Tuesday, 18 June 2019
KITUO CHA TAARIFA NA MAARIFA CHA MABIBO CHATEMA CHECHE DHIDI YA BAJETI
Salma Muhammad Mwanaharakati wa kituo cha taarifa na maarifa mabibo, ameitaka Serikali kuweka bajeti yeneye mlengo wa kijinsia kwani bajeti bajeti ilio wasilishwa na waziri wa fedha haijazingatiwa maswala ya kijinsia wala kuwakomboa wanyonge na badala bajeti imekuwa yenye machungu na ya ukandamizaji kwani swala lakumtua mama ndoo kichwani halijazingatiwa pia imekuja kumkandamiza na kumzofiisha mwanamke wa kitanzania pale waziri mpango alipo tamka kuwa taulo za kike zinazo ingizwa na kutengenezwa hapa nchini Tanzania zitalipa kodi kwa kiwango kikubwa hivyo ameitaka Serikali pamoja na wabunge kuja na mpango mkakati madhubuti wakufuta kabisa kodi za taulo za wanawake na pia amezungumzia swala la kuongezwa kwa kodi kwa nywele bandia kwani madhala yake wanawake watakosa ajira.
Amesema haya Mabibo jiji Dar es Salaam.
Habari Picha Ally Thabit
VIJANA WATAKWA NA MACHOZI JUU YA BAJETI
Robeati Sigwa amesema kuwa bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha Philip Mpango, haijainisha jinsi ya kuwakomboa kiuchumi vijana na badala yake bajeti hii imekuwa kandamizi na isiyotenda haki kabisa, masalani kwa kurejesha tozo za taulo za kike hii inaonesha jinsi gani mtoto wa kike atakapokosa fursa ya kuuzulia kimasomo kama inavyotakiwa pindi atakapokuwa akifika kipindi cha mabadiliko ya kibaiolojia kwakuwa taulo hizi zimekuwa na bei kuwa hivyo ameitaka serikali pamoja na wabunge kuondoa kabisa tozo ya kodi ya taulo za kike kwa ajili ya masilahi ya Taifa letu la Tanzania katika kumkwamua kielimu mtoto na kiuchumi mwanamke na kuleta usawa katika Taifa haya.
Amesema haya Mbezi Malamba mawili wilaya ya ubungo jiji Dar es Salaam.
Habari picha Ally Thabiti
MJASILIAMALI APAZA SAUTI BAJETI
Magdalena Ngaleni amesema bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha ni bajeti kandamizi kwani taulo za kike kodi yake haijafutwa wala kupunguzwa hivyo itasababisha na kuchangia kwa kiasi kikubwa watoto wakike kutohudhuria masomo inavyotakiwa na hatimae tutapata taifa la watoto wakike wasiojua kusoma na kuandika. Hivyo ameitaka Serikali kuweza kufanya mabadiriko ya bajeti hii kwa kufuta tozo kwa taulo zinazo tengenezwa na kuingizwa hapa nchini, lengo kumnusuru mtoto wa kike.
amesema haya eneo la kigogo Ruagwa jiji Dar es Salaam
Habari picha Ally Thabiti
KITUO CHA MAARIFA NA TAARIFA CHA SAYARI CHAFANYA MAZITO
pichani wanaharakati mbalimbali wakipata mafunzo ya ujasiliamali jinisi ya kutengeneza mifuko mbadala ambayo yameandaliwa na kituo cha sayari lengo kuwakwamua kiuchumi wakazi wa chanika wakiwemo wanawake na wanaume huku akiwemo mwenyekiti wa serikali za mitaa wagogo Ramadhani Mapunda Ramadhani, Mkurugenzi wa Gulu Plan na wengineo kwenye kata ya Zingiziwa Eneo la Chanika Manispa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Habari ya Picha na Ally Thabiti
ASASI YA BINTI MAKINI YATOA KILIO KIZITO JUU YA BAJETI
Msichana kutoka ASAS binti makini amesema kupandishwa kwa tozo za nywele bandia pamoja na taulo za kike imeleta tatizo katika Tanzania yetu, ameitaka Serikali kuweza kufanya mabadiliko ya bajeti hii kwani wasivyofanya hivyo watasababisha wanawake wengi kukosa ajira na kujihusisha maswala ya uwasherati. Amesema haya kwenye viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jiji Dar es Salaam.
Habari Picha na Ally Thabiti
WANAKISHAPU WALIA NA BAJETI
Diwani wa viti maalum kutoka kishapu amesma bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha ni bajeti ambayo inamkandamiza mwanamke hususani upanse wa upatikanaji wa maji vijijini hakijaekewa mkazo napia upande wa ujenzi wa vituo vya Afya na barabara ni changamoto kubwa na kutoondolewa tozo kodi za taulo za kike itasababisha watoto wa kike kutofanya vizuri kielimu, amesema haya kwenye viwanja TNGP Mtandao.
Habari picha na Ally Thabit
Wildafu Kuazinisha Mtoto wa Africa kivingine
Anna kulaya Mkurugenzi wa Wildafu amesema tarehe 20/06/2019 watafanya kongamano kubwa nala kipekee ambalo litajumuisha watoto lengo kuwapa elimu namafunzo juu ya Afya ya Uzazi na utoa taarifa kipindi watakapo kutana na maswala ya ukatili wa kijinsia.
Habari Picha na Ally Thabiti
Subscribe to:
Posts (Atom)




