Tuesday, 30 July 2019

HOSPITALI YA MOI YATAMBULISHA TEKNOLOJIA YA KUFANYA UPASUAJI BILA KUFUNGUA KICHWA

Na Ally Thabiti

Hospitali ya MOI hatimaye imetambulisha teknolojia itakoyotumika kufanya upasuaji wa kichwa kwa kuhusisha mfupa wa paja, badala ya upasuaji uliozoeleka, kwa maana ya kufungua fuvu la kichwa.

Hafla hiyo imefanyika katika taasisi ya MOI ambayo huduma hii inapatikana jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Afya ndugu Faustin Ndugulile

 Naibu Waziri wa Afya ndugu Faustin Ndugulile ameweka wazi kuwa serikali imetenga kiasi cha shlingi Bilioni 16.5 kwa ajili ya kununua vifaa tiba katika hospitali mbalimbali nchini Tanzania.

Na tayari serikali imetoa shilingi bilioni 7.9 ambazo zitatumika katika kununua vifaa mahususi katika huduma hii mpya - Upasuaji bila kufungua kichwa.

Pia amewatoa hofu watanzania kuwa ataimarisha rasilimali watu katika hospitali kwa lengo la kuhakikisha kuduma bora.

Image result for mkurugenzi mtendaji wa moi
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface wa taasisi ya Mifupa - MOI amesema upasuaji huo utafanyika kwa gharama ya shilingi laki tano hadi laki sita (500,000/= - 600,000/=) ukilinganisha na nchi zingine ambapo huduma hii hufanyika kwa kiasi cha shilingi milioni sitini (60,000,000/=)

Na amesisitiza kuwa hii teknolojia itasaidia katika kuongeza ufanisi wa kazi na itaokoa maisha ya walio wengi.

Baadhi ya waalikwa wakitoa maoni yao.

No comments:

Post a Comment