Friday, 13 June 2025

ISRAEL K. ILUNDE. AKOSOA MIFUMO YA KODI

 Ndg Israel K. Ilunde Mwenyekiti wa Policy Forum(PF) na Mkurugenzi mtendaji wa YPC kutoka Kibaha mkoa wa pwani amesema mifumo ya kodi iliyopo nchini tanzania si rafiki kwa wajasilia Mali na wafanyabiashara wadogo ndio maana watu awatoi ushirikiano pindi TRA wanapowahitaji wafike kwenye ofisi zao na kwenye mamlaka zingine za kikodi.

Na pindi mtu au taasisi ukihitaji uwe mlipa kodi unapofika kwenye ofisi zao unakutana na mambo mengi ya kukukatisha tamaa . 

Mwenyekiti na Mkurugenzi ametoa wito kwa serikali na mamlaka za kikodi nchini tanzania zifanye marekebisho kwenye mifumo ya kodi na waweke mazingira rafiki na wezeshi kwa wanaohitaji kulipa kodi ambao ni wapya na wale wanaoendelea kulipa kodi hii itasaidia nchi yetu kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa walipa kodi na kuachana na bajeti yetu ya tanzania . Kutegemea fedha za misahada na za waisani kutoka nje ya nchi.

Amesema haya makao makuu ya TGNP eneo la mabibo jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit Mbungo 

No comments:

Post a Comment