Thursday, 19 July 2018

SERA YA MAADILI NDO MWAROBAINI KABAMBE KWA WATUMISHI

Mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh Ali Hapi amesema sasa ni wakati muafaka kuanzishwa na kuwepo kwa sera ya taifa inayohusu maadili ili tupate sheria ambayo itawabana na kuhukumu viongozi na watumishi wa serikali  ambao wanakiuka misingi ya maadili kwenye kazi zao amesema haya kwenye mkutano ulioandaliwa na tume ya maadili kwa viongozi wa umma katika ukumbi wa Anatogo jijini Dar es salaam

MAGIZO YA WAZIRI WA ELIMU ,SAYANSI NA TEKNOROJIA YA VUTA HISIA NZITO

Naibu makamu mkuu wa chuo cha SUA(utawala wa fedha) prof,  Yonika Ngaja amesema maagizo yaliotolewa na waziri wa elimu wa sayansi na teknolojia prof Joyce Ndalichako ya vyuo vyote vifanye tafiti zenye kutatua matatizo ya jamii wamepokea na watatekeleza kwa vitendo pia vyuo ambavyo havijakidhi viwango na vigezo suala la kufutwa hatua vitachukuliwa kwa vyuo hivyo ilikupata wanafunzi bora  na elimu bora kwa lengo la kuelekea Tanzania ya viwanda lifanikiwe kwa kiasi kikubwa kuweza kupata wataalam wengi na wenye ujuzi amesema hayo wakati wakutoa neno la shukrani kwa waziri wa elimu,sayansi na teknolojia prof Joyce Ndalichako  wakatiwa kufungua maonyesho ya 13 ya vyuo vikuu ya siku nne kuanzia 18/07/2018 mpaka 20/07/2018 mnazi mmoja jijini Dar es salaam, habari picha na Ali Thabit
 

WADAU WA ASASI ZA KIRAIA, KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU WAKISHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE SERA MPYA

Wadau mbalimbali wakutana kwenye hoteli ya Wanyama iliyoko Sinza jijini Dar Es Salaam kwaajili ya kujadili sera mpya kwa asasi za kiraia kupitia kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu LHRC ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani ya Tanzania


ASASI ZA KIRAIA WATAKIWA KUUNGA MKONO SERA MPYA

Ismail Abdunuru Sulemani katibu mkuu wa asasi za kiraia nchini Tanzania zisizo za kiserikali amezitaka asasi zote nchini kuunga mkono jitihada na juhudi za serikali katika kubadilisha sera za asasi za kiraia kwa kushiriki katika utoaji wa maoni kwa lengo la kuondoa sera ya mwaka 2001 kwa kuleta sera mpya kwaajili ya kuendana na wakati wa sasa amesema haya kwenye mkutano ulioandaliwa na kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu LHRC uliofanyika sinza mori katika Wanyama hoteli jijini Dar es salaam.habari picha na Ali Thabit

WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO WAIPATANO SIDO

viongozi wa sido sabasaba
mjasiriamali Danius akiongea
Mjasiriamali Dainus Zabron Kaindi amesema amenufaika na elimu ya usindikaji wa mbogamboga za majani kupitia sido hivyo amewataka watanzania waweze kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na sido kwakuwa fursa hizo zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa watanzania katika wimbi la umasikini
mjasiriamali Lucia akiongea
Pia Lucia Cosmas amesema sido imemsaidia kwa kiasi kikubwa katika kutangaza bidhaa zake za furnituch kitaifa na kimataifa na amekiri waziwazi kuwa sido inaunga mkono adhima ya rais Magufuli kwa vitendo kuelekea Tanzania ya viwanda kwa kuwaibua na kuwainua watu wa viwanda vidogovidogo kwa kuwapa elimu,kuwatia moyo pamoja na masoko 




  wamesema hayo katika maonyesho ya 42 sabasaba Dar es salaam.                                  habari picha na Ali Thabit

SIDO YAWAFUTA MACHOZI WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO


mjasiriamali Merry akiongea na mwandishi
Mjasiriamali Merry kutoka sinza ameto shukrani zake kwa Sidokwakuweza kumtafutia masoko ya kuuza bidhaa zake za vipochi na bidhaa zingine anazotengeneza kwa shanga na ameweza kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya biashara ya kitaifa na kimataifa ambapo kumemjengea uwezo wa kibiashara na ameweza kunufaika kwa kukuwa kwa kipato cha uchumi wake pia ametowa wito kwa wafanyabiashara na watanzania wasisite kwenda sido kwa kupata elimu ya ujasiliamari 
baadhi ya bidhaa ya mjasiriamali Merry
Rasi Jeshi Beku akiongea na mwandishi wetu
Naye Rasi Jeshi Beku amesema sido ni mkombozi wa waanzilishi wa viwanda vidogovidogo hususa ni wanyonge na waliokata tamaa hili amelidhibitisha yeye baada ya kunufaika na elimu ya kutengeneza vikoi kutoka sido ambapo hapo awali alikuwa na malengo hayo lakini hakuwa na sehemu ya kuanzia hivyo ameshukuru na kuipongeza sido kwa kumuinua kwa namna moja au nyingine





wamesema hayo kwenye maonyesho ya biashara ya 42 sabasaba Dar Es Salaam habari picha na Ali Thabiti

Monday, 16 July 2018

BENKI KUU YA TANZANIA (B.O.T) YA ELEZA NAMNA YA KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI TANZANIA

Mchumi mwandamizi kutoka kurugenzi ya uchumi kutoka benki kuu ya Tanzania(B.O.T) mh Lusajo Mwamkemwa amesema wao wanajukumu lakudhibiti mfumuko wa bei wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa kushirikiana na ofisi ya taifa ya takwimu ambapo mfumuko wa bei unaweza kudumu kwa mwezi mmoja au miezi mitatu pia amesema mdhara ya mfumuko wa bei unaathiri maendeleo ya uchumi wa taifa.
Pia wao kama benki kuu huweza kusaidia njia mbalimbali kwaajili ya kudhibiti mfumuko wa bei  kwa kutoa elimu kupita redio,televesheni,magazeti na maonyesho mbalimbali ya kitaifa kama sabasaba na nanenane, amesama hayo kwenye maonyesho ya biashara ya 42 sabasaba jijini Dar es salaam habari picha na Ally Thabit