Picha 1 na b: Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wapya 57 (hawapo pichani) walioajiriwa na
Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo
wakati akifungua mafunzo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa JKCI jijini Dar es Salaam.
Picha 2 & 2b: Baadhi ya Wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia
Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kituo cha kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo elekezi kwa
wafanyakazi hao yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha 3: Daktari bingwa wa upasuaji Alex Msoka akitoa neno la shukrani kwa niaba ya
wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira ambao
wamepangiwa kituo cha kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa
mafunzo elekezi kwa wafanyakazi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo
iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha 4: Afisa Utumishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kelvin Manyanga
akiwafundisha wajibu wa mtumishi wa umma wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na
Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo
iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Ally Thabith
No comments:
Post a Comment