Saturday, 30 November 2019
TUME YA USHINDANI YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURUSA
PROF Humphrey P .B Mosh amesema katika kuelekea maazimisho ya ushindani wa kibiashara ambako yatakuwa tarehe 3 mpaka5 mwezi wa 12 viwanja vya mnazi mmoja wajitokeze kwa wingi kuonyesha biashara zao TASAC itakuweepo,TRRC ,TTCR,na TCAA tume ya ushindani inaendana na kauli mbiu ya Magufuli kueleekea Tanzania ya viwanda ivyo amewataka watanzania kuwa wabunifu tarehe 4 mwezi12 kutakuwa na kongamano la kujadili maswala ya biashara za mitandaoni na ushindani wa biashara
habari picha na Victoria Stanslaus
habari picha na Victoria Stanslaus
TUME YA USHINDANI YAWATAADHARISHA WATANZANIA BIASHARA ZA MTANDAONI
Mkurugenzi wa tume ya ushindani ya biashara amewataka watanzania kutoamini biashara za mitandaoni ivyo amesema makampuni ya Ally Baba na mengineyo ivyo waache kuttumia makampuni mengineyo watatapeliwa amesema haya wakati akitambulisha kuwa kutakuwa na maonyesho ya ushindani wa kibiashara tarehe 3 mpaka 5 mwezi wa12 viwanja vya mnazi mmoja
habari picha na Victoria Stanslaus
habari picha na Victoria Stanslaus
KAMISHINA WA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWARA BORA ATEMA CHECHE
Kamishina wa haki za binadamu na utawala bora Nyanda Shuri amezitaaka asasi za kiraia kuwafikia watu wa pembe zoni kwa kuwapa elimu ya maswala ya jinsia na haki
habari picha na Victoria Stanslaus
habari picha na Victoria Stanslaus
RUSHWA YA NGONO NITATIZO
Mkurugenzi wa TGNP mtandao Riliani Riundi amesema swala la rushwa yya ngono ni tatizo kwa wanawake hapa nchini maofisini,viwandani pamoja na vyuoni ivyo amewataka wanawake na wanaume kupaza sauti
habari picha na Victoria Stanslaus
habari picha na Victoria Stanslaus
WIZARA YA AFYA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA NHIF
Mkurugenzi wa wizara ya afya Gresi Magembe amesema wizara ya afya inawaunga mkono NHIF walivyo amua kuja na vifurushi vya watu wa hali ya chini ivyo amewataka watanzania kuchangamkia furusa zilizo tolewa na NHIF kwaajili ya kunusuru afya zao ivyo amesema serikali itazidi kuboresha huduma za afya na kutoa dawa zakutosha na vifaa tiba
habari picha na Victoria Stanslaus
habari picha na Victoria Stanslaus
MKURUGENZI WA HUDUMA NA UFUNDI WA NHIF WANAKUJA NA MIKAKATI MIZITO
Mkurugenzi wa huduma na ufundi wa NHIF amesema vifurushi walivyozindua vipya vya huduma ya afya watatoa elimu kwa kila mtu pili kila mtu ajiunge na bima ya afya ili wanusuru maisha ya watanzania amesema haya viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam
habari picha na Victoria Stanslaus
habari picha na Victoria Stanslaus
MKURUGENZII WA NHIF AWATTOA OFU WATANZANIA
Mkurugenzi wa NHIF Bernald Kongwa ameesema kuwa vifurushi vya bima walivyozindua kila mtanzania anavimudu kwani ni vya bei nafuu
habari picha na Ally Thabiti
habari picha na Ally Thabiti
NHIF KUNUSURU VIFO VYA WATANZANIA
Mwenyekiti wa bodi ya bima ya afya Taifa ANA MAKINDA amezindua vifurushi vya bima ya afya ambavyo vitawafikia hadi watu wenye vipato vidogo kwa bei nafuu zaidi lengo kumuunga mkono rais Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda
habari picha na Victoria Stanslaus
habari picha na Victoria Stanslaus
Tuesday, 26 November 2019
MBUNGE CHADEMA AJITOSA KUWANIA NAFASI YA UENYEKITI TAIFA
AGA KHAN YAELEZA SABABU ZA WATOTO KUZALIWA KABLA YA MUDA WAO
Friday, 8 November 2019
SIDO YAFUNGUA MILANGO KWA WABUNIFU
MACDONAD MAGANGA meneja mkowa wa Dar es salaam amewataka Watanzania ususani ni wabunifu kujitokeza kwa wingi kupeleka maandiko yao yanayohusiana na maswala ya ubunifu kwenye uoande wa Teknolojia na kuongeza samani ya mazao kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ambako washirki kuanzia 25 mpaka 30 ndiyo wanatakiwa kushiriki ambako leo tarehe 8 mpaka tarehe 21 mwezi huu 11 ndiyo mwisho wa kupeleka maombi yao ambako wanatakiwa kupeleka maombi yao SIDO kwa mkono au kwa S.L.P 22151, Dar es salaam au kupitia kwenye barua pepe daressalaam@sido.go.tz au kupitia tovuti hii http://www.ubunifu.or.tz na waombaji wote wanatakiwa kulipa kiasi cha pesa kisicholejesheka cha shilingi 50,000/= kupitia namba 0767 270 111 huku akisisitizi kuwa malipo haya yafanyike kupitia Control No. ambayo muombaji utapewa
Amesema haya jiji Dar es Salaam kwenye ofisi za Sido
Naye Gosbart Baitwa Mkurugenzi wa kampuni ya KRBF food Supplies ambako ofisi zake zipo geti rumo ameipongeza sido kwa kuanzisha ushindani kwa wabunifu kwani hii itasaidia kuchochea kwa ukuwaji wa viwanda kwa kasi na huku ndiyo kumuunga mkono Rais Magufuli katika kuelekea uchumi wa kati na ukuwaji wa viwanda.
Gosbert Baitwa anawapongeza SIDO kwakutoa mafunzo mbalimbali ya kuongeza samani ya mazao hii inawasaidia wajasilia mali kutengeneza bidhaa zenye ubora amesema haya kwenye mafunzo yaliondaliwa na SIDO ya siku tano yenye jumla washirki arobaini makao makuu ya SIDO.
Nae Jonathan Afisa Biashara wa SIDO amesema kuwa wanakabiliwa na uwaba wa maeneo kwani ni machache ndiyo maana wameamua kuchukua wabunifu 20 mpaka 30 hivyo changamoto hii ingetatuliwa wangechukua wabunifu zaidi ya miamoja hilindiyo lengo lao.
Habari picha na
Victoria Stanslaus
TAASISI YA UTAFITI YA AFYA YA IFAKALA YAJA NA MIKAKATI MIZITO YA KUTEKETEZA MALERIA
Mkurugenzi wa Taasisi ya afya ya Ifakala inayoshughulika na maswala ya utafiti wa Afya Tanzania Onorati Masanja wameamua kutoa chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano ili kupunguza vifo juu ya Maleria juu ya watoto hao pia wanatoa vyandalua kwa wamama wajawazito bure ili kutokomeza vifo vya maleria kwa mama wajawazito na sasa wanafanya tafiti ya matumizi ya ndala pamoja na langi mbalimbali ambako itasaidia kuondoa maleria nchini.
Taasisi ya Utafiti ya Afya Ifakala inatawi Dar es salaam, Ifakala Mkoani Morogoro na Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Mkurugenzi amesisitiza kuwatafiti zao juu ya Maleria zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa ugonjwa wa Maleria nchini na kuokoa maisha ya watu wengi.
Amesema haya Mjini Bagamoyo kwenye semina ya wanahabari.
Nae mwnahabari wa gazeti la mwananchi Lilian Timbuka kwa niaba ya wanahabari wote ameshukuru taasisi ya Utafiti ya Afya ya Ifakala kwa kuwapa mafunzo yanayousiana na maswala ya utafiti upande wa afya na namna ya kuandika habari za utafiti wa afya.
Lilian Timbuka ameitaka Taasisi ya utafiti ya afya ya Ifakala tafiti zao kuandika kwa lugha ya Kiswahili pia na amewahasa wanahabri mafunzo waliyoyapata wayatumie vizuri hii itawasaidia kuandika habari za afya kwa uweledi zaidi, ametoa wito kwa watafiti hapa nchini kutoa ushirikiano kwa wanahabari katika kutolea ufafanuzi maswala ya Afya.
Nae Dr. Shubis Kafuruki ambaye Principal Research kutoka taasisi ya utafiti wa afya ya Ifakala amewatoa ofu wanahabari kuwawakiitaji taarifa zozote kutoka taasisi ya afya ya Ifakala milango ipo wazi na wanakaribishwa amesema taasisi yao aifanyi tafiti kwa ugonjwa wa Maleria tu inafanya utafiti na ugonjwa wa HIV na magonjwa mengineyo ikiwemo TB.
Dr. Shibis Kafuruki amesema katika malengo yao matano kwenye utafiti maswala la kufanya semina na mafunzo kwa wanahabari ni moja ya malengo yao ivyo wameahidi kudumisha umoja, Ushirkiano na kuweka nguvu kwa pamoja katika maswala ya afya na wanahabari.
Amesema haya wakati akifunga semina kwa wanahabari mjini Bagamoyo kwenye mkoa wa Pwani kwenye Taasisi ya Afya ya Ifakala.
Pichani wanahabari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na Taasisi ya utafiti ya afya ya Ifakala mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Habari picha na
Victoria Stanslaus
Wednesday, 6 November 2019
MWANACHAMA WA CUF ATOA SHUTUMA MZITO KWA CCM
Rahma Ally Mkasi ni mwanachama wa CUF kutokea manzese ameraani vikali kitendo cha CCM kuvuruga uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani na yeye jina lake limehenguliwa katika kugombea nafasi ya ujumbe kwa upande wa wanawake hivyo ameitaka CCM kuacha kuingilia uchaguzi kwani watasababisha machafuko makubwa nchini amesema haya Makao Makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam.
Ally Thabiti
TUNU YA AMANI NA USALAMA KUTOWEKA KWA SABABU YA UCHAGUZI
Mwenyekiti wa chama cha CUF Professorial Ibrahim Aruna Lipumba amemtaka Rais Magufuli kuingilia kati uchaguzi wa serikali za mitaa kwani watendaji wanavuruga utaratibu wa uchaguzi pamoja na kanuni zinazowekwa kwa kuwaengua wagombea wa vyama vingine na kuwabambikia kasi ambako katika mkoa wa Lindi, Bagamoyo, Kinondoni, Kigamboni, Tabora wagombea wa chama cha CUF, CHADEMA na vyama vyengine wameondolewa kuwania nafasi za wenyekiti wa serikali za mitaa vitongoji na vijiji.
Hivyo wamevunja kanuni ya kumi na tano B Lipumba amewataka marais wastaafu akiwemo kikwete, Mkapa na Mwinyi kuingilia kati swala hili ili kunusulu amani na usalama visitoweke, Pia ametaka urejeshwaji wa fomu uwongezwe waliokatwa walejeshwe CUF inaraani vikali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuwepo kwa ufisadi na rushwa kwa watendaji wa kata.
Naye aliyetoka CCM kuingia chama cha CUF Mwalami Gundumu amewataka watendaji kuacha kufanya ubazilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ameingia chama cha CUF kwa ajili ya kufwata haki na amehipata kwani ndani ya CCM kata ya kijichi vimejaa vitendo vya Rushwa ufisadi pamoja na ubadhilifu anakishukuru chama cha CUF kwa kumpokea kwa mikono na moyo mmoja.
