Wajumbe saba kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wametangazwa hii leo baada ya kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ameteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, akichukua nafasi ya Shaka Hamdu Shaka.
Katika Kikao hicho kilichofanyika hii leo Januari 14, 2023 na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati kuu ya CCM iliketi na vikao vyote vilihitimishwa chini ya mwenyekiti wake kwa kutangaza safu mpya za wajumbe wa NEC na kuidhinisha sekretarieti.
habari picha na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment