Monday, 29 April 2019

SHIRIKISHO LA WANASAYANSI CHIPUKIZI, WAJIVUNIA MAMBO MAZITO.

Na. Ally Thabiti

Mtendaji mkuu wa shirikisho la wanasayansi wanaochipukia, Dkt. Gosbert Kamugisha, amesema kuelekea miaka saba ya maonesho ya wanasayansi wanaochipukia wameweza kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na tafiti wanazozifanya kutatua changamoto za hapa nchini Tanzania hasa katika sekta ya teknolojia, afya, maji.

Dr. Gosbert Kamugisha, Mtendaji Mkuu Shirikisho la Wanasayansi Wanaochipukia


Pia imeelezwa kuwa  Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTEC) wametumia tafiti za vijana hao wanasayansi hadi kuwa mawazo ya kibiashara na wafanyabiashara wa sekta binafsi wamenufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na mawazo ya vijana hao.

Dkt. Kamugisha ameyasema hayo wakati wa mkutano na wanahabari jijini Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya mwisho ya maonesho ya saba ya wanasayansi wanaochipukia yanayotarajiwa kufanyika mwezi August mwaka huu wa 2019 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC)

Dkt. Kamugisha ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo, wameweza kuhamasisha vijana wa kitanzania katika shule za msingi na sekondari kupenda masomo ya sayansi.

No comments:

Post a Comment