Wednesday, 26 June 2019

DAR RUNNING MARATHON

DAR RUNNING MARATHON wapewa TANO


Mshiriki wa Dar running Marathon amewapongeza waandaaji wa mashindano hayo kwani wamewakutanisha na watu mbalimbali pia wameweza kujifunza na kupata uelewa juu ya umuhimu wa kushiriki mashindano ya riadha na pia amewataka waweze kutanua wigo mkubwa zaidi wa mashindano hayo hayo yamesema jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya coco beach kwenye bwalo la maafisa wa jeshi la polisi na mmojab wa washiriki hao.

Habari Picha na ALLY THABIT

DAR RUNNING MARATHON

Mshindi wa Dar Running Marathon atoa neno
Manywele ni mshindi wa mbio za kilometa 21 ambaye ameshinda nafasi ya kumi amewataka watanzania kushiriki kwenye mbio za Dar RUNNING MARATHON kwakuwa ni moja ya sehemu tya mazoezi na kuimarisha afya pia amewapongeza waandaji wa mashindano hayo kwani yeye ameweza kuonyesha kipaji chake na uwezo wake na anaamini kupitia mashindano hayo ataweza kushiriki mashindano ya kit6aifa na kimataifa.

Mashindano hayo yalikuwa na washiriki zaidi ya elfu mbili kutoka afrika mashariki kwa kilomita 21 nafasi ya kwanza hadi ya tatu ilishika na watanzania.

Habari picha na ALLY THABITI


Friday, 21 June 2019

KUELEKEA AFCON 2019: CAF YAZITAHADHARISHA TIMU KUJIANDAA KUCHEZA KWENYE JOTO KALI

Ikiwa leo michuano ya Kombe la Afrika (AFCON) mwaka 2019 ndio inaanza kutimua vumbi nchini Misri, mataifa 24 yatakayoshiriki mtanange huo yameonywa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kwamba yajiandae kwa mashindano yatakayochezewa kwenye joto kali.

Taarifa kutoka nchini Misri ambako mashindano haya yatafanyika kuanzia leo Juni 21 hadi Julai 19 zinasema kwamba Kamati ya mashindano inayojihusisha na masuala ya afya kwenye CAF imeitisha mapumziko ya lazima ya dakika tatu baada ya dakika 30 za kwanza na pia itakapogonga dakika ya 75, mbali na yale ya kawaida ya dakika 15 kipindi cha kwanza kinapomalizika.

Mashindano haya makubwa barani Afrika yalihamishwa kutoka tarehe zake za kawaida za Januari na Februari hadi Juni na Julai kwa mara ya kwanza kutokana na mivutano kati ya klabu na nchi. Hali ya joto nchini Misri wakati huu inatarajiwa kufikia kati ya nyuzi joto 35 na 38.

SERIKALI YA TANZANIA YAJIPANGA KUTEKA SOKO LA WATALII CHINA

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwa sasa muelekeo wa soko la Utalii nchini umelenga kupata watalii wengi kutoka nchini China na kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Utalii,  suala la  kujifunza lugha ya kichina kwa baadhi ya watumishi na wadau wa utalii ili kuteka soko hilo ni jambo lisiloepukika.

Imesema nguvu nyingi kwa sasa zinaelekezwa nchini China hivyo  ni muda muafaka wa kuandaa timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo  waongoza watalii watakaoweza kuzungumza lugha ya kichina ili kuweza kulimudu soko hilo.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu  wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa  Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS.

Amesema  lengo mkutano huo ni  kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania katika suala la kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa Utalii nchini.

Mkutano huo  umehudhuriwa na ujumbe kutoka China ukiongozwa na Makamu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong,Kaimu huku kwa upande wa Wizara  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Lucius Mwenda pamoja na ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.

Amesema ni muhimu kwa watumishi wa wizara pamoja na wadau wa utalii kujiandaa ili kuweza kuzungumza lugha ya kichina badala ya vifaa maalum vya kutafsiri lugha ilhali kuna uwezekano kwa Watanzania kujifunza.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong amesema wamejipanga kutoa mafunzo mbalimbali likiwemo suala la lugha ya kichina pamoja na utalii ili kuwajengea uwezo Watumishi hao.

Ameongeza kuwa tayari wameshaomba kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala Bora  kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lucius Mwenda  ameahidi kutoa ushirikiano kwa Uongozi wa Chuo hicho ili  kujengeana uwezo  baina ya Serikali ya  Tanzania na China.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 21, 2019.














Wednesday, 19 June 2019

MOI WAJITOLEA KUWAFANYIA UPASUAJI WATOTO 15

 Madaktari bingwa wa MOI wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye kichwa kikubwa katika kambi maalum iliyofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akikagua jalada na kuzungumza na mgonjwa anayesubiri kufanyiwa upasuaji katika chumba cha upasuaji MOI.
 Kaimu mkurugenzi wa huduma za Uuguzi MOI Elizabet Mbaga akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa mkuu wa kitengo cha Mawasiliano, Uhusiano na elimu kwa Umma mfuko wa fidia kwa wafanyakazi Bi. Laura Kunenge
   Watumishi wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya MOI ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari katika vyumba vya upasuaji MOI katika kambi maalum ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongowazi ambayo imefanyika kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma na kuanzishwa kwa taasisi ya MOI miaka 23 iliyopita.
Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya fahamu MOI Dkt Hamis Shabani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vyanzo na matibabu ya kichwa kikubwa na mgongo wazi katika vyumba vya upasuaji MOI.

NA KHAMISI MUSSA
Watumishi wa Taasisi ya tiba ya Mifupa ya MOI leo wamejitolea kuendesha kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma pamoja na  miaka 23 toka Taasisi ya MOI kanzishwa.

Shuguli nyingine zimehusisha uchangiaji wa damu kwa hiari, usafi wa mazingira katika maeneo ya hospitali pamoja na kutoa zawadi na misaada ya kijamii kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa wodini.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface aliwaongoza watumishi katika shughuli zote za usafi, kuchangia damu pamoja na kambi ya upasuaji.

“Leo tunafanya kazi kwa kujitolea ikiwa ni sehemu ya wiki ya utumishi wa Umma na pia ni wiki ya maadhimisho ya miaka 23 ya kuanzishwa kwa Taasisi yetu ya MOI mwaka 1996, hivyo nimeshiriki kikamilifu na watumishi wenzangu ili kuonyesha mfano kama kiongozi” Alisema Dkt Boniface
Aidha, watumishi wa MOI wamepata fursa ya kupata mafunzo maalum kutoka kwa wataalamu wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kufanya kazi katika mazingira salama.

Pia, watumishi kutoka mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) wameshiriki katika kufanya usafi katika mazingira ya Taasisi ya MOI pamoja na kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.