Ndugu Wanahabari Mitihani ya Kidato cha sita ( ACSEE) na Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada imeanza tarehe 05 mei 2025 Tanzania Bara na Zanzibar. Mtihani wa Ualimu utakamilika tarehe 19 Mei,2025 na Kidato cha Sita tarehe 26 Mei,2025. Mtihani wa kidato cha sita utafanyika katika jumla ya shule za secondari 982 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 245. Aidha , Mtihani wa Ualimu utafanyika katika Vyuo vya Ualimu 68.
USAJILI WA WATAHINIWA
(a) Watahiniwa wa Kidato cha Sita
Jumla ya watahiniwa 134,390 wamesajiliwa kufanya mtihani wa Kidato cha Sita 2025 ambapo watahiniwa wa shule ni 126,957 na Watahiniwa wa Kujitegemea ni 7,433.
Kati ya Watahiniwa wa Shule 126,957 waliosajiliwa, wavulana ni64,581 sawa na asilimia 50.87 na Wasichana ni 62,376 sawa na asilimia 49.13. Aidha watahiniwa wenye mahitaji maalum ni 453 ambapo kati yao weenye Uoni hafifu ni 300, wasioona ni 16, wenye Uziwi 58, wenye ulemavu wa akili ni 04 na wenye ulemavu wa viungo vya mwili ni 75.
Kati ya Watahiniwa wa Kujitegemea 7,433 waliosajiliwa,wavulana 4,782 sawa na asilimia 64.33 na wasichana ni 2,651 sawa na asilimia 35.67. Aidha Watahiniwa wa Kujitegemea wenye mahitaji maalum wako 151 ambapo kati yao wenye uoni hafifu ni142 na wasioona ni 9.
Mwaka 2024 idadi ya watahiniwa wa Shule na Kujitegemea waliosajiliwa walikuwa 113,536. Hivyo, kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 20,854 (18.37) kwa mwaka 2025 ukilinganisha na mwaka 2014.
(b) Mtihani wa Ualimu
Jumla ya watahiniwa 10,895 wamesajiliwa kufanya mtihani wa Ualimu Mei 2025.
Kati ya watahiniwa hawa 3,100 ni wa ngazi ya Stashahada na 7,795 ni wa ngazi ya Cheti.kwa ngazi ya Stashahada, wanaume ni1,751 sawa na asilimia 56.48 na wanawake ni 1,349 sawa na asilimia 43.52. Aidha kwa ngazi ya Cheti watahiniwa 3,987 sawa na asilimia 51.15 ni wanawake .
Watahiniwa wenye Mahitaji Maalum waliosajiliwa kufanya mtihani wa Ualimu 24.Kati yao 2 ni wenye Uoni hafifu kwa ngazi ya Stashahada; na 16 wenye uoni hafifu ,3 wasioona ,1uziwi,1Ulemavu wa viungo ni wa ngazi ya Cheti.
Mwaka 2024 idadi ya Watahiniwa wa Ualimu waliosajiliwa walikuwa 11,435. Hivyo, kuna upungufu wa jumla ya watahiniwa 540 (4.72) kwa mwaka 2025 ukulinganisha na mwaka 2024.
MAANDALIZI YAMEKAMILIKA PAMOJA NA KUSAMBAZWA KWENYE VITUO USIKA PAMOJA NA VITABU VYA KUJIBIA NA NYARAKA ZOTE MUHIMU KWENYE MIKOA YOTE KWA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.
Mitihani wa kidato cha sita ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kwani upima maarifa .stadi na umahiri wa wanafunzi katika maeneo yote waliojifunza kwa kipindi cha miaka miwili ya elimu ya secondari ya juu. Matokeo ya mtihani huu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati katika fani mbalimbali za Utaalaam wa kazi kama vile Afya ,Kilimo,Ualimu,Ufundi na nyinginezo. Hivyo Mtihani huu ni muhimu sana kwa wanafunzi ,Wazazi na Taifa kwa ujumla.kwa upande wa mtihani wa Ualimu,mtihani hufanyika kwa lengo la kupata walimu makini ambao watafundisha katika ngazi ya Elimu ya Msingi na Secondari.
WITO KWA KAMATI ZA MITIHANI,WASIMAMIZI,WAMILIKI WA SHULE NA JAMII
Wito kwa Kamati za Mitihani
Pamoja na Maandalizi yote muhimu yaliyofanyika Kamati za Miitihani za Mikoa na Almashauri ziakikishe kuwa usalama wa Vituo vya Mitihani vinaimarishwa na kwamba Vituo hivyo vinatumika kwa mujibu wa Mwongozo uliotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania .Aidha , Wahaakikishe wasimamizi wote waliopangwa kusimamaia uendeshaji wa mtihani katika kituo husika wanafika kwa wakati katika vituo husika.
WITO KWA WASIMAMIZI
Baraza linatoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa kusimamia mitihani kufanya kazi yao kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu.Wasimamizi wahakikishe kuwa wanazingatia kanuni za mitihani, Tarabu na Miongozo ya Baraza la mitihani waliyopewa ili kila mtahiniwa apate haki yake.
Aidha ,wasimamizi wahakikishe watahiniwa wote wenye mahitajiamaalum wanafanya mitihani yao ipasavyo ili wapate haki zao za msingi.Haki hizo ni pamoja na kuwapa mitihani yenye maandishi ya nukta nundu kwa watahiniwa wasio ona na Maandishi ya kukuza kwa watahiniwa wenye uoni hafifu. Watahiniwa wote wenye mahitaji maalum waongezewe muda wa dakika 20 kwa kila saa kwa somo la Hisabatina dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine,kama kanuni za mitihanizinavyoelekeza .Wasimamizi wahakikishe watahiniwa wote wanafanya mitihani kwa muda ulio pangwa na katika hali ya utulivu.
WITO KWA WATAHINIWA
Baraza linaamini kuwa walimu na wanafunzi wamewaandaa vizuri katika kipindi cha miaka miwili ya secondari ya juu na kozu ya mafunzo ya Ualimu. Hivyo ni matarajio ya Baraza la mitihani kuwa kila mtahiniwa atafanya mtihani wake kwa kuzingatia kanuni za mitihani.Aida,Baraza halitarajii kuona mtahiniwa yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu. Mtahiniwa yeyote atakayebainiwa kufanya udanganyifu kwa Mitihani matokeo yake yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za Mitihani.
WITO KWA WAKUU WA SHULE MA WAMILIKI WA SHULE NA VYUO
Baraza linawaasa Wakuu wa Shule na Wakuu wa Vyuo kutekeleza majukumu yao ya usimamizi kwa kuzingatia mwongozo wa usimamizi uliotolewa na Baraza la Mitihani na kuepuka kuingilia usimamizi wa watahiniwa ndani ya vyumba vya mitihani.
Aidha, Baraza linawaasa Wamiliki wa Shule na Vyuo kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa mitihani hii. Baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha pasipo shaka kuwa uwepo wake unahatqrisha usalama wa Mitihani.
WITO KWA JAMII
Baraza linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa katika kuhakikisha Mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu mwaka 2015 inafanyika kwa amani na utulivu. Wananchi wanaombwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote asiyehusika na mitihani anaingia kwenye maeneo ya shule na vyuo katika kipindi chote chamitihani. Kwa kufanya hivyo,tutawawezesha wanafunzi waliosajiliwa kufanya mitihani ya Kidato cha Sita na Ualimu Mei 2025 kwa amani na utulivu.
Haya yanesemwa na Katibu Mtendaji Dkt .Said A. Mohamed.
Habari na Ally Thabit Mbungo
No comments:
Post a Comment