Naye Mzee Uredi amesema ametoka chama cha CCM kata ya Kijichi ameingia chama cha CUF kwani viongozi wa CCM amejaa Ukilitimba ikiwemo kukatwa kwa viongozi wizi wa kura ndani ya CCM.
Naye Mzee wa CUF kutoka Mlali Mkoa wa Morogoro Mzee Abdallah amemlani vikali mtendaji msaidizi wa kata ya Mlali kwa kuwafanyia ubadhilifu ambako wamekata majina ya wana CUF hivyo wamemtaka Rais Magufuli kutofumbia macho vitendo hivi kwani vitaleta machafuko makubwa nchini ikiwemo kumwagika kwa Damu za Watanzania amesema haya kwenye makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam.
Habari picha na
Victoria Stanslaus
Saturday, 2 November 2019
TBS YATANGAZA VITA KARI KWA WAINGIZAJI NA WASAMBAZAJI WA VIPODOZI FEKI
Shirika la viwango Tanzania TBS limepiga marufuku vipodozi vyovyote kutoka nje kuingizwa nchini bila kufanyiwa maombi kupitia njia ya mtandao ya tovuti ya anuani ya shirika hilo
Hatua hiyo ni mkakati wa TBS kutaka kuviifanyia uhakiki vipodozi vyote vinavyoingizwa nchini Kama ambavyo vimeruhusiwa kwa matumizi ya Tanzania ama la
Marufuku hiyo imetolewa na mkaguzi mwandamizi wa viwango TBS Donald Manyama wakati wa zoezi la ukamataji wa vipodozi vyenye viambata sumu linaloendelea kwenye maduka ya jumla na rejareja jijini Dar es Salaam.
Amesema kumekuwa na wimbi la uingizwaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku ambapo wafanyabiashara wengi wanadai wanapoagiza hawajui vimeruhusiwa ama lah hivyo uhakiki utasaidia kutoa taarifa ni vipodozi vipi vinarusiwa vipi haviruhusiwa.
Pia Donald Manyama Mkaguzi Mwandamizi TBS akaelezea walivyojipanga kukabiliana na wale wote wasio waaminifu watakapenyeza vipodozi hivyo kwa njia ya panya.
Yamesema haya na Donald manyama mkaguzj mwandamizi TBS.
Pichani maafisa wa TBS wakikagua vipodozi vyenye viambata vya sumu.
Habari Picha na
Ally Thabiti
WANA GDSS WARAANI VIKALI MIFUMO DUME
Janeth John Mwanaharakati wa TGNP Mtandao ambaye anahuzulia semina za GDSS amewataka Watanzania kuachana na mifumo dume kwani mifumo hii imekuwa kandamizi kwa wanawake katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na katika kujikwamua kiuchumi amepongeza semina za GDSS kwani zimemjengea uwezo mkubwa katika maswala ya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.
Naye mshirki wa semina za GDSS Nepo Musenti amesema semina za GDSS yeye ameweza kuelimisha jamii anapoishi kuachana na maswala ya ukatili wa kijinsia hivyo ameiyomba TGNP Mtandao waendeleza kuzitoa semina hizi za GDSS kwa kasi kubwa kwani zimeweza kuleta mafanikio makubwa kwa jamii ambako kumepelekea kupungua kwa maswala ya ukatili wa kijinsia nchini ambako kila jumatano kuanzia saa 9 mpaka saa 11 semina hizi za GDSS zinatolewa Mabibo kwenye ofisi za TGNP Mtandao.
Pichani ni washiriki wa semina za maswala ya jinsia na jinsi za GDSS kutoka Temeke, Makumbusho, Mabibo, Chanika na maeneo mengineyo ya Dar es Salaam.
Habari picha na
ALLY THABITI
Subscribe to:
Posts (Atom)