Kamishina Uhamiaji Nchini Tanzania Dr Ana Makakala amesema lengo la nchi ya tanzania kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji kutoka nchi ya Drc Kongo Roland Kashwakale ni kuhimarisha ulinzi na usalama kati ya Tanzania na Drc Kongo na kukuza uchumi wa nchi zote mbili Pamoja na kuleta maendeleo.
Dr Ana Makakala Kamishina Mkuu wa Uhamiaji nchini tanzania amesema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu jeshi la Uhamiaji la tanzania limeweka nguvu kubwa mipakani kote kwenye nchi zinazozunguka tanzania kwaajili ya kudhibiti wahamihaji ambao awana vibali vya kuingia tanzania hili kuimarisha ulinzi na usalama wa tanzania kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Dr Ana Makakala amesisitiza kuwa tanzania itaendelea kufanya mikutano yake na nchi za Rwanda, Burundi,Uganda na nchi zinginezo.
Mfano Mkutano wa Drc Kongo na Tanzania ni mwanzo tu wa mikutano mingiyo Dr Ana Makakala ametoa wito kwa watu wanaotaka kuja tanzania wafuate kanuni,miongozo,taratibu na sheria kabla awajaingia tanzania .
Amesema haya jijini dar es salaam
Habari picha na Ally Thabit Mbungo.