Friday, 9 May 2025

WALIP MPIGA KATIBU MKUU BARAZA LA MAASKOFU WATIWA MBALONI

 Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam  Mulilo Jumanne Mulilo amethibitisha kuwa watu waliompiga na kumjeruhi Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Dkt Charese  Kitima wamekatwa na utaratibu wa kufikishwa Mahakamani unafanyika .

Ambako hivi karibuni eneo la Kurasini Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu nchini Tanzania majira ya saa nne ya usiku watu hawa walifika eneo hili na kumshambulia Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Habari na Ally Thabit 

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AIMIZA UTUNZAJI WA AMANI NA USALAMA WAKATI WA UCHAGUZI


 Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Tanzania Nyaoza awataka Wanachama,Wapenzi na Viongozi wa Vyama vya Siasa Kutunza na Kuilinda Amani iliyopo kipindi cha Uchaguzi na baada ya uchaguzi. 

Anesema haya kwenye mkutano mkuu wa chama cha NLD ambako chama hiki wanachama wake walipomchagua na kumpitisha Doyo Hassan Doyo  kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya urais ifikako mwezi wa kumi mwaka huu 1025 kwenye uchaguzi mkuu.

Habari picha na Ally Thabit Mbungo 

DOYO KUWA RAISI WA TANZANIA


 Doyo Hassan Doyo amesema Mwaka huu 2025 Katika Uchaguzi Mkuu Utakao Fanyika mwezi wa Kumi yeye ndiye atakayekuwa Rais wa Tanzania. Kupitia Chama cha NLD.

Kitu ambacho kinamfanya awe na uhakika wa kuwa Raisi kutokana na dira ya chama chake cha NLD ambako kusimamia Kilimo kwa kuwapa wakulima mbegu bora na za kisasa pamoja na kuwatafutia masoko ya kitaifa na kimataifa. Ugawaji wa mbolea na pembeje bule kwa wakulima . Kilimo cha kisasa kupitia umwagiliaji,Usimamizi bora kwenye sekta ya madini ambako atahakikisha kila mchimbaji anapata vifaa vya kisasa vya kuchimbia madini na kuweka bei elekezi, Utoaji wa resen kwa wazawa bila mashariti magumu.

Sekta ya Ajira .

Doyo Hassan Doyo Mgombea kiti cha urais kupitia chama cha NLD atahakikisha kila mtanzania anapata ajira ya kudumu,hatakuza sekta ya viwanda na upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na kuimarisha sekta ya Afya na upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa gharama nafuu.

Vile vile atakuza sekta ya Usafirishaji na Uchukuzi kwenye miundombinu ya majini ,nchikavu na Angani amesema haya baada ya kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya uraisi kupitia chama cha NLD . Hivyo amewataka watanzania wamchague Doyo Hassan Doyo  awe rais wa tanzania kupitia chama cha NLD. Kwani ccm walio ahixi hawajatekeleza hata moja .

Habari picha na Ally Thabit Mbungo 

WAZIRI WA AFYA WA ZANZIBAR AWATOA HOFU WATALII


 Nasoro Mazrui Waziri wa Afya wa Zanzibar amesema  wizara yake ya afya  inasimamia kikamilifu maswala ya Afya Zanzibar kwa kina na umakini mkubwa .Hivyo anawataka watalii kutoka nchi mbalimbali duniani wafike Zanzibar kufanya Utalii. Kwani Afya iko salama na imeimarika kwa Zanzibar na wakipata changamoto za kiafya mara nyingi wizara yake inawatibu bule.

Pia miundombinu ya kiafya imezidi kujengwa na kuimarishwa kwa Unguja na Pemba na Madaktali bingwa wapo wa kutosha .

Waziri wa Afya wa Zanzibar anawataka wazanzibar wakate bima za Afya.vilevile ameongeza kwa kusema  katika mwaswala ya watu wenye ulemavu zanzibar yanazingatiwa kwa kiasi kikubwa .Mfano Mashuleni kuna miundombinu rafiki na wezeshi kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa aina zote.

Kwa upande wa wanafunzi wasioona kuna maandishi ya nukta nundu pia kwa watu wenye ulemavu wakienda kupata huduma kwenye vituo vya Afya ,Zahanati, Mahospitalini na maeneo mengine wanapewa kipaumbele.

Habari picha na Victoria Stanslaus. 

BARAZA LA MITIHANI LAJIVUNIA ONGEZEKO LA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA

 Ndugu Wanahabari Mitihani ya Kidato cha sita ( ACSEE) na Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada imeanza tarehe 05 mei 2025 Tanzania Bara na Zanzibar. Mtihani wa Ualimu utakamilika tarehe 19 Mei,2025 na Kidato cha Sita tarehe 26 Mei,2025. Mtihani wa kidato cha sita utafanyika katika jumla ya shule za secondari 982 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 245. Aidha , Mtihani wa Ualimu  utafanyika katika Vyuo vya Ualimu 68.

USAJILI WA WATAHINIWA

(a) Watahiniwa wa Kidato cha Sita 

Jumla ya watahiniwa 134,390 wamesajiliwa kufanya mtihani wa  Kidato cha Sita 2025 ambapo watahiniwa wa shule ni 126,957 na  Watahiniwa wa Kujitegemea ni 7,433.

Kati ya Watahiniwa wa Shule 126,957 waliosajiliwa, wavulana ni64,581 sawa na asilimia 50.87 na Wasichana  ni 62,376 sawa na asilimia 49.13. Aidha  watahiniwa  wenye mahitaji maalum ni 453 ambapo kati yao weenye Uoni hafifu ni 300, wasioona ni 16, wenye Uziwi 58, wenye ulemavu wa akili ni 04 na wenye ulemavu  wa viungo vya mwili ni 75.

Kati ya  Watahiniwa wa Kujitegemea 7,433 waliosajiliwa,wavulana 4,782 sawa na asilimia 64.33 na wasichana ni 2,651 sawa na asilimia 35.67. Aidha Watahiniwa  wa Kujitegemea wenye mahitaji maalum wako 151 ambapo kati yao wenye uoni hafifu ni142 na wasioona ni 9.

Mwaka 2024 idadi ya watahiniwa wa Shule na Kujitegemea waliosajiliwa walikuwa 113,536. Hivyo, kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 20,854 (18.37) kwa mwaka 2025 ukilinganisha na mwaka 2014.

(b) Mtihani wa Ualimu

Jumla ya watahiniwa 10,895 wamesajiliwa kufanya mtihani wa Ualimu Mei 2025.

Kati ya watahiniwa hawa 3,100 ni wa ngazi ya Stashahada na 7,795 ni wa ngazi ya Cheti.kwa ngazi ya Stashahada, wanaume ni1,751 sawa na asilimia 56.48 na wanawake ni 1,349 sawa na asilimia 43.52. Aidha kwa ngazi ya Cheti watahiniwa 3,987 sawa na asilimia 51.15 ni wanawake .

Watahiniwa  wenye Mahitaji Maalum waliosajiliwa kufanya mtihani wa Ualimu 24.Kati yao 2 ni wenye Uoni hafifu kwa ngazi ya Stashahada; na 16 wenye uoni hafifu ,3 wasioona ,1uziwi,1Ulemavu wa viungo ni wa ngazi ya Cheti.

Mwaka 2024 idadi ya Watahiniwa wa Ualimu waliosajiliwa walikuwa 11,435. Hivyo, kuna upungufu wa jumla ya watahiniwa 540 (4.72) kwa mwaka 2025 ukulinganisha na mwaka 2024.

MAANDALIZI YAMEKAMILIKA PAMOJA NA KUSAMBAZWA KWENYE VITUO USIKA PAMOJA NA VITABU VYA KUJIBIA  NA NYARAKA ZOTE MUHIMU KWENYE MIKOA YOTE  KWA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR. 

Mitihani  wa kidato cha sita  ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kwani upima  maarifa .stadi na umahiri wa wanafunzi katika maeneo yote waliojifunza  kwa kipindi cha miaka miwili ya elimu ya secondari ya juu. Matokeo ya mtihani huu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga  na Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati katika fani mbalimbali za Utaalaam wa kazi kama vile Afya ,Kilimo,Ualimu,Ufundi na nyinginezo. Hivyo Mtihani huu ni muhimu sana kwa wanafunzi ,Wazazi na Taifa kwa ujumla.kwa upande wa mtihani wa Ualimu,mtihani hufanyika kwa lengo la kupata walimu makini ambao watafundisha  katika ngazi ya Elimu ya Msingi na Secondari.

WITO KWA KAMATI ZA MITIHANI,WASIMAMIZI,WAMILIKI WA SHULE NA JAMII

Wito kwa Kamati za Mitihani

Pamoja na Maandalizi yote muhimu yaliyofanyika  Kamati za Miitihani za Mikoa  na Almashauri ziakikishe kuwa usalama  wa Vituo vya Mitihani vinaimarishwa na kwamba Vituo hivyo vinatumika kwa mujibu wa Mwongozo uliotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania .Aidha , Wahaakikishe wasimamizi wote waliopangwa kusimamaia uendeshaji wa mtihani  katika kituo husika  wanafika kwa wakati katika vituo husika.

WITO KWA WASIMAMIZI

Baraza linatoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa kusimamia mitihani kufanya kazi yao kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu.Wasimamizi wahakikishe kuwa wanazingatia kanuni za mitihani, Tarabu na Miongozo ya Baraza la mitihani waliyopewa ili kila mtahiniwa apate haki yake.

Aidha ,wasimamizi wahakikishe watahiniwa wote wenye mahitajiamaalum wanafanya mitihani yao ipasavyo ili wapate haki zao za  msingi.Haki hizo ni pamoja na  kuwapa mitihani yenye  maandishi ya nukta nundu kwa watahiniwa wasio ona  na Maandishi ya kukuza kwa watahiniwa wenye uoni hafifu. Watahiniwa wote wenye mahitaji maalum waongezewe muda wa dakika 20 kwa kila saa kwa somo la Hisabatina dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine,kama kanuni za mitihanizinavyoelekeza .Wasimamizi wahakikishe watahiniwa wote wanafanya mitihani kwa muda ulio pangwa na katika hali ya utulivu.

WITO KWA WATAHINIWA

Baraza linaamini kuwa walimu na wanafunzi wamewaandaa vizuri katika kipindi cha miaka miwili ya secondari ya juu na kozu ya mafunzo ya Ualimu. Hivyo ni matarajio ya Baraza la mitihani kuwa kila mtahiniwa atafanya mtihani wake kwa kuzingatia kanuni za mitihani.Aida,Baraza halitarajii kuona mtahiniwa yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu. Mtahiniwa yeyote atakayebainiwa kufanya udanganyifu  kwa  Mitihani matokeo yake yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za Mitihani.

WITO KWA WAKUU WA SHULE  MA WAMILIKI WA SHULE NA VYUO

Baraza linawaasa Wakuu wa Shule na Wakuu wa Vyuo kutekeleza majukumu yao ya usimamizi kwa kuzingatia  mwongozo wa usimamizi uliotolewa na Baraza la Mitihani  na kuepuka kuingilia usimamizi wa watahiniwa ndani ya vyumba vya mitihani.

Aidha, Baraza linawaasa Wamiliki wa Shule  na Vyuo kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa  namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa mitihani hii.  Baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha pasipo shaka kuwa uwepo wake unahatqrisha usalama wa Mitihani.

WITO KWA JAMII

Baraza linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa katika kuhakikisha Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu mwaka 2015 inafanyika kwa amani na utulivu. Wananchi wanaombwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote asiyehusika na mitihani anaingia kwenye maeneo ya shule na vyuo katika kipindi chote chamitihani. Kwa kufanya hivyo,tutawawezesha  wanafunzi waliosajiliwa kufanya mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu Mei 2025 kwa amani na utulivu.

Haya yanesemwa na Katibu Mtendaji Dkt .Said A. Mohamed.

Habari na Ally Thabit Mbungo