Tuesday, 17 June 2025

MWENYEKITI WA CHAMA CHA CHAUMA AZIDIWA MAUTUTI

 Ashim Rungwe  Mwenyekiti wa Chama cha Chauma Maarufu Mzee wa Ubwabwa yupo  Maututi Mkoani Kilimanjaro Mjini Moshi na kupelekea kulazwa kwenye hospitali ya Kisms hali hii ya ugonjwa imemtokea kwenye zoezi la kukieneza na kukitangaza chama cha Chauma haya yamesemwa na mkuu wa Idara ya chama  cha Chauma John Mrema . 

Ambae amesema plesha na sukari vimepanda kwa Ashim Rungwe maarufu Mzee wa Ubwabwa.

Habari na Ally Thabit Mbungo  

WADAU WA KILIMO WAKUTANA

 Dr Mustafa amewasilisha Mada ya Namna ya ubunifu utakavyo wasaidia wakulima  kulima kilimo chenye tija .

Habari na Ally Thabit Mbungo.  

Monday, 16 June 2025

NCHI YA DRC KONGO YAJA NA MIKAKATI KABAMBE KWA TANZANIA


 Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji nchi ya Drc Kongo Roland Kashwakale  amesema watahakikisha kudhibiti kwenye mipaka yao dhidi ya wahamiaji wanaotaka kuingia tanzania . Pia watakuwa wanafanya doria mara kwa mara na pindi watakapo wakamata watu wasifuata taratibu za kuingia tanzania  kupitia Drc Kongo sheria kali watachukuliwa amemuhakikishia Kamishina Mkuu wa Tanzania Dr Ana Makakala kuwa nchi ya Drc Kongo itatoa ushirikiano wao na kuimarisha ulinzi na usalama kwe nye mipaka ya nchi ya Drc Kongo na nchi ya Tanzania  kama wanavyoonekana kwenye picha ya pamoja viongozi hawa.

Habari picha na Ally Thabit Mbungo 

TANZANIA NA DRC KONGO YAKUTANA KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAM


 Kamishina Uhamiaji Nchini Tanzania Dr Ana Makakala amesema lengo la nchi ya tanzania kukutana na Mkurugenzi  Mkuu wa Uhamiaji kutoka nchi ya Drc Kongo Roland Kashwakale ni kuhimarisha ulinzi na usalama kati ya Tanzania na Drc Kongo na kukuza uchumi wa nchi zote mbili Pamoja na kuleta maendeleo.

Dr Ana Makakala Kamishina Mkuu wa Uhamiaji  nchini tanzania  amesema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu jeshi la Uhamiaji la tanzania limeweka nguvu kubwa mipakani kote kwenye nchi zinazozunguka tanzania  kwaajili ya kudhibiti wahamihaji ambao awana vibali vya kuingia tanzania hili kuimarisha ulinzi na usalama wa tanzania kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Dr Ana Makakala amesisitiza kuwa tanzania itaendelea kufanya mikutano yake na nchi za Rwanda, Burundi,Uganda na nchi zinginezo.

Mfano Mkutano wa Drc Kongo na Tanzania ni mwanzo tu wa mikutano mingiyo Dr Ana Makakala ametoa wito kwa watu wanaotaka kuja tanzania wafuate kanuni,miongozo,taratibu na sheria kabla awajaingia tanzania .

Amesema haya jijini dar es salaam 

Habari picha na Ally Thabit Mbungo. 

Friday, 13 June 2025

TANZANIA YAWASIRISHA BAJETI YA KIMKAKATI

 Waziri wa Fedha Dr Mwigulu Mchemba amesema bajeti alioiwasirisha bungeni jijini dodoma kiasi cha tilioni56.49 bajeti hii itamalizia miradi mbalimbali ya kimkakati na ile itakayoanzishwa . Bajeti hii fedha nyingi za ndani zitaendesha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 bila kutegemea mataifa ya nje .

Habari na Ally Thabit Mbungo 

ISRAEL K. ILUNDE. AKOSOA MIFUMO YA KODI

 Ndg Israel K. Ilunde Mwenyekiti wa Policy Forum(PF) na Mkurugenzi mtendaji wa YPC kutoka Kibaha mkoa wa pwani amesema mifumo ya kodi iliyopo nchini tanzania si rafiki kwa wajasilia Mali na wafanyabiashara wadogo ndio maana watu awatoi ushirikiano pindi TRA wanapowahitaji wafike kwenye ofisi zao na kwenye mamlaka zingine za kikodi.

Na pindi mtu au taasisi ukihitaji uwe mlipa kodi unapofika kwenye ofisi zao unakutana na mambo mengi ya kukukatisha tamaa . 

Mwenyekiti na Mkurugenzi ametoa wito kwa serikali na mamlaka za kikodi nchini tanzania zifanye marekebisho kwenye mifumo ya kodi na waweke mazingira rafiki na wezeshi kwa wanaohitaji kulipa kodi ambao ni wapya na wale wanaoendelea kulipa kodi hii itasaidia nchi yetu kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa walipa kodi na kuachana na bajeti yetu ya tanzania . Kutegemea fedha za misahada na za waisani kutoka nje ya nchi.

Amesema haya makao makuu ya TGNP eneo la mabibo jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit Mbungo 

MJUMBE WA TGNP AIMIZA BAJETI YENYE USAWA WA KIJINSIA

 Mwanaharakati na Mjumbe wa TGNP Ana amesema serikali ya tanzania iakikishe bajeti wanazozipanga zizingatie usawa wa kijinsia .Kwani bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Dr Mwigulu Mchemba yenye kiasi cha shilingi za kitanzania tilioni 56.49 ,kwa kiasi kikubwa aijazingatia misamaha ya kikodi kwenye taulo za kike,visaidizi vya watu wenye ulemavu na mengineyo.

Ametoa wito kwa Wanaharakati wa tanzania kuendelea kupaza sauti kwa serikali amesema haya makao makuu ya TGNP eneo la mabibo jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit Mbungo