Saturday, 12 July 2025

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KUTOKA MKOANI MARA WAMACU LIMITED CHAFICHUA SIRI NZITO KWENYE MAONYESHO YA SABASABA YA 49


 Olais Piniel Meneja Shughuri wa Chama Kikuu cha Ushirika kutoka Mkoani MARA WAMACU LIMITED   amesema ni muhimu watu kutumia kahawa aina ya Arabica  kwani miongoni mwa siri zilizojificha kuasaidia mtu kutopata kisukari steji ya pili ,kansa steji ya oili,kulinda maungio ya mguu,kibofu cha mkojo kutopata matatizo , kulinda Figo kutopata na magonjwa, na  inapunguza unene uliokithiri.

Ivyoamesema bei zao ni rafiki na nafuu kwa wateja wao na pia kahawa inawawezesha watu kupata ajira amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit Mbungo 

CHAMA CHA USHIRIKA CHA MARA COOPERATIVE UNION WAMACU LIMITED YAJITANGAZA KWENYE MAONYESHO YA SABASABA YA 49 JIJINI DAR ES SALAAM


 Alfred Msajigwa Afisa Tehama Chama Kikuu cha Ushirika kutoka Mkoani MARA WAMACU LIMITED  amesema wao ni mara  ya kwanza kushiriki kwenye maonyesho ya Sabasaba  yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es salaam  licha ya ugeni wao wamepata faida ya kujitangaza na kupata masoko ya kitaifa na kimataifa  ambako nchi ya Bulgaria,Ukraine  na Rashia. 

Kahawa yao aina ya Arabika ina ubora ivyo wanawataka watanzania na wasio watanzania kutumia kahawa yao aina ya Arabika . Chama kikuu cha Wakulima Mkoani MARA WAMACU LIMITED  itafanya ka'i ya kufungua masoko jijini dar es salaam  na mikoa mingine kwaajili ya kuwafikia wateja wao amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 kwenye banda la Wizara ya Kilimo .

Habari picha na Ally Thabit 

Friday, 11 July 2025

MAMLAKA YA AFYA YA MIMEA NA VIWATILIFU TANZANIA YAMPONGEZA RAIS SAMIA


 Dr Mujuni Kabululu Kaimu Mkuu Kitengo cha Kuifadhi Nasaba za Mimea Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania  amempongeza rais Dr Samia  kwa kuweza kununua ndege kwaajili ya kupambana na kuwadhibiti Viwavijeshi,Kweleakwelea na Nzige .

Ndege hii imekuwa mkombozi kwa wakulima ambao mazao yao yalikuwa yanaaribiwa na  vivamizi  hata ivyo serikali itaepukana na gharama ya kukodi ndege nchi za nje kwaajili ya kudhibiti kwelea Kwelea,Viwa vijashi , Nzige na Panya .

Dr Mujuni amesema Mamlaka yao inatoa vibali vya kuingiza na kupeleka nje ya nchi mazao vilevile Mamlaka  hii inatoa vibali vya kuingiza viwatilifu na kusambaza teknolojia  kwa wakulima na wanatoa elimu kupitia Almashauri  kwa wakulima namna ya kutumia viwatilifu kwenye mazao yao .

Pia wanatumia redio,TV,Vipeperushi  na Mafunzo mbalimbali kwa wakulima anawataka watu wote kufika  kwenye banda la Wizara ya Kilimo na kutembelea Mamlaka  ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania  ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye maonyesho ya 49 yanayofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

TARI YAJA NA MUAROBAINI KWA WAKULIMA


 Dr Filson Kagimbo Mkurugenzi Mkuu wa TARI  Kigoma amesema wakulima wengi walikuwa wanakumbwa na changamoto za kulima bila tija ivyo Taasisi ya Kilimo Tanzania TARI  imeamuwa kufanya tafiti na kuwapelekea teknolojia wakulima.

Moja ya majukumu ya TARI  kufanya utafiti wa Afya ya Udongo,Utafiti wa mazao na Ugunduzi wa mbegu bora,Kulinda mazao yasishambuliwe na wadudu pamoja na magonjwa mbalimbali, Namna ya kuongeza thamani kwenye mazao na kutunza pia wanawafundisha na kufanya utafiti wa za kuifadhi na kusindika mazao pamoja na kuwapelekea teknolojia mbalimbali.

Amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 wilayani temeke jijini dar es salaam  kwenye  banda la TARI. 

Habari picha na Ally Thabit 

TAWA YAVUTIWA NA MWITIKIO WA WATU VIWANJA VYA SABASABA


 Zuwena Kikoti Muifadhi  Mkuu wa TAWA amesema kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika jijini dar es salaam  wilayani temeke Tawa wamevutiwa kwa kiasi kikubwa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuona wanyama .

Maombi ya watu kutaka kuwepo kwa Tembo na Twiga watafanyia kazi kutokana na mazingira ya Ikolojia  hata ivyo amewataka watu kufika eneo la Pande lililopo Bunju ambako kuna hifadhi ya wanyamapori ambako kiingilio elfu 11800 .

Habari picha na Victoria Stanslaus 

CHUO KIKUU CHA CBE CHAWAFIKIA WAKULIMA KIDIGITALI


 Martin Alfred Lwafu ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha CBE kwa ngazi ya Diploma ICT amesema wakulima nchini tanzania wanapata changamoto nyingi sana katika kuuza mazao yao kwa njia ya MNADA ivyo ameamua kuja na mfumo wa Tehama ambao utamuwezesha mkulima kuuza mazao yake kupitia njia ya kidigitali  ambako mkulima anaweza kutumia simu janja au kompyuta mpakato .

Kama inavyoonekana pichani mazao ya Mpunga na Korosho amesema haya ndani ya viwanja vya Sabasaba  kwenye  banda  la CBE kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA CBE KUTATUA SIDA YA MAEGESHO YA MAGARI


 Petero ni Mwanafunzi wa Ngazi ya Diploma Mwaka wa pili Chuo Kikuu cha CBE  ICT amebuni mfumo ambao utatumika kutatua matatizo ya maegesho ya magari Mfumo huu utamwezesha mtu kutambua maegesho ya magari kama yamejaa ama ayajajaa kupitia simu janja au kompyuta mpakato  miongoni mwa faida zitakazo patikana kupitia mfumo huu serikali itakusanya pesa yake kwa wepesi , kuepuka usumbufu  kwa wenye magari na kunusuru upoteaji wa mafuta .

Petro  amewaakikishia watu kuwa mfumo huu ni salama huku akitoa wito watu wajiunge na Chuo Kikuu cha CBE  amesema haya ndani ya banda la CBE lililopo kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 wilaya ya temeke jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit