Tuesday, 24 January 2023

MKURUGENZI MKUU MTENDAJI WA REA AELEZA NAMNA YA KUWAZINGATIA WAITAJI


 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Wakala wakusambaza Umeme vijijini (REA)  Mhandisi Hassan Seif  Saidy amesema katika utoaji wa  huduma zao wanawapa vipaumbele watu wenye ulemavu,wazee na wanawake.

Pia amesema kampuni zinazosambaza Umeme zinatoa Akira ndogondogo Kwa wazawa.

Habari picha na Ally Thabiti

WAZIRI WA NISHATI NA UMEME ATOA MIEZI MIWILI KWA WAKANDARASI WA REA

 January Makamba Waziri wa Nishati na Umeme ametoa miezi miwili kwa WAKANDARASI ambao wameshindwa kusambaza Umeme vijijini kupitoa mradi wakwani wakishindwa hatiwakali Zita hukuliwa dhidi yao .

Pia Tanzania itasambaza Umeme kwenye Vitongoji Kwa kiasi cha shilingi tilioni Sita 6,ivyo amewataka wakandarasi wa kitanzania wachangamkie fursa.

Habari na Ally Thabiti 

Saturday, 21 January 2023

DKT RAHMA SALIM MAHFOUDH KATIBU MTENDAJI TUME YAMIPANGO ZANZIBAR AMEPONGEZA KUWEPO KWA KONGAMANO LA KODI ZANZIBAR

 Dkt Rahma Mahfoudh Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar amewataka wazanzibar kutumia kongamano la kikodi kwaajili ya kukuza Biashara zao na uchumi wa Zanzibar.

Habari na Ally Thabiti

MWENYEKITI WA ZNCC ALI AMOUR SULEIMAN


 Mwenyekiti wa ZNCC Ndugu Ali Amour Suleiman amesema naipongeza serikali ya Zanzibar Kwa kuja na kongamano la Kodi na kuwashirikisha wafanya Biashara kwani itasaidia kutatuwa changamoto za kikodi na kudhibitiwa mfumuko wa bei Zanzibar utapunguwa Zanzibar.

Amekitaka serikali iwe inawashirikiaha wafanyabiashara kwenye maswala ya Kodi na bajeti.

Habari na Ally Thabiti

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA WA ZANZIBAR

 Omar Said Shaaban amesema ni Vem


a wafanyabiashara wa Zanzibar amewataka waeleze vikwazo vya Kodi ili serikali iweze kutatuwa .

Habari na Ally Thabiti 

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AIMIZA ULIPAJI WA FEDHA


 Naibu Waziri wa Fedha  na Mipango (JMT).Hamad Hassan Chande amewataka wazanzibar kulipa Kodi  kwani ndio maendeleo yatapatikana kama Husuma za Afya ,Elimu na Miundombinu. Amesema kongamano la kikodi litaleta tija Kwa kupanga bajeti yenye Usawa.

Habari na Ally Thabiti

WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA KONGAMANO LA KODI ZANZIBAR

 Dkt Saada Mkuya Salim Waziri wa Fedha Ofisi ya RĂ is Fedha na Mipango amesema Lengo la kongamano la Kodi ni kuboresha mifumo ya Kodi na kuiwezesha Zanzibar kukusanya Fedha za kutosha ivyo amewataka wazanzibar kutoa mawazo yao.

Habari na Ally Thabiti

Thursday, 19 January 2023

MKURUGENZI WAHOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI AIMIZA UWAZI NA UADILIFU KWENYE FEDHA ZA HIMOFILIIA


Prof Mohamed  Janabi amesema Mradi wa Ugonjwa wa Himofilia umesaidia Kwa kiasi kikubwa kuokoa Manisha ya watanzania ,ambako gharama zote za vipimo na matibabu zinatolewa na chama cha Himofilia ambako mgonjwa mmoja dawa zake milioni moja.

