Saturday, 22 March 2025

BODI YA SUKARI YAJIVUNIA MAFANIKIO YA RAIS DR SAMIA KWA MIAKA MINNE


 Prof Keneth Bengesi Mtendaji Mkuu wa  Bodi ya Sukari  Tanzania amesema tangu tarehe 19 mwezi wa 3 mwaka 2021 baada ya Dr Samia  kuapishwa na kuwa rais wa tanzania  amewezesha sekta ya Sukari  kukuwa na kupiga hatuwa kwa kuwapa ruzuku wakulima wa miwa, kwa kufanya mabadiliko ya sheria ya NFRA kwa kupewa mamlaka ya kuhifadhi Sukari ambako mwanzoni wafanyabiashara wa sukari walikuwa wanaifadhi wenyewe na kupelekea ufichaji wa sukari na kusababisha kupanda kwa bei ya sukari olela olela na kupelekea usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa sukari  nchini tanzania. 

Ujenzi wa viwanda vya sukari na upanuzi wa viwanda vya zamani vya sukari. Prof Keneth Bengesi amesema rais Dr Samia  kwa kipindi cha uongozi wake wa miaka minne amekamilisha miradi yote ilioachwa na mtangulizi wake.mfano ujenzi wa bwawa la mwalimu nyerere, daraja la Kigongo busisi mwanza, ujenzi wa SGR, uwanja wa msarato jijini dodoma , amekuza demokrasia kwa kuwa nafasi viongozi wa vyama vya siasa kufanya mikutano yao kwa uhuru, maridhiano kwa kupitia farsafa yake ya R nne na kuwarejesha watu wote waliokimbia nje ya nchi.

Na mengineyo mengi ameyafanya rais Dr Samia ikiwemo kufunguwa fursa kwa wafabiashara, wasanii kwa kusafiri nao nje ya nchi kwaajili ya kuwatafutia masoko ya kitaifa na kimataifa , ameweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji kuwekeza kwenye sekta ya sukari na maeneo mengineyo.

Ametoa wito kwa watanzania waendelee  kumuunga mkono na mwaka huu kwenye uchaguzi wampe kura za kutosha rais Dr Samia  ili aendekee kuwa rais wa Tanzania hakika rais Dr Samia  mitano tena. 

Habari picha na Victoria Stanslaus 

No comments:

Post a Comment