Sunday, 17 January 2021
BARAZA LA MITIHANI LAPONGEZA
katibu mtendaji wa baraza la mitihani Dr. Charles Msombe amesema ufaulu wa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 5.19 kwa kidato cha nne hivyo amewapongeza wanafunzi, walimu, wazazi na walezi, pamoja na walimu wakuu kwa kuweza kuwasimamia vijana wao huku baraza likiwafutia matokeo wanafunzi 215 kwa udanganyifu.
Habari picha na Ally Thabith
MKURUGENZI WA TBS AMEAHIDI MAZITO
Yusuph Othaman Ngenya Mkurugenzi mkuu wa TBS amemwambia waziri wa viwanda na biashara Geofrey Mwambe kuwa yeye na watendaji wengine wa TBS wanatekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo yanayotolewa na waziri GEOFREY MWAMBE pia amewatoa hofu wajasilia mali wadogowadogo kuwa milango ya tbs iko wazi.
Habari na Ally Thabith
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATOA NENO KWA TBS
Jofery Mwambe waziri wa viwanda na biashara ameutaka uongozi wa TBS kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogowadogo na kupunguza muda wa kutoa vibali kutoka miezi sita (6) mpaka miezi mitatu (3) na vile vya mwaka bila kupunguza pia Tbs itengez biashara kwa watanzania. Amesema haya alivyofanya ziara makao makuu ya TBS kama inavyoonekana pichani akiwa na ndani ya Maabara za TBS jijini Dar es Salaam.
Habari picha na Ally Thabith
Thursday, 7 January 2021
GOBA MARASONI KUNUSURU VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO
Mwenyekiti wa mbio za Goba Marasoni Benson Luwoga ameishukuru NIC kwa kuifadhili miaka mitatu Goba Marasoni kwani ufadhili wao utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii ambako fedha za mwaka huu zitakazo patikana kupitia Goba Marasoni zitakwenda kupunguza vifo vya Wamama Wajawazito na Watoto wakati wa kujifungua.
Ambako kauli mbihu mwaka huu inasema kimbia kwa kuboresha maisha ya mama na mtoto ambako tarehe 30/01/.2021 kutakuwepo na mbio za Goba Marasoni ambako washiriki watakuwa 2000 pia mbio hizi zinasaidia watu kuimarisha afya zao na kuepukana na marazi nyemerezi yasio ambukiza Mfano Kisukari.
Benson Luwoga ametoa wito kwa taasisi na wadau wengine kujitokeza kwa wingi kuzamini mbio hizi za Goba Marasoni
Habari Picha na
Ally Thabiti
NIC YAMWAGA MAPESA KWA GOBA MARASONI
Mkurugenzi wa shirika la Bima nchini Tanzania (NIC) Elirehema Doriye asema wameamua kuwa wazamini wa mda wa miaka mitatu kwenye goba marasoni rengo kuunga mkono juhudi za Raisi Magufuli na kutekeleza ibara ya Nane ya chama cha Mapiduzi katika kukuza ajila kwa vijana amesema wameanza kutoa kiasi cha Shilingi Milioni Ishirini na Tano (Tsh. 25,000,000/=) kwa mwaka huu mmoja ila kiwango cha pesa kitazidi kukuwa kila mwaka
Habari Picha naAlly Thabiti


