Wakiri Msomi na Mkurugenzi wa Shule za St. Matthew's Dr Peter Tadeo Mtembei amesema tarehe 19 mwezi wa 3 mwaka 2025 rais Dr Samia ametimiza miaka minne ya uongozi wake .Katika miaka hii amekuza na kustawisha maridhiano, miundombinu mfano ujenzi wa SGR,Barabara , Madaraja na Upatikanaji wa Maji safi na salama kwa wananchi wote.
Pia rais Dr Samia ameanzisha miradi mipya na kukamisha miradi ilioachwa na mtangulizi wake. kupitia sekta ya elimu amejenga madarasa mapya, mabweni, ameajili waalimu, ujenzi wa nyumba za walimu na mabadiliko ya sera ya elimu ambako inamuwezesha mwanafunzi akimaliza elimu yake anaweza kujiajili ama kuajiliŵa.
Vilevile Wakiri Msomi na Mkurugenzi wa Shule za St. Matthew's Dr Peter Tadeo Mtembei amewataka wa'azi na walezi kuwaandikisha watoto wao kwenye shule zote nane za St Matthew's kwani shule zao zinatoa elimu bora nidhamu na usalama ni vitu vya msingi na wanavizingatia na ufahuru wa uhakika na wakiwango cha juu.
Ametoa rai kwa wahitimu 97 wa kidato cha sita kwenye shule ya St. Matthew's iliyopo mkoa wa wa pwani wilaya ya mkuranga kata ya mwandege katika maafari haya ya 20 kwa mwaka 2025 pindi wa wakimaliza mitihani ya taifa wakawe mabalozi wema , waendeleze maadili mema kwa jamii, tabia njema na watumie elimu walioipata kutatuwa changamoto za kijamii.
Pia amewasisitiza wazazi na walezi kwa elimu bora, nidhamu na usalama kwa wanafunzi na gharama nafuu za ada ni vyema wachague shule za St Matthew's kwani kupitia Maendeleo Bank wazazi na walezi watakopeshwa ada kwa riba nafuu ya asilimia moja .
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment