Mkurugenzi Mtendaji Tgnp Liliani Liundi amesema tarehe 19 ya mwezi 3 mwaka 2025 rais Dr Samia ametimiza miaka minne ya uongozi wake kitendo hiki wanaharakati wanaopigania haki za binadamu kwao ni mafanikio makubwa kwani watu wengi waliamini kuwa mwanamke awezi kuiongoza nchi . Kupitia rais Dr Samia zana hii mbaya na potofu dhidi ya mwanamke imeweza kufutwa na kunjwa.
Pia Tgnp na wadau wanaopigania haki za binadamu wanampongeza rais Dr Samia baada ya kuapishwa alipohutubia bunge alisema atapigania na kuondoa mifumo dume, ataondoa mila na destuli potofu dhidi ya mwanamke na atawapa fursa mbalimbali wanawake na hili amelitekeleza kwa vitendo kwa kuwapa fursa mbalimbali wanawake kwenye sekta tofauti na amewafungulia milango ya uongozi . Pia amemtua ndoo mama kichwani kwa kuanzisha miradi ya maji, amewapigania maswala ya ardhi, amefanya maboresho ya sera ya ardhi ambako zamani mwanamke ananyimwa fursa ya kumiliki ardhi, kwenye sekta ya elimu amejenga madarasa, mabweni , matundu ya vyoo na amefanya maboresho dhidi ya mtoto wa kike akipata ujauzito baada ya kujifungua aweze kuludi shule na kuendelea na masomo, kuwainuwa wanawake kiuchumi kwa kuanzisha majukwaa mbalimbali na kuwapa mikopo nafuu.
Amesema haya kwenye viwanja vya Tgnp mabibo kwenye maadhimisho ya mwanamke duniani na uzinduzi wa ripoti ya miaka 30 ya tamko la Beijing nilipofanya nae mahojiano.
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment