Exaudi Kigae Naibu Waziri WA Viwanda na Biashara. Amesema Chuo Kikuu cha IFM kinatoa elimu ya maswala ya bima ,matumizi ya ICT katika kukuza uchumi wa kidigitali pia inawasaidia wajasiliamali wadogo nanna ya kuendesha na kukuza Biashara zao Kwa kutumia Tehama.
Ametoa wito Kwa kampuni za bima watoe elimu Kwa jamii umuhimu wa kukata bima pia amekitaka Chuo cha IFM watengeneze wataalam wa ICT ambao watasaidia wawekezaji kuwekeza nchini na kudhibiti utapeli wa Biashara mtandaoni.
Nae Mkuu wa Chuo Kikuu cha IFM Prof Josephat Lotto amesema maadhisho ya miaka 50 ya Chuo Chao wanajivunia Kwa kuweza kutoa elimu Kwa wajasiliamali na kuwafundisha watu namna ya kukuza uchumi wao kidigitali, Pia Wana mpango wa kutoa elimu Kwa watu wenye ulemavu kuusiana na ujasilia mali.
Walikuwa wanatoa program mbili Chuo kilipoa za na Sasa zipo program 34 za masomo .
Habari na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment