Tuesday, 30 July 2019

Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakimsikiliza mtoto anayetibiwa  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara iliyofanywa na Naibu waziri huyo ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa JKCI kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo. 


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimwelezea Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin namna ambavyo chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa watoto wenye magonjwa ya moyo kitakavyorahisisha huduma za matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri huyo alitembelea JKCI leo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara fupi ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinayotolewa na Taasisi hiyo. Naibu Waziri huyo alitembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa China na kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na Hospitali kuu ya jimbo la Shandong.

Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian Mlawi akiwaelezea Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin jinsi wauguzi wa chumba hicho wanavyowahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo.


Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin akimpa pole mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa nchini China. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Makamu Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong la nchini China  Li Leping  wakisaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya hospitali hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Moja ya makubaliano hayo ni wataalamu wa afya kutoka JKCI kwenda katika hospitali hiyo kujifunza matibabu ya moyo kwa kutumia vifaa vya kisasa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Makamu Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong   la nchini China  Li Leping wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya hospitali hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi zawadi ya ngao Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), hospitali ya jimbo kuu la Shandong  na Ubalozi wa China nchini wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Picha na Genofeva Matemu - JKCI

HOSPITALI YA MOI YATAMBULISHA TEKNOLOJIA YA KUFANYA UPASUAJI BILA KUFUNGUA KICHWA

Na Ally Thabiti

Hospitali ya MOI hatimaye imetambulisha teknolojia itakoyotumika kufanya upasuaji wa kichwa kwa kuhusisha mfupa wa paja, badala ya upasuaji uliozoeleka, kwa maana ya kufungua fuvu la kichwa.

Hafla hiyo imefanyika katika taasisi ya MOI ambayo huduma hii inapatikana jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Afya ndugu Faustin Ndugulile

 Naibu Waziri wa Afya ndugu Faustin Ndugulile ameweka wazi kuwa serikali imetenga kiasi cha shlingi Bilioni 16.5 kwa ajili ya kununua vifaa tiba katika hospitali mbalimbali nchini Tanzania.

Na tayari serikali imetoa shilingi bilioni 7.9 ambazo zitatumika katika kununua vifaa mahususi katika huduma hii mpya - Upasuaji bila kufungua kichwa.

Pia amewatoa hofu watanzania kuwa ataimarisha rasilimali watu katika hospitali kwa lengo la kuhakikisha kuduma bora.

Image result for mkurugenzi mtendaji wa moi
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface wa taasisi ya Mifupa - MOI amesema upasuaji huo utafanyika kwa gharama ya shilingi laki tano hadi laki sita (500,000/= - 600,000/=) ukilinganisha na nchi zingine ambapo huduma hii hufanyika kwa kiasi cha shilingi milioni sitini (60,000,000/=)

Na amesisitiza kuwa hii teknolojia itasaidia katika kuongeza ufanisi wa kazi na itaokoa maisha ya walio wengi.

Baadhi ya waalikwa wakitoa maoni yao.

Friday, 26 July 2019

LHRC YALAANI VIKALI PICHA ZINAZOSAMBAA MTANDAONI

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Haki za Binaadam LHRC Bi Anna Henga amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali polisi wa kituo cha Mburahati kwa kuwadhalilisha wanawake baada ya kuwabebesha mabango na kusambaza picha za utupu na kuwapa maneno ya kashfa kuwa wanawake hao ni malaya.

Bi Anna Henga - Mkurugenzi Mtendaji LHRC
Tukio hilo limetokea baada ya wanawake hao kufikishwa kituoni hapo kisha polisi kuwabebesha mabango yenye maneno ya kuwa ni wao ni malaya. Katika kikao na waandishi wa habari hii leo, Bi Henga amelaani tukio hilo huku akitaja baadhi ya vifungu vya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania vilivyokiukwa.

Bi Henga amesema kuwa kitendo hicho ni udhalilishaji wa utu wa mwanamke, ukiukwaji wa hakiza binadamu, ukiukwaji wa misingi ya dhana ya kutokuwa na hatia, kuingiliahaki ya uhuru binafsi (faragha) pamoja na kuvunja inara ya 10 Mkataba wa Kimataifa wa haki za kiraia wa mwaka 1966.

Bi Henga amelitaka jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kinidhamu polisi waliofanya kitenfo hiki. LHRC itawasaidia wanawake walioathiriwa kupata msaada wa kisheria na kisaikolojia ili waweze kupata haki zao na kuweza kurudi katika hali ya kawaida.

