Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China
Mhe. Lin Bin wakimsikiliza mtoto anayetibiwa katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara iliyofanywa na
Naibu waziri huyo ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la
Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa
JKCI kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akimwelezea Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu
wa China Mhe. Lin Bin namna ambavyo chumba cha uangalizi maalum (ICU)
kwa watoto wenye magonjwa ya moyo kitakavyorahisisha huduma za matibabu
katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri
huyo alitembelea JKCI leo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za
matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu
wa China Mhe. Lin Bin wakizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara fupi ya kuangalia
huduma za matibabu ya moyo zinayotolewa na Taasisi hiyo. Naibu Waziri
huyo alitembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo inayofanywa na
madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa China na kushuhudia
utiaji saini wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu
ya moyo baina ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na Hospitali kuu ya
jimbo la Shandong.
Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha
uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian
Mlawi akiwaelezea Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri
ya watu wa China Mhe. Lin Bin jinsi wauguzi wa chumba hicho
wanavyowahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe.
Lin Bin akimpa pole mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua
kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu
kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao
wa nchini China. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya watu
wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kufanya
kambi maalum ya upasuaji wa moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.
Mohamed Janabi na Makamu Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong la
nchini China Li Leping wakisaini mkataba wa
makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya
hospitali hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Moja ya makubaliano hayo
ni wataalamu wa afya kutoka JKCI kwenda katika hospitali hiyo kujifunza
matibabu ya moyo kwa kutumia vifaa vya kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.
Mohamed Janabi na Makamu Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong la nchini China Li
Leping wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika
mafunzo na matibabu ya moyo baina ya hospitali hizo mbili leo jijini Dar
es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa
China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kufanya kambi
maalum ya upasuaji wa moyo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi zawadi ya ngao Naibu Waziri wa Afya wa
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin mara baada ya kumaliza
ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa
ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Serikali ya
Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la Shanding
imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa JKCI kufanya
upasuaji wa moyo nchini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China
Mhe. Lin Bin wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), hospitali ya jimbo kuu la Shandong na Ubalozi wa China nchini wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Picha na Genofeva Matemu - JKCI
No comments:
Post a Comment