maonyesho ya 42 sabasaba Dar es salaam.                                  habari picha na Ali Thabit

SIDO YAWAFUTA MACHOZI WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO


mjasiriamali Merry akiongea na mwandishi
Mjasiriamali Merry kutoka sinza ameto shukrani zake kwa Sidokwakuweza kumtafutia masoko ya kuuza bidhaa zake za vipochi na bidhaa zingine anazotengeneza kwa shanga na ameweza kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya biashara ya kitaifa na kimataifa ambapo kumemjengea uwezo wa kibiashara na ameweza kunufaika kwa kukuwa kwa kipato cha uchumi wake pia ametowa wito kwa wafanyabiashara na watanzania wasisite kwenda sido kwa kupata elimu ya ujasiliamari 
baadhi ya bidhaa ya mjasiriamali Merry
Rasi Jeshi Beku akiongea na mwandishi wetu
Naye Rasi Jeshi Beku amesema sido ni mkombozi wa waanzilishi wa viwanda vidogovidogo hususa ni wanyonge na waliokata tamaa hili amelidhibitisha yeye baada ya kunufaika na elimu ya kutengeneza vikoi kutoka sido ambapo hapo awali alikuwa na malengo hayo lakini hakuwa na sehemu ya kuanzia hivyo ameshukuru na kuipongeza sido kwa kumuinua kwa namna moja au nyingine





wamesema hayo kwenye maonyesho ya biashara ya 42 sabasaba Dar Es Salaam habari picha na Ali Thabiti

Monday, 16 July 2018

BENKI KUU YA TANZANIA (B.O.T) YA ELEZA NAMNA YA KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI TANZANIA

Mchumi mwandamizi kutoka kurugenzi ya uchumi kutoka benki kuu ya Tanzania(B.O.T) mh Lusajo Mwamkemwa amesema wao wanajukumu lakudhibiti mfumuko wa bei wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa kushirikiana na ofisi ya taifa ya takwimu ambapo mfumuko wa bei unaweza kudumu kwa mwezi mmoja au miezi mitatu pia amesema mdhara ya mfumuko wa bei unaathiri maendeleo ya uchumi wa taifa.
Pia wao kama benki kuu huweza kusaidia njia mbalimbali kwaajili ya kudhibiti mfumuko wa bei  kwa kutoa elimu kupita redio,televesheni,magazeti na maonyesho mbalimbali ya kitaifa kama sabasaba na nanenane, amesama hayo kwenye maonyesho ya biashara ya 42 sabasaba jijini Dar es salaam habari picha na Ally Thabit

Tuesday, 10 July 2018

MKE WA RAISI MSTAAFU WA AWAMU YA NNE NCHINI TANZANIA ANENA MAZITO

Mke wa raisi mstaafu wa awamu ya nne nchini Tanzania mama Salma R Kikwete ameitaka jamii ya kitanzania kutowafungia ndani na kuwanyanyapaa watoto wenye ulemavu na badala yake wapeleke shule iliwapate elimu waweze kujikwamua kiuchumi na wasiwe tegemezi kwenye maisha yao, ameyasema haya wakati wa kukabidhii msaada mbalimbali katika shule ya msingi ya Uhuru Mchanganyiko iliopo manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam wakati wakipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa ubalozi wa Kuwait nchni kwaajili ya watoto wenye ulemavu shule ya msingi ya UHURU MCHANGANYIKO msaada huo uliwasilishwa na mh Jasem Al Najem barozi wa Kuwait nchini Tanzania  ambaye anamaliza muda wake Tanzania pia ameahidi ataendeleza ushirikiano wake na nchi ya Tanzania.habari picha na Ally Thabit
Mama Salma R Kikwete akitoneno wakati akipokea msaada katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam kulia mh Jasem Al Najem balozi wa Kuwait nchini Tanzania 

MHADHILI WA CHUO CHA KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE AWEKA MAMBO HADHARANI

Dkt Fillip Daninga ambaye ni mhadhili wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya mwalimu  nyerere amesema kuwa "lengo la luanzishwa kwa chuo hiki kuandaa vijana kuongoza nchi hii baada ya kupata uhuru wa Tanganyika ambapo waliweza kufundishwa na mpaka sasa wanafundisha maswala ya maadili,uadilifu,nidhamu,siasa na uchumi ili kuweza kupata viongozi bora ambapo lengo hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa"

Dkt Fillip Daninga akizungumza na mwanahabari katika maonyesho ya 42 ya biashara sabasaba Dar es salaam
Pia vilevile hakusita kutaja baadhi ya viongozi nguli ambao walinufaika na elimu hiyo akiwemo raisi mstaafu wa awamu ya nne mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,Mzee Kaduma,Mzee Fillip Mangula,mh Nape Nauye ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama Lindi na mh Isaya Mwita ambaye ni meya wa jiji la Dar Es Salaam
Hakusita kusema jinsi chuo kinavyo wafikia jamii kwa njia ya makongamano,matangazo ya radio na televisheni, kwa machapisho mbalimbali kwa njia ya vitabu,majarida na kielectronic pia wamejipanga kutoa elimu ya ngazi ya juu masters, amesemahayo kwenye maonyesho ya biashara 42 sabasaba Dar Es Salaam.habari picha na Ally Thabit

BUNGE YAJA NA MIKAKATI MIZITO MASHULENI


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa mheshimiwa RITA KABATI amesema "kwamba wameamua kuja na mpango maluum wa kutengeneza vyoo kwa kila jimbo moja kwa lengo kuwasaidia wanafunzi wa kike na wanafunzi wenye ulemavu kutopa shida mashuleni pindi wanavyokwenda kujisaidia vyoo"
 
mhs Rita Kabati akizungumza na mwanahabari katika maonyesho ya biashara 42 sabasaba, Dar es salaam.
Pia wameamua kuwatafutia fursa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu Bi Rita Kabati amewapongeza wabunge wa Tanzania kwa kuunga mkono hoja za watu wenye ulemavu pamoja na watoto wakike ambao hupitia kwenye changamoto mashuleni amesema hayo kwenye maonyesho ya  biashara ya 42 sabasaba ambayo yanaendelea jijini Dar Es Salaam wilaya ya Temeke. Habari picha na Ally Thabit

Thursday, 5 July 2018

WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOROJIA AWEKA HAZARANI MIKAKATI MIZITO

Wazirin wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO  amesema wamekuja na muongozo wa kuwatambuwa na kuwaweka pamoja wabunifu wadogowadogo na kuwafikia kwa ngazi ya halmashauri pia wameamua kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwenye bajeti ya mwaka huu kiasi cha zaidi ya bilioni30 kwaajili ya utafiti na ubunifu na mambo ya sayansi na teknorojia .Lengo kupata wataalam vifaa pamoja na mashine ili kufikia hazima Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati kama rais Magufuli anavyo elekeza  .Pia ametoa wito kwa tume ya sayansi na teknorojia kutumia fedha hizi kama inavyotakiwa. Pia ameipongeza tume ya sayansi na teknorojia kwa uhadilifu' uzarendo na kwa kwakufanya tafiti zenye tija kwa maslai ya Taifa na kwa kuandaa kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu


Habari picha na ALLY THABITI

WADAU WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAUNGA MKONO WABUNIFU

Wadau wa sayansi na teknorojia pichani wakionekana kuunga mkono jitiada zinazofanywa na serikali kwa kuanzisha muongozo wa kuwatambua wabunifu wadogowadogo na kuwafikia kwa ngazi ya halmashauri

habari picha na Ally thabiti

VIJANA WABUNIFU WATOA YA MOYONI KWA WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOROJIA

Mmoja ya kijana mbunifu amemuomba waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO wawawezeshe kwa hali na mali na kitaaluma ili wafikishe malengo yao ya kuwa wabunifu wa kimataifa  hamesema  aya alipotembelewa kwenye banda lake katika ukumbi wa mlimani city katika kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu baada ya kutembelewa na waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO

Habari picha na Ally Thabiti

WABUNIFU WAUNGA MKONO HAZIMA YA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

Pichani mwana mama akimuelezea waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO namna walivyo buni mashine mbalimbali  Lengo ni kumuunga mkono rais Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati .amesema haya kwenye kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu  kwenye ukumbi wa mlimani city jijini dar es salaam

habari picha na  Ally Thabiti