Nasoro Mazrui Waziri wa Afya wa Zanzibar amesema wizara yake ya afya inasimamia kikamilifu maswala ya Afya Zanzibar kwa kina na umakini mkubwa .Hivyo anawataka watalii kutoka nchi mbalimbali duniani wafike Zanzibar kufanya Utalii. Kwani Afya iko salama na imeimarika kwa Zanzibar na wakipata changamoto za kiafya mara nyingi wizara yake inawatibu bule.
Pia miundombinu ya kiafya imezidi kujengwa na kuimarishwa kwa Unguja na Pemba na Madaktali bingwa wapo wa kutosha .
Waziri wa Afya wa Zanzibar anawataka wazanzibar wakate bima za Afya.vilevile ameongeza kwa kusema katika mwaswala ya watu wenye ulemavu zanzibar yanazingatiwa kwa kiasi kikubwa .Mfano Mashuleni kuna miundombinu rafiki na wezeshi kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa aina zote.
Kwa upande wa wanafunzi wasioona kuna maandishi ya nukta nundu pia kwa watu wenye ulemavu wakienda kupata huduma kwenye vituo vya Afya ,Zahanati, Mahospitalini na maeneo mengine wanapewa kipaumbele.
Habari picha na Victoria Stanslaus.
No comments:
Post a Comment