Wednesday, 19 March 2025

MAENDELEO BANK YAJA NA CLICK BANK SMILE

 Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank Plc Prof Ulingeta Mbamba Azindua Huduma ya CLICK BANK SMILE amesema uzinduzi wa Internet Banking .

Amechukua fursa ya kuwapongeza kwa dhati Menejimenti na  wafanyakazi wa Maendeleo bank kwa juhudi kubwa walizofanya kuhakikisha  huduma hii mpya ya  inakamilika na kuzinduliwa kwa mafanikio.jitohada,maarifa,na kujituma kwao kumeifanya Maendeleo bank kuwa kinara wa ubunifu katika sekta ya kifedha amewaponeza sana .

Katika Ulimwenngu wa sasa wa kidigitali,benkiinayoendelea ni ile inayokwenda sambamba na teknolojia- Click Bank Smile ni jibu sahihi kwa mahitaji yawateja wa leo wanaotaka huduma za haraka ,salama na zinazoweza kupatikana mahali popote  na muda wowote .

Hivyo Matarajio ya huduma  hii itaongeza ufanisi wa biashara, hasa kwa wafannyabiashaara wadogo na wa kati na kuokoa muda na gharama za wateja  kwa kila kitu kinapatikana kwa mfuso wa kidole  kwenye simu au kompyuta.

Huu ni ushahidi kwa Maendeleo Bank Plc inatekeleza kwa vitendo mkakati wake wa ukuaji wa kidigitali na kufanikisha azma ya kuwa benki ya kisasa inayoendana na mabadiliko ya kiteknolojia.

Kwa Mujibu wa Fin-Scope Survey ya Mwaka 2023 kiwango cha upatikanaji na matumizi ya huduma rasmi za kifedha kiliongezeka hadi 89% na 76% mwaka 2023 kutoka 86% na 65% mwaka 2017". Hii ilichangiwa sana na uimarikaji wa huduma za kifedha kwa njia ya kidigitali na hasa huduma za kifedha kwa njia ya simu.

Hivyo ni Imani kuwa huduma  hii ya Internet banking  si tu kwamba itawanufaisha wateja wa Maendeleo Bank  tu bali pia itasaidia ukuaji wa uchumi wa wananchi kwa kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini. Kwa namna hii, Maendeleo Bank inachangia moja kwa moja katika malengo ya serikali , katika kuimarisha uchumi wa kidigitali na kuhakikisha wananchi wengi wanapata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi.

Pia ametoa wito kwa watanzania wote kutumia  huduma hii ya CLICK BANK SMILE  ili kujionea urahisi wake na manufaa yake .Hii ni huduma iliyoandaliwa kwa ajili yenu hivyo ni jukumu letu kuitumia kwa tija . 

Kwa heshima na taadhima ,sasa ameitangaza rasmi kuwa huduma ya Internet banking  ya Maendeleo Bank Plc -CLICK BANK SMILE- imezinduliwa rasmi, leo tarehe 18 mwezi wa tatu mwaka 2025 .PONGEZI KWA MAENDELEO BANK PLC!.

Habari na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment