Friday, 26 July 2019

LHRC YALAANI VIKALI PICHA ZINAZOSAMBAA MTANDAONI

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Haki za Binaadam LHRC Bi Anna Henga amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali polisi wa kituo cha Mburahati kwa kuwadhalilisha wanawake baada ya kuwabebesha mabango na kusambaza picha za utupu na kuwapa maneno ya kashfa kuwa wanawake hao ni malaya.

Bi Anna Henga - Mkurugenzi Mtendaji LHRC
Tukio hilo limetokea baada ya wanawake hao kufikishwa kituoni hapo kisha polisi kuwabebesha mabango yenye maneno ya kuwa ni wao ni malaya. Katika kikao na waandishi wa habari hii leo, Bi Henga amelaani tukio hilo huku akitaja baadhi ya vifungu vya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania vilivyokiukwa.

Bi Henga amesema kuwa kitendo hicho ni udhalilishaji wa utu wa mwanamke, ukiukwaji wa hakiza binadamu, ukiukwaji wa misingi ya dhana ya kutokuwa na hatia, kuingiliahaki ya uhuru binafsi (faragha) pamoja na kuvunja inara ya 10 Mkataba wa Kimataifa wa haki za kiraia wa mwaka 1966.

Bi Henga amelitaka jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kinidhamu polisi waliofanya kitenfo hiki. LHRC itawasaidia wanawake walioathiriwa kupata msaada wa kisheria na kisaikolojia ili waweze kupata haki zao na kuweza kurudi katika hali ya kawaida.

Na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment