Doyo Hassan Doyo amesema Mwaka huu 2025 Katika Uchaguzi Mkuu Utakao Fanyika mwezi wa Kumi yeye ndiye atakayekuwa Rais wa Tanzania. Kupitia Chama cha NLD.
Kitu ambacho kinamfanya awe na uhakika wa kuwa Raisi kutokana na dira ya chama chake cha NLD ambako kusimamia Kilimo kwa kuwapa wakulima mbegu bora na za kisasa pamoja na kuwatafutia masoko ya kitaifa na kimataifa. Ugawaji wa mbolea na pembeje bule kwa wakulima . Kilimo cha kisasa kupitia umwagiliaji,Usimamizi bora kwenye sekta ya madini ambako atahakikisha kila mchimbaji anapata vifaa vya kisasa vya kuchimbia madini na kuweka bei elekezi, Utoaji wa resen kwa wazawa bila mashariti magumu.
Sekta ya Ajira .
Doyo Hassan Doyo Mgombea kiti cha urais kupitia chama cha NLD atahakikisha kila mtanzania anapata ajira ya kudumu,hatakuza sekta ya viwanda na upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na kuimarisha sekta ya Afya na upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa gharama nafuu.
Vile vile atakuza sekta ya Usafirishaji na Uchukuzi kwenye miundombinu ya majini ,nchikavu na Angani amesema haya baada ya kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya uraisi kupitia chama cha NLD . Hivyo amewataka watanzania wamchague Doyo Hassan Doyo awe rais wa tanzania kupitia chama cha NLD. Kwani ccm walio ahixi hawajatekeleza hata moja .
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
No comments:
Post a Comment