Friday, 5 July 2019

MKURUGENZI WA MANISPAA YA KIGAMBONI AWATOA MCHECHETO NA HOFU


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ng'wilabuzu Ludga amesema kuwa wakazi wa Kigamboni wapuuze taarifa za uongo zinazosambazwa mitandaoni na Magrupu ya wasapa juu ya Vibali vya ujenzi kuwa vinachelewa maneno haya hayana ukweli wowote kwani watu ambao awapati vibali hivyo kwa wakati awatoi ushirikiano pindi wanapopigiwa simu na wengine wanadaiwa kodi ya Ardhi na pia wajalipa lamani za micholo kwani manispaa ya Kigamboni vibali vya ujenzi vilikuwa vikitolewa kwa muda wa miezi mitatu kupitia baraza la madiwa na ilikuwa ikikwamisha ujenzi wa viwanja vya watu na sasa manispaa ya Kigamboni kupitia mkurugenzi huyu vibali vinatolewa ndani ya wiki moja kwa wanaotimiza masharti mpaka sasa vibali vya ujenzi zaidi ya 3000 zimetolewa ndani ya manispaa ya Kigamboni.

Nae mwenyekiti wa vibali vya ujenzi manispaa ya Kigamboni Magdalena Malunda  amewataka wakazi wa kigamboni kutowatumia madalali wanapotaka vibali vya ujenzi na badala yake waendee kwenye ofisi za manispaa ya Kigamboni ili kuepusha usumbufu pia amewataka wenye malalamiko wawasilishe kwenye dawati la maswala ya vibali vya ujenzi na si kwenye mitandao ya kijamii na magrupu ya wasapu

Nae mwansheria wa Manispaa ya Kigamboni Charles Lawiso amesema mtu yeyote atekutwa anajenga nyumba bila kibali ususa ni mafundi watashitakiwa na kosa la kijinai na kupigwa faini ya shilingi 200,000 au kutumikia kifungo cha kwenda jera .

Mkurugenzi wa manispaa amemalizia wananchi kutokubali kutoa fedha kwa watu wanao wakamata siku za weekend kwani hiyo ni rushwa na akibaini na kumkamata mfanyakazi yeyote anayefanya kazi hizo atamkuza kazi katika Manispaa ya Kigamboni, amesema haya kwenye ofisi za Manispaa ya Kigamboni jijini Dar Es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment