Tuesday, 17 May 2022

JAJI MSTAAFU TOMASI MIHAYO APONGEZA JUHUDI ZA RAIS SAMIA SULUHU HASSANI


 Jaji Mstaafu Tomasi  Mihayo amesema Kitendo cha rais Samia Suluhu Hassani kuzinduwa Loyo Tuwa itasaidia Kwa kiasi kikubwa kuongezeka Kwa Ajira,kukuwa Kwa uchumi na kuimarika na kukuwa sekta ya Utalii Tanzania .

Jaji Mstaafu Tomasi Mihayo amewataka watu kumuunga mkono rais Samia Suluhu Hassani Kwa vitendo. 

Habari picha na Ally Thabiti

MKURUGENZI MTENDAJI WA BODI YA UNUNUZI NA UGAVI ATANGAZA VITA KALI


 Godfred Mbanyi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa  Ununuzi na Ugavi (PSPTB) amewataka Waajiri nchini Waajili wataalam wa Ununuzi na Ugavi wenye sifa na waliosajiliwa na PSPTB lengo kuwa na wataalam wenye uweredi zaidi.

Ambako itasaidia kuondokana na upotevu wa fedha mpaka kupelekea serikali kupoteza mapato na hatinaye kukosa kukusanya Kodi,  Godfred Mbanyi amewataka wataalam wa Ununuzi na Ugavi kujisajili kwenye PSPTB .

 Yeyote atakae puuza maagizo haya hatuwa Kali za kisheria zitatumika  Ikiwemo kutozwa faini  milioni mbili na kwenda jera miakamiwili.

Mkurugenzi wa PSPTB amesema wameamuwa kuja na kampeni kwenye vyombo vya habari lengo Kutoa elimu Kwa Jamii umuhimu wa kuwaajili maafisa Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na PSPTB.

Habari na Ally Thabiti

Sunday, 1 May 2022

COSOTA YAGUSWA NA WATU WENYE ULEMAVU


 Mkurenzi mtendaji wa COSOTA, DORIS SINALE amesema kupitia mkataba wa MARA CASH utasaidia kiasi kikubwa watu wenye ulemavu kuweza kupata haki ya kuchapisha vitabu mbalimbali na majalida kupitia maandishi ya Nukta nundu kwaaajili wasioona lengo la COSOTA ni kuyafikia makundi yote.


Habari picha na Ally Thabit

WILAYA YA MKURANGA YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA.

 


KHADIJA NASRI ALI Mkuu wa Wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani amesema katika mbio za mwenge ambako wilaya ya mkuranga itatembekewa na mwenge tarehe 03/05/2022 ambapo jumla ya miradi saba itazinduliwa na mingine itawekewa mawe ya msingi thamani ya miradi hii ni kiasi cha Bilioni saba nukta sita (7.6) Bi. Khadija Nasri Ali amesema wanapongeza juhudi na jitihada za utendaji kazi za Raisi Samia Suruh Hassan ndio maana wilaya yake ya mkuranga itakeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo ya Rais Samia Suruh Hassan ikiwemo uzinduzi wa msitu wa vikindu ambao watalii zaidi ya mia tano (500) hutembelea kila mwezi na ujenzi wa miundo mbinu sehemu za kihistoria. Bi Khadija Nasri Ali ametoa wito kwa watu wote kumuombea Rais Samia Suruh Hassan na kumuunga mkono kwa moyo na vitendo pia ametoa rai kwa wanamkuranga na watanzania kwa ujumla kulinda na kudumisha amani iliyopo nchini Tanzania.

Habari Picha na Ally Thabiti

Thursday, 21 April 2022

LHRC YAJA NA RIPOTI KAPAMBE


 ANNA HENGA    Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC amesema ripoti walio izindua imebainisha changamoto mbalimbali zinazotokana na maswala ya ukatili wa kijinsia namna ya kuweza kukabilaiana na maswala ya ukatiri wa kijinsia lengo ni kutokomeza kabisa mfano ndoa za utotoni, ukatiri wanaofanyiwa watoto na wanawake mitandaoni, haki za watu wenye ulemavu, haki za wanawake wajane namna ya kumiliki mali  ANNA HENGA ameitaka Serikali na taasisi mbalimba za watu binafsi waitumie ripoti ya LHRC kwaajili yakuweza kutatua changamoto katika jamii pia amewatoa hofu watu wenye ulemavu wakuto kuona kuwa ripoti ya LHRC imeandikwa kwa maandishi nukta nuni ambao nao watapata fursa ya kusoma yaliyopo kwenye ripoti hii.

habari picha na Ally Thabith

BANK YA NBC YAJA NA MIKAKATI MIZITO





Mkurugenzi mtendaji wa NBC amesema wameamuwa kuwafikia watu kuanzia ngazi ya chinikupitia bank ya NBC lengo kuwakwamua watu kiuchumi kwa kutoa mikopo ya fedha bila masharti magumu. Amesema Bank ya NBC inaunga mkono juhudi na jitihada za Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuweka matawi kila kona ya Tanzania, ametoa rai watu waendelee kuiamini na kuitumia Bank ya NBC kwani usalama wa pesa zao ni wauhakika. Amewataka waislam huduma za NBC wajitokeze kwa wing

Amesema haya kwenye Iftar Selena Hotel 

habari picha na Ally Thatbith



SHEKH MKUU WA DAR ES SALAAM AIPONGEZA BANK YA NBC


 Alhaji Mussa Salim Shekh wa mkoa wa Dar es Salaam ameipongeza na kuishukuru bank ya NBC jinsi wanavyotoa huduma kwa kasi kubwa na namna inavyoweza kuwafikia waislam ambako wanatoa mikopo bila riba. Ametoa wito kwa watu waitumie bank ya NBC amesema haya wakati wa IFTAR selena Hotel iliyoandaliwa na BANK ya NBC.

habari picha na Ally Thabith