Kwa  mwaka zinaitajika milioni 4 Kwa mgonjwa mmoja Mradi huu ulianza tarehe 18/11/2020 ambako mpaka Sasa wagonjwa elfu sita wapi. Pia zimefunguliwa kiliniki mikoa mitano Mbeya ,Morogoro,Bugando,Dodoma na DSM ambako Kwa mwaka Jana watu 20 walifanyiwa tohara.

Prof Mohamed Janabi amekitaka chama cha Himofilia wawe wawazi na wawajibikaji ameo gezea Kwa kusema kuwa hospitali ya taifa ya muhimbili wako mbioni kuajili wataalamu wa Lugha ya Alama.

Habari na Ally Thabiti

Wednesday, 18 January 2023

KONGAMANO LA KODI KULETA MAFANIKIO TANZANIA

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Lameck Nchemba  amesema kongamano la mabadiliko ya Sera ya Kodi itasaidia Kwa kiasi kikubwa kuongezeka Kwa walipa Kodi Tanzania .

Habari na Ally Thabiti

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA ,BIASHARA NA UWEKEZAJI AKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA IFM

 Exaudi Kigae Naibu Waziri WA Viwanda na Biashara. Amesema Chuo Kikuu cha IFM kinatoa elimu ya maswala ya bima ,matumizi ya ICT katika kukuza uchumi wa kidigitali pia inawasaidia wajasiliamali wadogo nanna ya kuendesha na kukuza Biashara zao Kwa kutumia Tehama.

Ametoa wito Kwa kampuni za bima watoe elimu Kwa jamii umuhimu wa kukata bima  pia amekitaka Chuo cha IFM watengeneze wataalam wa ICT ambao watasaidia wawekezaji kuwekeza nchini na kudhibiti utapeli wa Biashara mtandaoni.


Nae Mkuu wa Chuo Kikuu cha IFM Prof Josephat Lotto amesema maadhisho ya miaka 50 ya Chuo Chao wanajivunia Kwa kuweza kutoa elimu Kwa wajasiliamali na kuwafundisha watu namna ya kukuza uchumi wao kidigitali, Pia Wana mpango wa kutoa elimu Kwa watu wenye ulemavu kuusiana na ujasilia mali.

Walikuwa wanatoa program mbili Chuo kilipoa za na Sasa zipo program 34 za masomo .

Habari na Ally Thabiti


Sunday, 15 January 2023


Picha 1 na b: Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.

Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wapya 57 (hawapo pichani) walioajiriwa na

Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo

wakati akifungua mafunzo yaliyofanyika  leo katika ukumbi wa JKCI jijini Dar es Salaam.

 

Picha 2 & 2b: Baadhi ya Wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia

Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kituo cha kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya

Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo elekezi kwa

 wafanyakazi hao yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

 

Picha 3: Daktari bingwa wa upasuaji Alex Msoka akitoa neno la shukrani kwa niaba ya

wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira ambao

wamepangiwa kituo cha kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa

mafunzo elekezi kwa  wafanyakazi yaliyofanyika  leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo

iliyopo jijini Dar es Salaam.

 

Picha 4: Afisa Utumishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kelvin Manyanga

akiwafundisha wajibu wa mtumishi wa umma wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na

Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo

iliyopo jijini Dar es Salaam.

Picha na: Ally Thabith


HIZI HAPA HATUA ZILIZOFIKIWA NA BENKI KUU YA TANZANIA (BoT) KUHUSU FEDHA YA KIDIJITALI YA BENKI KUU

 


Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la ubunifu katika mifumo ya uendeshaji wa shughuli za kifedha duniani kote kutokana na maendeleo ya teknolojia. Mojawapo ya ubunifu unaotawala katika mijadala ya kisasa ya kisera ni fedha ya kidijitali ya benki kuu (Central Bank Digital Currency [CBDC]).

Ijapokuwa inafafanuliwa kwa njia mbalimbali, CBDC ni aina ya fedha ya kidijitali katika nchi inayotolewa na kudhibitiwa na benki kuu. Kwa hiyo, inapotolewa, CBDC inakuwa fedha halali, sawa na fedha ya kawaida inayoshikika. Kulingana na maandiko mbalimbali ya kitaalamu, CBDC inaelezwa kuwa na faida nyingi kwa uchumi.

Kwa kuzingatia ukweli kwamba CBDC inaweza tu kutolewa na benki kuu, hivyo, kuwa chini ya mamlaka yake, Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikitafiti uwezekano wa kutoa CBDC yake. Katika hatua hii ya utafiti, Benki Kuu ya Tanzania iliunda timu ya wataalamu wa fani mbalimbali kuchunguza vipengele vya kiutendaji vya CBDC na kuijengea uwezo timu hiyo kwa njia mbalimbali.

 Pia, katika kuongeza uelewa wa CBDC kwa umma, Benki Kuu ya Tanzania iliandaa Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini Tanzania mwaka 2021 ukiwa na mada kuhusu CBDC na fedha za kidijitali (crypto). Aidha, Benki Kuu ya Tanzania ilikutana na wadau wa sekta ya fedha nchini ili kupata maoni yao kuhusu suala hili. 

Pia, Benki Kuu imenufaika na mikutano mbalimbali ya kimataifa kama vile ya Kamati ya Magavana wa Benki Kuu ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Kamati ya Masuala ya Fedha ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kupitia Kituo cha IMF cha kanda (IMF AFRITAC), na Muungano wa Benki Kuu za Afrika. Benki Kuu ya Tanzania pia ilifanya vikao kadhaa na kampuni binafsi za kimataifa zinazotoa miundombinu na ufundi kwa CBDC.

Mambo muhimu yaliyozingatiwa wakati wa hatua hii ya utafiti ambayo Benki Kuu ya Tanzania inaendelea nayo ni kuchagua namna inayofaa katika kutumia CBDC
 

kulingana na muktadha wa Tanzania. Hii inahusisha aina ya CBDC itakayotolewa (jumla, rejareja au mchanganyiko wa zote mbili), miundo ya utoaji na usimamizi (ya moja kwa moja, isiyo ya moja kwa moja, au ya mseto), aina ya CBDC (token-based au account based), muundo (remunerated au non-remunerated) na kiwango cha uwazi au ufuatiliaji. Aina itakayochaguliwa inapaswa kuzingatia vihatarishi vya utoaji wa fedha ya kidijitali ya benki kuu na njia za kudhibiti hivyo vitahatarishi katika utoaji na utumiaji wa fedha hiyo.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na Benki Kuu ya Tanzania yalibainisha kuwa zaidi ya nchi 100 duniani ziko katika hatua tofauti za kutaka kutumia fedha ya kidijitali ya benki kuu, 88 zikiwa katika utafiti, 20 katika uthibitisho wa dhana, 13 katika majaribio na 3 katika uzinduzi. Uchambuzi wa matokeo haya unaonyesha kuwa benki kuu nyingi duniani zinakwenda kwa tahadhari katika utekelezaji wa mpango wao wa kutaka kutumia fedha ya kidijitali ya benki kuu (CBDC) ili kuepuka hatari zozote zinazoweza kuvuruga utulivu na usalama wa uchumi wao.

Pia, ilionekana kuwa, nchi 6 zilighairi kutumia CBDC hasa kutokana na changamoto za kimuundo na teknolojia katika awamu ya utekelezaji. Changamoto za kimuundo ni pamoja na kutumia fedha taslimu katika kufanya miamala, kuwepo kwa mifumo isiyofaa ya malipo, gharama kubwa ya utekelezaji na viashiria vya hatari vya mfumo wa utoaji wa fedha uliopo.

Katika kuzingatia hili, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kutumia mbinu ya kwenda hatua kwa hatua, ikichukua tahadhari na kuzingatia vihatarishi katika kutumia fedha ya kidijitali ya benki kuu. Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kufuatilia, kutafiti na kushirikiana na wadau, zikiwemo benki kuu nyingine, katika jitihada za kufikia matumizi ya fedha ya kidijitali ya benki kuu na kuchagua teknolojia stahiki kwa ajili ya utoaji wa

shilingi ya Tanzania katika mfumo wa kidijitali. Baada ya kuhitimisha awamu ya utafiti, Benki Kuu ya Tanzania itatoa taarifa kwa umma kwa ujumla juu ya namna ya kusonga mbele. Taarifa hiyo inaweza kujumuisha mpangokazi katika kuanzisha fedha ya kidijitali ya benki kuu (CBDC) nchini.

Mafuriko: Mvua kubwa yawakumba wakazi wa Morogoro, Mama aangua kilio Mbele ya Mbunge

Hali ya Taharuki imewakumba wakazi wa kata za Lukobe,Kihonda  na Mkundi Manispaa ya Morogoro baada ya mvua Kubwa kunyesha usiku wa kuamkia Leo na kusababisha mafuriko katika maeneo hayo.



habari kamili

Tambo za Mandonga nchini Kenya aahidi Ushindi, ‘Wanyonyi nitampiga ngumi Sugunyo’

 


Ni January 13, 2023 ambapo Bondia Kareem Mandonga amezungumza kuhusu pambano lake dhidi ya mpinzani wake Daniel Wanyonyi huko nchini Kenya linalotarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa KICC nchini Kenya.

habari picha na Ally Thabith

Mamlaka yatoa nauli mpya Mwendokasi, Taxi

 


Kupitia ukurasa wake mtandao wa kijamii wa Instagram, Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), wametangaza nauli mpya za mabasi ya mwendo wa haraka zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia Jumatatu, Januari 16, 2023 huku nauli kwa Wanafunzi zikibaki kama zilivyo.

Katika ukurasa huo, DART imeandika kuwa, “Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), unapenda kuwaarifu watumiaji wa mabasi yaendayo haraka kuwa kuanzia Jumatatu, Januari 16, 2023 nauli mpya zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) zitaanza kutumika.”

Taarifa hiyo imeonyesha kuwa nauli katika njia kuu  ya Kimara-Kivukoni, Kimara-Gerezani na Kimara-Morocco itakuwa Shilingi 750 wakati Kimara-Mbezi nauli itakuwa Shilingi 500 na njia ya Kimara – Kibaha na Kimara-Mlongazila itakuwa Shilingi 700, huku Gerezani –Muhimbili ikiwa Shilingi 750.

Vishikambwi 3782 wapewa walimu wa Dar es Salaam

 Mkuu wa wilaya ya ilala yaikabidhi vishikwambi kwa walimu wa mkoa wa Dar es salaam 3782 lengo walimu watumie katika kufundishia nae afisa takwimu wa elimu mkoa wa Dar es Salaam Asha Mapunda amemshukuru Rais Dr. Suuhu Hassani kwakutoa vishikwambi kwa walimu pia amesema wanafunzi wenye ulemavu watafundishwa bila shida amesema haya kwenye shule ya msingi ya Diamond Dar es Salaam wakati akikabidhiwa vishikwambi.


Habari picha na Ally Thabit

Ajali ya Lori, Gari dogo yauwa wanne wa familia moja

 


Takriban watu wanne wamefariki Dunia, baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha magari mawili aina ya Toyota Spacio na Lori kugongana uso kwa uso katika eneo la Kwambe Wilayani Kilosa lililopo Barabara kuu Morogoro – Dodoma.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mukama amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari dogo kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Habari picha na Ally Thabit

Mabadiliko CCM: Sophia Mjema Katibu wa itikadi na uenezi

 


Wajumbe saba kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wametangazwa hii leo baada ya kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ameteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, akichukua nafasi ya Shaka Hamdu Shaka.

Katika Kikao hicho kilichofanyika hii leo Januari 14, 2023 na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati kuu ya CCM iliketi na vikao vyote vilihitimishwa chini ya mwenyekiti wake kwa kutangaza safu mpya za wajumbe wa NEC na kuidhinisha sekretarieti.

habari picha na Ally Thabith

WAZIRI WA ARDHI ATOA ONYO KWA KAMPUNI ZA UPIMAJI

 Angelina Mabula waziri wa ardhi nyumba na makazi amezifungia kampuni saba na zingine kumi na tano za upimaji ardhi kushindwa kutekelezwa mikataba.

Habari kamili na Ally Thabith