Sunday, 15 January 2023

WAZIRI WA ARDHI ATOA ONYO KWA KAMPUNI ZA UPIMAJI

 Angelina Mabula waziri wa ardhi nyumba na makazi amezifungia kampuni saba na zingine kumi na tano za upimaji ardhi kushindwa kutekelezwa mikataba.

Habari kamili na Ally Thabith

Thursday, 22 December 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kufunga geti li maji yaweze kujaa katika Bwawa la Mwalimu Nyerere hii leo Desemba 22, 2022.

Tanzania tunaweza kujifanyia mambo makubwa wenyewe: Rais Samia

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mradi wa ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere unatoa taswira kuwa Watanzania wanaweza kujitengenezea mambo makubwa wao wenyewe bila kupata msaada kutoka sehemu nyingine.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Desemba 22, 2022 mara baada ya kushuhudia tukio la ujazaji maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere na kuongeza kuwa licha ya uwepo wa changamoto kadhaa lakini hii leo nchi inaingia katika historia ambayo ilitarajiwa na kusubiriwa kwa muda mrefu.

Habari picha na Ally Thabit

WAZIRI WA NISHATI ATOA NENO KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA


Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa ni mchango mkubwa katika kufanikisha mradi wa ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), kutokana na kujipanga na kuulinda tangu awali hadi kukamilika kwake.

Makamba ameyasema hayo hii leo Desemba 22, 2022 wakati akiongea katika tukio la ujazaji maji Bwawa la Mwalimu Nyerere ambao utashuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Vyama, Serikali na Wananchi, huku ukitarajiwa kusaidia uchumi wa nchi.

Habari picha na Ally Thabith

WAZIRI WA NISHATI AWEKA HISTORIA

 Amesema haya tarehe 19/12/2022

Waziri wa nishati January makamba nilipo muhoji tarehe 19/12/2022 alisema ifikapo tarehe 22.12.2022 Tanzania itaweka historia kwa kuweza kujaza maji kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere hatimaye historia hiyo imeandikwa rasmi.

habari kamili na Ally Thabith

LATRA YAJADILI BEI YA TRENI YA UMEME

 





Habari picha na Ally Thabith

WAZIRI MKUU ATOA NENO KWA TANAPA

 


Waziri mkuu Kassim Majiliwa Kassim ameitaka Tanapa kutangaza mafanikio wanayoyapata.

habari kamili na Ally Thabith