Monday, 7 July 2025

PICHANI NAMNA YA JOSEPH JOACHIM MTEI


Kama inavyoonekana  Pichani Kijana  Joseph Joachim  Mtei hii ndio njia ambayo anatumia kuchora ramani za majengo ambako chuo cha Veta  Dodoma  ilivyoweza kumpa mbinu ya kuchora ramani kupitia miguu yake, Joseph Joachim Mtei anawataka watu watembelee kwenye banda la Veta ndani ya viwanja  vya Sabasaba kwenye maonyesho  ya 49 jijini dar es salaam. 

Lengo wajifunze namna  ya watu wenye ulemavu  wanavyofanya kazi zao na Veta walivyoludisha tumaini la watu wenye ulemavu  katika maisha yao .

Habari picha na Victoria Stanslaus 

VETA YAIBUA VIPAJI VYA WATU WENYE ULEMAVU


Joseph Johachim Mtei  ni Kijana  Mwenye  Ulemavu  wa Viungo ambae Veta imempa  Mafunzo ya Uchoraji wa Ramani mafunzo haya anapata mkoani Dodoma, Joseph amesema lengo lake anataka awe Mwandisi wa kucora ramani za majengo Licha yakuwa na changamoto ya mikono Joseph  ndoto zake na ndoto zake zimeweza kuibuliwa na Chuo cha Veta Dodoma ambako anachora ramani za majengo kupitia Miguu.

Ameishukuru Veta kwakuweza kuibua matumaini yake ya maisha yake na kukamilika kwa ndoto zake. 

Ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watu wenye Ulemavu Veta amesema haya kwenye  banda la Veta  ndani ya viwanja  vya Sabasaba kwenye maonyesho ya 49 Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. 

Habari picha na Victoria Stanslaus 

Saturday, 5 July 2025

SIDO YAPONGEZWA KWA MKAA MBADALQ


Bi Fatma ameipongeza Sido na Kuishukuru kwa kuweza kumpa mafunzo ya kutengeneza Mkaa Mbadala ambao auchafui mazingira na gharama yake nafuu .Bi Fatma anawataka watu wote nchini tanzania watumie mkaa mbadala kwani ni nishati safi na salama kwa kupikia na ambayo aichafui mazingira Pia aina madhara kwenye mwili wa binadamu, Bi Fatma ametoa wito kwa watu wote kufika kwenye banda la Sido kununua mkaa mbadala kwani ni nishati safi ya kupikia na inapatikana ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye maonyesho  ya 49 yanayofanyika jijini Dar es salaam. 

Habari picha na Victoria Stanslaus 

PICHANI NI MAJIKO YA NISHATI MBADALA YANAYOPATIKANA KWENYE BANDA LA SIDO VIWANJA VYA SABASABA


Hama hakika  haya ni majiko yenye ubora na imara yanayotengenezwa na Sido ambayo yanatumia nishati safi ya kupikia  hivyo ni vyema watu wote kufika kwenye banda la Sido kwenye  viwanja vya Maonyesho ya sabasaba  ambako maonyesho haya ni ya 49 yanayofanyika Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. 

Habari picha na Victoria Stanslaus. 

SIDO YAUNGA MKONO MATUMIZI YA NISHATI SAFI


 Afisa Masoko Mwandamizi Sido Makao Makuu Christopha Eduwadi Mwakyusa amesema katika kuunga mkono juhudi na jitihada za Dr Samia  ifikapo mwaka 2030 watu wote nchini tanzania watumie nishati safi ya kupikia  ambako upande wao Sido wanatoa mafunzo ya kutengeneza mkaa mbadala Mkaa huu auchafuhi mazingira . 

Pia Sido imewaandaa wataalam wa kutengeneza majiko ambayo yanatumia mkaa mbadala vilevile Sido wanatengeneza mashine na vipuri vya majiko yote Mali ghafi zake zinatoka hapa nchini tanzania .

Sido wameweza kuwafikia Mama Lishe na Baba Lishe kwa kuwapa elimu na mafunzo namna ya kutumia nishati safi ya kupikia ,Taasisi , kampuni,mashuleni,kwenye kambi za jeshi ,polisi na magerezani Sido imeweza kupeleka majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia huku akiwataka watu kutembelea kwenye banda la Sido  ili wanunue majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia  kwenye viwanja vya Sabasaba Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam  katika maonyesho ya 49. 

Habari picha na Ally Thabit Mbungo. 

PPRA YAWAFIKIA WATU WENYE ULEMAVU


 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPRA  Josefu Muozi amesema watu wenye ulemavu katika  kupata fursa za tenda za PPRA  wamefikiwa kwa kiwango kikubwa huu ni mpango maalum ulioandaliwa na serikali tangu mwaka 2011 na sheria ya PPRA  ikafanyiwa maboresho mwaka 2023  ambako maboresho haya yamesaidia kwa kiasi kikubwa watu wenye ulemavu wa aina zote kupata zabuni za tenda za PPRA. 

Pia PPRA  imeandaa majarida yenye maandishi ya nukta nundu kwaajili ya walemavu wasio Ona na vifaa vya kurekodia sauti zana hizi zimewezesha watu wenye ulemavu kupata elimu na uwelewa kuhusu  zabuni na tenda zinazotolewa na PPRA  vilevile PPRA  inatoa elimu kwa watu wote kupitia redio,tv,magazeti,na makongamano pamoja na semina  kupitia taasisi za watu wenye ulemavu. 

Josefu Muozi amewataka watu kutembelea banda la PPRA  viwanja vya sabasaba maonyesho Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam kwenye maonyesho ya 49 habari picha na Victoria Stanslaus. 


PPRA YAFUNGUA FURSA KWA WATANZANIA


 Mkurugenzi  Mkuu wa PPRA Denisi Simba amewataka watanzania kuchangamkia fursa  za Uzabuni wa tenda mbalimbali zinazotolewa na PPRA  kwani serikali imetenga kiasi cha tilioni 38  kwaajili ya wale wote wanaopata tenda za serikali .

Denisi Simba amesema PPRA  wameweka mazingira rafiki na wezeshi kwa makundi yote ikiwemo wanawake ,vijana,wazee na Watu wenye ulemavu Pia amewataka watu watembelee banda la PPRA  kwenye maonyesho ya 49 ya sabasaba yanayofanyika jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit Mbungo