MAELEZO YA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
YA MHE. MKUU WA MKOA WA DSM KWA NIABA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZIJUU
YA TUKIO LA SHUGHULI YA KUFUNGA MRADI WA MAJARIBIO WA MPANGO WA
HATUA KUMI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA SALAMA NCHINI TANZANIA
Tarehe 2 Machi, 2023
Habari za asubuhi kwenu nyote.
v Napenda kutoa shukrani zangu za dhati
kwa taasisi zilizofanikisha Mradi huu kwa Tanzania, ambazo ni:
i.
Mfuko
wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani, UK Aid, na Global Road Safety
Facility ya Benki ya Dunia kwa ufadhili wa Mpango huu.
ii.
Tume
ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (UNECA) kwa kuwa taasisi ya Umoja wa
Mataifa inayotekeleza mradi huo.
iii.
Shirikisho
la Barabara la Kimataifa (IRF) ambalo makao makuu yake yako Geneva, Uswizi kwa
kuwa kiongozi wa mradi, na Mpango wa Kimataifa wa Tathmini ya Barabara (iRAP),
Chama cha Barabara Duniani (PIARC) na Chama cha Barabara Tanzania (TARA) kwa
kufanya kazi kama taasisi washirikakatika utekelezaji wa mradi huu hapa nchini Tanzania.
Pongezi zangu pia
ziwaendee wadau wote kwa kuhusika kikamilifu katika mradi huu ambao umeifanya
Tanzania kuwa nchi ya kwanza kabisa duniani kutekeleza Mradi wa Majaribio wa Mpango wa Hatua Kumi wa Miundombinu
ya Barabara Salama nchini Tanzania. Tunajisikia fahari kupata fursa hii
na kwa matokeo ambayo miezi hii 30 ya kazi ya pamoja imeleta. Leo tupo
kusherehekea kwa pamoja mafanikio haya ambayo utekelezaji wake utasaidia
kuifanya nchi yetu kuondokana na barabara hatarishi.
v Ripoti ya Hali ya Kimataifa ya
Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu Usalama Barabarani ya mwaka 2018
inakadiria kuwa zaidi ya watu 16,000 huuawa kwenye
barabara za Tanzania kila mwaka. Vifo vingi huwa ni vijana. Usalama barabarani ndio
chanzo kikuu cha vifo vya watoto na vijana wenye umri wa miaka 5-29.
Tumepewa dhamana na watanzania na
hivyo tunalazimika kuchukua hatua na kubadili mwelekeo huu na Mradi wa Hatua
Kumi umetupatia maarifa, ujuzi na zana za kufanya hivyo.
Septemba mwaka 2022tulikuwa na uzinduzi
wa Programu ya Kitaifa ya Kutathmini
Viwango na Usalama wa Barabara Tanzania (TanRAP) ambayo inaipatia nchi yetu
jukwaa la kubadilishana na kujifunza kutoka kwa mataifa mengine, kupitisha
viwango vya kimataifa vya ubora wa usalama wa barabara zetu kwa kuzipatia
madaraja ya nyota 3 au zaidi kwa watumiaji wote wa barabara na kujenga uwezo na
maarifa ya ndani kwa nchi yetu kwa siku zijazo.
Leo, shukrani pia kwa mradi huu wa
Hatua Kumi, karibu Km 10,000 za barabara na miundo zimefanyiwa tathmini kupitia
mbinu za iRAP ili kubaini usalama uliojengwa ndani ya barabara zote zilizopo na
barabara zinazopendekezwa kuboreshwa. Tathmini hizo zimethibitisha kuwa hatua
za usalama barabarani zitapunguza hatari za vifo barabarani na kuwa na faida
kubwa kwenye uwekezaji.
v Makadirio ya gharama ya kila mwaka ya
vifo na majeraha makubwa nchini Tanzania hugharimu dola za Marekani bilioni 4.1
sawa na asilimia 8.2 ya Pato la Taifa. Kwa hiyo, Ajali za barabarani zinawakilisha
changamoto kubwa kwa Tanzania ambayo inahitaji mikakati na mipango ya kutosha.
Kupitia Mradi wa Hatua Kumi, wadau wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa muda katika kuandaa
rasimu ya mapendekezo ya mkakati mahususi wa usalama wa miundombinu ya barabara
na mpango kazi na ninayofuraha kushuhudia leo matunda ya kazi hiyo ambayo
yataarifu hatua ya serikali tunapoandaa mkakati wa jumla wa usalama barabarani
kwa nchi na tunapoandaa mipango ya uwekezaji wa barabarani. Mpango ulioandaliwa
katika mfumo wa Mradi wa Hatua kumi unawasilisha mkakati wa kitaifa wa usalama
wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania kwa kipindi cha 2021-2030. Mpango wa
utekelezaji unalenga kutoa maendeleo, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya
hatua za usalama. Kama ilivyoripotiwa katika ripoti, uwekezaji wa takriban 0.15%
wa pato la Taifa (GDP) kwa mwaka hadi kufikia 2030 utakuwa umewezesha kwa
kiwango kikubwa kuokoa maisha ya watu 7,100 kwa mwaka na pia USD 26 ya faida
itapatikana kwa kila USD 1 itakayowekezwa.
v Ingawa hatua nyingi zinazohitajika
ili kuokoa maisha ni rahisi kitaalamu na ni rahisi kujenga, kuna vikwazo vingi
vya kufikia na kudumisha matokeo ya usalama barabarani nchini Tanzania. Viwango
vilivyopitwa na wakati, na miongozo ni sehemu ya vikwazo hivyo. Tunashukuru kwa
juhudi ambazo zimefanywa na wengi wenu katika kuandaa rasimu ya mapendekezo ya
marekebisho ya Mwongozo wa Usanifu wa Kijiometri wa Barabara Tanzania (RGDM)
ili kutathmini ufaafu wake katika kushughulikia mahitaji ya usalama wa
watumiaji wote wa barabara na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa
Mataifa (UNSDG) namba 3 na 4 kwa usalama wa barabara mpya na zilizopo.
v Maarifa,
ujuzi na ufahamu wa uhandisi usalama barabarani bado ni mdogo kati ya wataalamu
wa usafiri katika nchi yetu. Nimefurahishwa kujua kwamba shughuli za kujenga
uwezo wa Mradi wa Hatua Kumi kwa ujumla zimefikia zaidi ya wataalamu 500 wa
Kitanzania na kwamba sasa tunaweza kutegemea wataalamu 150 ambao kupitia kozi
za Mradi wa Hatua Kumi wamethibitishwa katika Uhandisi wa Usalama Barabarani. Tathmini
za iRAP, Ukadiriaji wa Nyota wa Miundo na Ukaguzi wa Usalama Barabarani.
Tumepanga kuweka ari na kasi
sawa, kutoa mafunzo kwa watu wengi zaidi na kufanya maendeleo kwa nchi yetu na
watu wetu kupitia mpango wa kitaifa wa mafunzo na ithibati kama ilivyoandaliwa
na Mradi wa Hatua Kumi kufuatia mapitio ya kina ya mafunzo yaliyopo na tathmini
ya mapungufu ya mafunzo.
Sasa tuendelee na kazi nzuri
na tuifanye kwa pamoja Tanzania bila barabara hatarishi!
Ahsanteni Sana.