Na Ally Thabit

Tuesday, 23 July 2019

WAZIRI WA KILIMO ATANGAZA NJAA KARI


Waziri wa kilimo Japhet Asunga amesema mikoa kumi tatu itakumbwa na ukosefu wa chakula mikoa hiyo Iringa, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Tabora, Lindi, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Manyara, Singida.  Amesema chanzo cha kukumbwa na njaa kwa mikoa hii uwaribifu wa mazao ulisababishwa na ndege aina ya Kweleakwelea, Viwavijeshi na ukosefu wa pembejeo na kubadilika kwa misimu ya mvua.

Japheti Asunga ameitaka mikoa yenye chakula cha kutosha kuto uza kiolelaolela amesema haya kwenye ofisi ya wizara ya kilimo jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na wanahabari.

Habari picha na

Ally Thabiti.

Tuesday, 9 July 2019

CHUO CHA ANGERA KAIRUKI YATANGAZA FULSA NA KUFUNGUA MILANGO KWA WATANZANIA


Harasafa Juba Afsa masoko na mawasiliano wa Hospital ya Kairuki amewataka vijana wa kitanzania wajiunge na chuo cha Angera Kairuki kwani wanatoa mafunzo mazuri ya uhuguzi pia amewataka wazazi kuwasisitiza watoto wao kusoma masomo ya Sayansi na wawapeleke chuo cha
Kairuki kwa ajili ya kupata elimu bora na mzuri pia amewataka watanzania watembelee banda la Kairuki ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye jengo la Jakaya Kikwete ili wapate elimu juu ya maswala ya Afya na wajue fursa zinazopatikana kwenye chuo cha kairuki amewatoa hofu wazazi na walezi kuwa hospitali ya kairuki inatoa huduma bora na za gharama nafuu pia wanamikakati ya kwenda kwenye mikoa mengine ya Tanzania na amewataka watu wenye bima waende hospital ya kairuki watapata tiba

Hamesema haya kwenye maonyesho ya sabasaba ya 43 wilaya ya temeke jijini Dar es salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

Monday, 8 July 2019

DAWASA YAJA NA MUHARUBAINI KABAMBE


Mkurugenzi mkuu wa Dawasa Mwandisi Krispin Ruwemeja amesema sasa hivi kuna sheria ya maji safi na usafi wa mazingira ni sheria namba tano ya mwaka 2019 ambako apo mwanzo ni sheria mzuri ambayo imekuja kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji na uzembe wa watu mbalimbali ambako imeshaanza kutumika na ndiyo maana kuna mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa maji na sasa zaidi ya  85% ya watanzania wanapata maji na lengo la kuja sheria hii pia ni kuwasajili wachimbaji wa visima pia Dawasa hivi sasa wanakusanya kiasi cha pesa hivi sasa bilioni 11.2 pesa ya kitanzania ametoa wito kwa watumiaji wa Dawasa kutoa ushirikiano pindi wanapopatwa na changamoto zozote.

Amesema haya ndani ya banda la Dawasa kwenye maonyesho ya 43 ya sabasaba jijini Dar Es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

MTEJA WA DAWASA ATOA TANO


Asia Rashidi ameipongeza shirika la maji safi na maji taka la mkoa wa Dar es salaam kwa kutoa huduma safi na bora amesema wanapata maji kwa wakati na uwakika pia wanalipa bili zao kwa kutumia mfumo wa Technolojia ambako inasaidia wateja kuokoa muda na kuepuka usumbufu na kupanga foleni.

Amewataka wakazi wa mkoa wa Dar es salaam kutoa ushirikiano kwa Dawasa pia ametoa wito kwa Dawasa waendelee kutoa elimu ya kutosha kwa jamii juu ya matumizi ya visima lengo wapate maji safi na salama na waepukane magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu pia ameitaka jamii wanapoona hualibifu unapofanyika wa mabomba au kwenye vyanzo vya majiwatoe taalifa kwa Dawasa amesema haya alipotembelea banda la Dawasa viwanja vya Sabasaba kwenye maonyesho ya 43 jijini Dar es salaam.

Habari picha na
Ally Thabiti

Saturday, 6 July 2019

VETA YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWA KISHINDO KIKUBWA


Sita Peter Meneja husiano wa Veta amesema wameweza kutoa Elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wengi pia namna ya kutengeneza mashine rengo viwanda vitakavyo anzishwa watumike katika utaaramu amesema mpaka sasa wameweza kutoa mafunzo pia kwa watu wenye ulemavu amewataka vijana wa kitanzania wajiunge na Veta kwani ndiyo mkombozi wao.

Amesema haya kwenye mbanda la Veta katika maonyesho ya 43 yanayofanyika viwanja vya sabasaba wilaya ya Temeke jijini Dar Es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti.

VETA NA AIRTEL YAFUFUA MATUMAINI YA AJIRA KWA VIJANA


Chazi Mapuli Meneja miradi wa misomo amesema mpaka sasa mradi wa visomo umeweza kuwasaidia vija zaidi ya 3000 kupata vyeti na kujiajili na wengine wameajiliwa ambako hapo hawali walipoteza matumaini kwa kukosa vyeti lakini baada ya kujiunga na mladi wa visomo wameweza kufanikiwa kujikwamua kiuchumi na kuondokana na ofu na wasiwasi wa kupata ajira mladi wa visomo umeanzishwa na veta kwa kushirikina na kampuni ya simu za mikononi ambako mwanafunzi anaweza kusoma masomo yote Veta zaidi ya kumi na tatu kupitia simu yake ya mkononi kwa Application ya visomo na wengine zaidi ya 128 wanaendea na mafunzo kupitia visomo chazi mapuli amewatoa hofu vijana kuwa program hii yatumia lugha ya kiswahili na kingeleza masharti ujue kusoma na kuandika tu unapata mafunzo.

Amesema haya kwenye banda la Veta katika maonyesho ya 43 yanayofanyika viwanja vya sabasaba wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti. 

VETA YAWAKWAMUA WATU WENYE ULEMAVU


Zaria Mohamed ni fundi wa kufuma kofia licha ya kuwa na ulemavu wa viungo wa miguu hakukata tamaa na badala yake akapata ujuzi wa kufuma kofia baada ya kupata mafunzo kutoka veta kutoka mkoani Singida ameitaka Veta kutoa mafunzo na Elimu kwa watu wenye ulemavu kwa kiwango kikubwa ametoa wito kwa watu wenye ulemavu wajiunge na Veta ili wapate Elimu itakayo weza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kimaisha.

Amesema haya kwenye banda la Veta katika maonyesho ya 43 yanayofanyika maonyesho ya sabasaba jijini Dar Es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

BOT YAFANIKIWA VITA YA UTAKATISHAJI WA FEDHA FARAMU


Gamwaka Chazi mkaguzi wa mabenki nchini Tanzania asema swala la utakatishaji fedha haramu wameweza kulizibiti baada ya kuyafunga maduka ya kubadilisha fedha za kigeni pia mabenki hapa nchini yanajitaidi kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za kifedha za kigeni kwa kiwango kikubwa amesema haya kwenye maonesho ya 43 ya sabasaba yanayofanyika jijini Dar es salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

Friday, 5 July 2019

MKURUGENZI WA MANISPAA YA KIGAMBONI AWATOA MCHECHETO NA HOFU


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ng'wilabuzu Ludga amesema kuwa wakazi wa Kigamboni wapuuze taarifa za uongo zinazosambazwa mitandaoni na Magrupu ya wasapa juu ya Vibali vya ujenzi kuwa vinachelewa maneno haya hayana ukweli wowote kwani watu ambao awapati vibali hivyo kwa wakati awatoi ushirikiano pindi wanapopigiwa simu na wengine wanadaiwa kodi ya Ardhi na pia wajalipa lamani za micholo kwani manispaa ya Kigamboni vibali vya ujenzi vilikuwa vikitolewa kwa muda wa miezi mitatu kupitia baraza la madiwa na ilikuwa ikikwamisha ujenzi wa viwanja vya watu na sasa manispaa ya Kigamboni kupitia mkurugenzi huyu vibali vinatolewa ndani ya wiki moja kwa wanaotimiza masharti mpaka sasa vibali vya ujenzi zaidi ya 3000 zimetolewa ndani ya manispaa ya Kigamboni.

Nae mwenyekiti wa vibali vya ujenzi manispaa ya Kigamboni Magdalena Malunda  amewataka wakazi wa kigamboni kutowatumia madalali wanapotaka vibali vya ujenzi na badala yake waendee kwenye ofisi za manispaa ya Kigamboni ili kuepusha usumbufu pia amewataka wenye malalamiko wawasilishe kwenye dawati la maswala ya vibali vya ujenzi na si kwenye mitandao ya kijamii na magrupu ya wasapu

Nae mwansheria wa Manispaa ya Kigamboni Charles Lawiso amesema mtu yeyote atekutwa anajenga nyumba bila kibali ususa ni mafundi watashitakiwa na kosa la kijinai na kupigwa faini ya shilingi 200,000 au kutumikia kifungo cha kwenda jera .

Mkurugenzi wa manispaa amemalizia wananchi kutokubali kutoa fedha kwa watu wanao wakamata siku za weekend kwani hiyo ni rushwa na akibaini na kumkamata mfanyakazi yeyote anayefanya kazi hizo atamkuza kazi katika Manispaa ya Kigamboni, amesema haya kwenye ofisi za Manispaa ya Kigamboni jijini Dar Es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA TEMEKE ATANGAZA VITA



Amon Kapwale Kamishna msaidizi wa polisi mkoa wa temeke amewataka watu wote wanaojishuhulisha na maswala ya wizi, Ujambazi, Ukabaji na Udokozi waache mala moja kwani Jeshi la Polisi litawashughulikia kwa kuwakamata na kuwapeleka mahakamani amesema haya wakatia akizungumza na wana habari kituo cha polisi cha Kigamboni ambako vitu mbalimbali wamevikamatwa na watumiwa nao wametiwa mbaloni pia ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwafuatilia mienendo ya watoto wao kwani eneo la kigamboni watoto nne wamekamatwa walikuwa wakitumika katika wizi na hawa ni wa shule ya msingi.

Amewatoa ofu wana temeke na kusema teemeke ni shwari

Habari Picha na
Ally Thabiti

PICHANI VIFAA VYA WIZI VILIVYOMATWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA TEMEKE ENEO LA KIGAMBONI


Kama inavyonekana hivi ni vitu vilivyo ibiwa mkoa wa Temeke maeneo ya Kigamboni na kushikiliwa na Polisi

Habari Picha na
Ally Thabiti

PICHANI BIDHAA ZA JOHARI YUSUPH KWENYE BANDA LA SIDO MAONYESHO YA 43 YA SABASABA


Hizi ni bidhaa zenye ubora owa kiwango cha Kitaifa na Kimataifa zinazotengenezwa na Johari Yusuph kupitia mradi wa Feed Future pamoja na Sido.

Hivyo ni vyema tumuunge mkono Johari Yusuph kwa kununua bidhaa zake kwenye viwanja vya Sabasaba ndani ya banda la Sido na baada ya maonyesho kuisha pia tuendelee kununua bidhaa zake.

Habari Picha na
Ally Thabiti

VIJANA WA ASWA KUTOINYOSHEA SERIKALI JIDOLE


Johari Yusuph Kasuke mjasilia mali kutoka mkoa wa ilinga kata ya kilogota wilaya ya Isimani vijijini amewataka vijana wa kitanzania kuchangamkia miladi inayokuja hapa nchi kwani inafaida kubwa.

Johari ameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza mafuta ya Alizeti, Vikoi, Kupikia mladi wa Feed Future pia amewapongeza Sido kwa kumpa mafunzo juu ya usindikaji uwekaji wa lebo na kupata masoko amesema haya kwenye maonyesho ya 43 viwanja vya Sabasaba kwenye banda la Sido jijini Dar Es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

STEVENI NDENGA ATANGAZA FURSA


Steveni Ndenga amewataka vijana wa kitanzania waungane nae katika ufugaji wa nyuki na kulina Asali lengo waweze kupata kipato cha fedha ili wajikwamue kimaisha pia amewapongeza Sido na Feed Future kwa kutafutiwa masoko na kushiriki kwenye masoko na kushiriki kwenye maonyesho ya 43 ya Sabasaba na kuweza kufanya biashara ya Asali.

Ametoa wito kwa Sido na Feed Future  kutowaacha vijana katika elimu ya ujasilia mali pia ametoa wito kwa vijana waache kukaa vijioweni na kulalamika  swala la oajira.

Habari Picha na
Ally Thabiti

SIDO YAPEWA TANO MAONESHO YA SABASABA


Mkami Yusuph Tetele mjasiliamali kutoka mkoa wa mbeya wilaya ya Kyela ameipongeza Sido na Feed Future kwa kuwapa mafunzo ya ujasilia mali ya kutengeneza unga wa Dona na bidhaa zingine kwani yeye ameweza kujikwamua kiuchumi na amewataka vijana wezake ususani Mabinti wezake wajiunge na Sido. Ametoa wito kwa Feed Future waendelee kuwawezesha vija mbalimbali katika kiuchumi na kimaisha amesema haya kwenye maonesha ya 43 ya Sabasaba kwenye banda la Sido jijini Dar Es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti