Wednesday, 4 October 2017
MKUU WA WILAYA AWATANGAZIA KIAMA MATAPELI
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ALLY HAPI amesema atawachukulia atuwa kali matapeli wanao zulumu ardhi na nyumba za wajane pia amewataka madarali wote kuacha utapeli .Pia amewataka viongozi wa kata zote za wilaya ya Kinondoni wawatumikie wananchi wao vizuri asa wanyonge na wawafichue matapeli wote . ametoa rai kwa wakuu wa idara mbalimbali kufanya kazi kwa bidii amesema haya wakati wa kukabiziwa ripoti za idara mbalimbali ofisini kwake
habari picha na VICTORIA STANSLAUS
habari picha na VICTORIA STANSLAUS
MIFUGO NI SHIDA WILAYA YA KINONDONI
Kiongozi wa idara ya mifugo wilaya ya Kinondoni amesema mifugo inazulura mno na kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira wilaya ya Kinondoni. amemuomba mkuu wa wilaya ya Kinondoni ALLY HAPI awatafutie eneo ili wakikamata mifugo wapate sehemu ya kuiweka .licha ya kuwapa elimu wafugaji jinsi ya kutunza mifugo yao lakini awatekelezi ipasavyo
habari picha na ALLY THABITI
habari picha na ALLY THABITI
IDARA YA MAZINGIRA WILLAYA YA KINONDONI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI
Kiongozi wa usafi na mazingira wilaya ya Kinondoni ABILLU PETER amesema ukosefu wa dampo,magari ya kubebea takataka na uhaba wa vifaa ni kikwazo kikubwa katika wilaya yake ya Kinondoni juu ya kusafisha mazingira .amemuomba mkuu wa wilaya ya Kinondoni ALLY HAPI kuwawezesha kipesa na kupata eneo la dampo ili wafanye kazi zao kwa wepesi . amesema haya wakati wa kutoa tathimini ya ali ya usafi wa mazingira mbele ya mkuu wa wilaya ya kinondoni ALLY HAPI ofisini kwake
habari picha na ALLY THABITI
habari picha na ALLY THABITI
IDARA YA AFYA KUIPAISHA KINONDONI
Afsa afya JOHN KIJUMBE amesema wamejipanga kikamilifu katika idara yao ya afya kwa kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu wilaya ya Kinondoni kwa kufukia madimbwi ya maji, kutoa elimu na kupulizia dawa vyooni.pia wanamipango ya kukusanya kiasi kikubwa cha pesa kwa watakao kiuka sheria za afya . Ivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa mapato wilaya ya Kinondoni amesemaa haya wakati wa kuto tathimi ya afya wilaya ya Kinondoni mbele ya mkuu wa wilaya ya Kinondoni ALLY HAPI ofini kwake
habari picha na VICTORIA STANSLAUS
habari picha na VICTORIA STANSLAUS
GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA AZITOLEA UVIVU SEKTA ZA KIBENKI
Gavana wa benki kuu ya Tanzania [ BOT] BEENO NDURU amezitaka sekta za kibenki zilizopo Tanzania ziwafikie wananchi wa ali za chini kwa kuwapa mikopo yenye mashariti nafuu. Pia zifanye tafiti kwenye kilimo kwaajili ya kupata matatizo yanayowakabili wakulima . Lengo kumuunga mkono rais MAGUFULI kuelekea Tanzania ya viwanda
habari picha na ALLY THABITI
habari picha na ALLY THABITI
WATANZANIA WAASWA JUU YA FEDHA ZAO
Mkurugenzi mtendaji sekta za kibenki amewataka watanzania waache tabia ya kuweka pesa zao kwenye majumba yao badala yake wapeleke benki kwaajili ya usalama
habari picha na ALLY THABITI
habari picha na ALLY THABITI
Subscribe to:
Posts (Atom)