Tuesday, 9 May 2023

UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO MKOANI MANYARA


 Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Manyara  watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Manyara. Upimaji huo utaenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani yatakayofanyika  tarehe 17/05/2023.

Upimaji huo utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 15/05/2023  hadi tarehe 19/05/2023  saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Manyara.

 

Kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

 

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.


Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayebainika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0768408984 Vailine Osward na 0714956529 Abubakar Mjaka.


        • “Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.


Habari Picha na Ally Thabiti

 


WADAU WAKUTANA NA KUWEKA MIKAKATI YA KUENDELEZA KILIMO BIASHARA

 


SEKTA ya kilimo bado inazo fursa mbalimbali ambazo zikitumika ipasavyo zitawezesha uchumi wa nchi kukua sambamba na kuzalisha ajira nyingi kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, wakati akifungua kongamano kuwajengea uwezo wakulima kuhusu kilimo biashara lililoandaliwa na ubalozi wa Uholanzi nchini na kufanyika mjini Dodoma, likiwa linawashirikisha wakulima na wadau mbalimbali katika sekta hiyo.

Kwa upande wake,Balozi wa Uholanzi nchini,Mh. Wiebe De Boer, alisema Serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ili izidi kukua na kuongeza uchumi.


Balozi wa Uholanzi nchini, Mh.Wiebe De Boer, akibadilishana mawazo na Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe ,muda mfupi kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.

Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe. akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa wa Uholanzi nchini,Mh.Wiebe De Boer baada ya kufungua kongamano la kuendeleza kilimo biashara nchini.

Habari Picha na Ally Thabiti

Kanisa Lahukumiwa Kulipa Milioni 70 Kwa Kosa La Gari Kugonga Na Kusababisha Kifo

 


Njombe

MAHAKAMA ya hakimu Mkazi Njombe imelihukumu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini kulipa fidia ya shilingi Milioni 70 baada ya gari mali ya kanisa hilo kugonga na kusababisha kifo cha marehemu Kaselida Mlowe wa mjini Njombe.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Njombe Lihad Chamshama amesema mdaiwa namba mbili ambaye ni kanisa anahukumumiwa kulipa fidia ya milioni 70 kutokana na uzembe uliofanywa na mdaiwa namba moja bwana Rajab Kitwana ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo wakati ikitoka mjini Makambako kwenye matengenezo na kusababisha kifo cha Marehemu Kaselida.

Aidha Mahakama hiyo imetoa jukumu kwa kanisa kulipa ghalama zote za uendeshaji wa kesi iliyoendeshwa kwa zaidi ya miaka miwili mpaka sasa huku ikitoa haki ya kukata rufaa kwa kanisa dhidi ya hukumu hiyo.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama kutokana na kesi No 2 ya mwaka 2022 ya madai ya fidia ya Milioni 100 dhidi ya kanisa la KKKT iliyofunguliwa na Siglada Mligo msimamizi ambaye ni msimamizi wa mirathi wa marehemu Kaselida Mlowe baada ya kifo kilichotokana na ajali ambapo marehemu aliacha wategemezi wakiwemo watoto wake watatu.

Kesi ilifunguliwa baada ya msimamizi wa mirathi kushinda kesi No 6,2021 ya makosa ya usalama barabarani kutokana na ajali iliyotokea eneo la Kibena Mlima wa Ichunilo mjini Njombe hapo September 25,2020 baina ya Hiace Namba T 298 DNE na gari NO T 210 - AHU Mercedes Benz Track mali ya kanisa na kupelekea kifo cha Kaseleida Mlowe.

Kesi hiyo imeendeshwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe Lihad Chamshama huku upande wa madai ukiwakilishwa na mawakili watatu akiwemo Emmanuel Chengula,Frank Ngafumika na Gervas Semgabo huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Marco Kisakali.

Habari na Ally Thabiti

DAWASA AWATAKA WATEJA WAAO KULIPA BILLS

 Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa Dawasa Kiula Kingu amewataka wateja wa Dawasa kulipa bills kwa wakati na kulinda miundo mbinu ya maji.

Habari na Ally Thabiti

OCEAN ROAD KUNUSULU VIFO VYA WAGONJWA WA SALATANI

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dr. Julius Mwaiselage amesema kwa kushirikiana na wabunge na umoja wa cheif Tanzania watacheza mchezo wa mpira wa miguu mjini Dodoma kwenye uwanja wa jamuhiri tarehe 27/05/2023 kati ya wabunge na machief lengo kukusanya kiasi cha shilingi milion mia tatu (Tsh. 300,000,000/=) kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa salatanu hospitali ya Ocean Road. Dr. Julius Mwaiselage ametoa wito kwa Taasisi,makampuni na mashirika na watu binafsi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia kiasi cha milioni mitaatu, kwani kitaenda kuokoa wangonjwa wa salatani wapatao mia moja. 

Pia kuanzia tarehe 25/05/2023 mpaka tarehe 28/05./2023 kutatolewa chanjo na elimu ya lishe ambapo Hospitali ya Ocean Road itawafikia watu wenye ulemavu wa aina yote kama wanavyofanya siku zote.


Habari na Ally Thabiti

RAIS SAMIA AWAFUTA CHOZI WAKAZI WA MAGOMENI KOTA

 Mkurugenzi mkuu mtendaji wa wakala wa majengo Tanzania (TDA) DAUDI KANDOLO amesema Rais wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassani ametoa maelekezo kwa watu wanaoishi kwenye nyumba za magomeni kota wakae miaka thelasini ambako miaka mitano watakaa bule na miaka Ishirni na Tano kwa mtu mwenye chumba kimoja atanunua kwa shilingi milioni arobaini na nani nukta tano na kwa mtu anaishi kwenye vyumba viwili atalipa kiasi cha milioni Amthini na sita nukta nane. Daudi Kandolo amesema kwa wasioweza kulipa watoe taarifa lakini watakaa bure kwa miaka mitano.

Habari  na Ally Thabiti

Tuesday, 2 May 2023

WIZARA YA FEDHA YAKUTANA NA IFC

 1. Wageni waalikwa , Mabibi na Mabwana;

2. Ni heshima kubwa kuwepo hapa leo kuongoza warsha hii muhimu inayohusisha miradi

inayotarajiwa kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP, ambayo inalenga sekta za Nishati pamoja na

Uchukuzi. Sekta ya Nishati na Uchukuzi ni muhimu kwenye ukuaji wa uchumi na maendeleo

katika nchi zinazoibukia kiuchumi kama Tanzania. Kuwekeza katika sekta hizi kupitia Ubia kati

ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kunaweza kuweka mazingira mazuri ya ukuaji wa kiuchumi

na maendeleo.

3. Mabibi na Mabwana, tunaweza kuendeleza na kuboresha miundombinu ya usafirishaji

kupitia- utaratibu wa PPP, kutoa fursa za ajira pamoja na masoko ya kibiashara . Hii, kwa

upande wake, itasaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma, pamoja na kuchochea

shughuli za kiuchumi. Zaidi ya hayo, tunaweza kutoa nishati ya kuaminika na ya bei nafuu

kwenye maeneo ya majumbani, biashara, na viwanda.

4. Kwa pamoja, tunaweza kutumia utaalamu na rasilimali za sekta ya Umma na sekta

Binafsi ili kuongeza ufanisi. Warsha hii inaashiria hatua kubwa katika kutambua na kuendeleza

miradi ya PPP ambayo italeta manufaa ya kudumu kwa wananchi wa Tanzania.

Kuendeleza miundombinu kunahitaji uwekezaji mkubwa ambao unaweza kuwa mzigo mkubwa

kwa serikali, haswa wakati hazina ya nchi inapokua ndogo, na kiwango cha deni la taifa likizidi

kuongezeka . Kwa kuzingatia changamoto hizi, ushirikishwaji wa sekta binafsi umezidi kuwa

muhimu ili kuisaidia serikali kwa kuwekeza kwenye miundombinu.

5. Zaidi ya hayo, kutokana na kukua na kubadilika kwa uchumi wa dunia,utaalam na

teknolojia unahitajika ili kuchochea maendeleo ya miundombinu. Ubia kati ya Sekta ya Umma

na Binafsi (PPPs) hutoa fursa nzuri ya kutumia rasilimali na utaalamu wa sekta binafsi. Kwa

kushirikiana na Sekta Binafsi, tunaweza kutumia mitaji yao, teknolojia na maarifa itakayosaidia

ukuaji wa miundombinu muhimu na huduma zinazohitajika nchini kwetu. PPPs zinaweza

kufungua fursa mpya za ukuaji wa uchumi na maendeleo kiujumla.

6. Naipongeza Idara ya PPP iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa warsha

hii ya kimkakati kwa ajili utekelezaji wa miradi ya PPP,vileile Nimeridhishwa na maandalizi

yaliyofanyika kwenye warsha hii. kama Katibu Mkuu wa Wizara, naahidi kuiunga mkono idara

na kuiwezesha kila itakapo hitajika ili kuhakikisha mipango yake inafanikiwa.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba wakati Kituo cha PPP kinatumika kama mratibu,

jukumu la kuandaa miradi na kukusanya rasilimali liko chini ya Mamlaka za usimamizi, kwa

msaada wa serikali chini ya Wizara ya Fedha.


7. Vile vile, ningependa kutoa shukrani ya dhati kwa Benki ya Dunia na IFC, washirika wetu

wa muda mrefu na wawezeshaji. Ushirikiano wenu umekuwa wa thamani sana kwa maendeleo

ya PPP nchini Tanzania, kuanzia hatua za awali hadi uundaji na marekebisho ya mifumo yetu ya

PPP. Utaalam wa kiufundi, na usaidizi wa kifedha umekuwa muhimu katika kuweka msingi

thabiti wa mafanikio kwenye utelezaji wa miradi ya PPP.

8. Kwa kipindi hiki , miradi inayotarajiwa kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP imeandaliwa,

bila kusahau msaada wa marekebisho ya Sheria ya PPP. Zaidi ya hayo, tunashukuru sana

msaada wa Benki ya Dunia kwenye mchakato wa marekebisho ya Sheria ya PPP hapa nchini.

Ninashukuru kwa msaada wa Benki ya Dunia katika uundaji wa Kituo chetu cha PPP, ikijumuisha

uanzishaji wa miongozo mbalimbali ya uendeshaji. Tunatambua juhudi na ari kubwa

inayohusika katika kazi hii.

Warsha hii itaongeza chachu ya ushirikiano mzuri kati ya Idara ya PPP na IFC. Juhudi zetu za

pamoja zimesababisha warsha hii yenye mwelekeo wa vitendo, ambayo inaashiria hatua

muhimu ya kusonga mbele katika mpango wa utekelezaji wa miradi nchini kwa utaratibu wa

PPP.

9. Wakati wa vikao hivi vya kazi, tutafaidika kutokana na uzoefu mzuri wa sekta ya Nishati

na Uchukuzi, tukitumia mafunzo tuliyojifunza, na mikakati iliyoandaliwa kutokana na miradi

yenye mafanikio. Lengo ni kubainisha hatua za kiutendaji za kufikia malengo katika FYDP III.

10. Ni matumaini yetu kwamba majadiliano katika warsha hii yatatoa mpango kazi mzuri

kwa kila kundi la washiriki, ikijumuisha Benki ya Dunia, IFC, Idara ya PPP, Wizara za Nishati na

Uchukuzi, na Mamlaka za Usimamizi . Hii ni juhudi shirikishi, na jukumu letu kama waratibu

litaendelea kuwa muhimu hadi tutakapotoa miradi ya PPP ambayo inakidhi viwango vya juu,

ambavyo tumejiwekea wenyewe chini ya FYDP III.

Utayari wao na ushiriki wao kamili katika kikao hiki bila shaka utatoa matokeo mazuri, sio tu

katika suala la matokeo ya mradi wa PPP wa kuahidi lakini pia katika kusikia uzoefu na utaalamu

kutoka kwa wataalamu wa kiufundi wa IFC kuhusu suala hilo. Kwa hiyo, nawaomba kuchukua

fursa hii kuuliza maswali yote, hasa yale ambayo yanajikita katika uundaji wa miradi ya PPP na

namna ya kugharamia miradi husika.

11. Napenda pia kuchukua fursa hii kutoa pongezi zangu kwa Mamlaka za usimamizi kwa

kuibua baadhi miradi ya PPP na Kuwa wa kwanza kuchukua hatua.

Warsha hii inazingatia sekta za usafiri na nishati, ambazo hupokea sehemu kubwa ya bajeti ya

maendeleo. Hata hivyo, tusisahau kwamba mustakabali wa nchi yetu unategemea mabadiliko

ya sekta mbalimbali na huduma za kijamii. Haja ya miundombinu thabiti ni muhimu katika

kufikia mabadiliko haya.


12. Kutokana na utimilifu wa jukumu muhimu la miundombinu thabiti katika kuleta

mabadiliko ya viwanda na huduma za jamii, Tanzania ilijiwekea malengo madhubuti ya kufadhili

Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Tatu, ambapo TZS 21.03 trilioni zitapatikana kutoka sekta

binafsi na shilingi bilioni 9 kupitia PPPs.

13. Kwa vile hiki ni kiasi kikubwa cha fedha, ni lazima tuhakikishe mbinu iliyoratibiwa ni

thabiti kwenye utekelezaji wa miradi ya PPP. Wakati Wizara ya Fedha na Idara ya PPP ina

jukumu la kutekeleza, kazi iliyopo inahitaji ushirikishwaji wa wizara za kisekta na mamlaka za

usimamizi. Warsha hii, inayolenga sekta ya Nishati na Uchukuzi, inaashiria hatua ya kwanza

katika safari hii, na warsha kama hizi zimepangwa kufanyika kwa sekta nyingine katika siku za

usoni.

14. Tunafahamu kikamilifu changamoto zilizopo katika kufanikisha mpango wetu kabambe.

Kwa hiyo, tunarekebisha mifumo yetu ya kisheria ili kuweka mazingira mazuri zaidi ya kuvutia

mtaji wa Sekta Binafsi. Hata hivyo, tunatambua pia hitaji la dharura la kuanzisha Kituo cha PPP

na dhana zake za uendeshaji, ikijumuisha Mfuko wa Uwezeshaji wa PPP pamoja na miongozo

yake. Zaidi ya hayo, ili kuhakikisha kwamba maafisa wetu wa PPP na timu za usimamizi wa

miradi wanapata ujuzi unaohitajika wa kiutaalam, tunahitaji kuweka kipaumbele katika kujenga

uwezo kuwaunga mkono kwa kuhudhuria mafunzo mbalimbali juu ya utaalam wa PPP na

kupata uthibitisho wa kitaalamu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Kibinafsi (CP3P).

15. Pia nimechukua hatua za kuharakisha mchakato wa kuweka muundo wa PPP chini ya

kila Wizara na Mamlaka za Usimamizi. Lengo ni kufafanua kwa uwazi majukumu na wajibu wa

maafisa wa PPP katika ngazi zote. Ili kufanikisha hili, nimewasiliana na Sekretarieti ya Ajira

katika Utumishi wa Umma na kuwaomba walipe kipaumbele suala hili.

16. Warsha hii inaashiria hatua muhimu katika juhudi zetu za kuunda mpango wa PPP

ulioratibiwa na thabiti nchini Tanzania. Ni muhimu katika kufikia malengo yetu ya maendeleo ya

kitaifa, haswa katika sekta ya uchukuzi na nishati. Kupitia PPPs, tunaweza kuunda msingi wa

ukuaji endelevu na shirikishi ambao utanufaisha wananchi wote.

17. Tunalenga kuweka mazingira mazuri ambayo yanavutia uwekezaji wa sekta Binafsi na

kusaidia maendeleo ya kiuchumi. Nina imani kuwa tunaweza kufikia malengo kupitia ushirikiano

wetu na IFC na kuendeleza programu ya PPP yenye mafanikio kwa ajili ya manufaa ya Taifa.

18. Asanteni nyote kwa kuhudhuria, na ninatarajia warsha yenye tija.

Habari na Ally Thabiti