Kwani Umeme huu unanunuliwa kwa gharama ndogo kwani umeme utasaidia mikoa ya kaskazini kupata umeme wa uhakika kwenye viwanda na maeneo wanayoishi wananchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Eng Felchesmi J. Mramba amesema tanzania itapata umeme huu kupitia kutoka Ethiopia kwa kutumia miundombinu ya Kenya kwani Kenya na Ethiopia zipo karibu . Serikali ya tanzania imefanya uhamuzi huu kwa sababu tunapoteza megawati kumi na saba za umeme kwa kutumia kupitisha umeme kwa njia za ndani ya nchi yetu Pia sera zetu zinaruhusu kununua umeme nchi za nje .
Mfano Mkoa wa Rukwa umeme unaotumika ni kutoka nchi ya Zambia ,Umeme unaotumika mkoa wa Kagera unatoka nchi ya Uganda hata nchi ya Ethiopia amnayo inatuuzia tanzania umeme licha ina megawati elfu sita lakini bado inanunua umeme nchi zinginezo na mpaka sasa nchi zipatazo tatu zimeleta maombi za kuuziwa umeme na tanzania na wamekubaliana na wapo hatua za mwisho nchi hizi ni Burundi,Rwanda na Zambia .
Na sasa Tanzania kwa Kushirikiana na Zambia wanatekeleza mradi wa Taza ambao megawati sita za umeme zitauzwa nchini Zambia na mradi umefikia asilimia hamsini .Nakampu ya Mifodi ya Zambia itanunua megawati mia moja tanzania nchi zinginezo zitazonunu umeme tanzania Msumbiji,Marawi,Dr kongo
Katibu Mkuu amesisitiza kuwa bei tunayouziwa umeme na nchi ya Ethiopia ni bei na fuu na rafiki kwani ni dora saba nukta saba sent .
Swala la Bwawa la Mwalimu Nyerere limeleta ukombozi katika kupatikana umeme wa kutosha nchini tanzania hivyo watanzania tuunge mkono uwamuzi uliofanywa na serikali yetu ya tanzania na tuendelee kumpongeza rais Dr Samia kwa kukamilisha bwawa la mwalimu nyerere na miradi mingineyo mpaka kuwezesha nchi kuondokana na tatizo la kukatikakatika umeme mara kwa mara.
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment