Sunday, 1 May 2022

WILAYA YA MKURANGA YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA.

 


KHADIJA NASRI ALI Mkuu wa Wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani amesema katika mbio za mwenge ambako wilaya ya mkuranga itatembekewa na mwenge tarehe 03/05/2022 ambapo jumla ya miradi saba itazinduliwa na mingine itawekewa mawe ya msingi thamani ya miradi hii ni kiasi cha Bilioni saba nukta sita (7.6) Bi. Khadija Nasri Ali amesema wanapongeza juhudi na jitihada za utendaji kazi za Raisi Samia Suruh Hassan ndio maana wilaya yake ya mkuranga itakeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo ya Rais Samia Suruh Hassan ikiwemo uzinduzi wa msitu wa vikindu ambao watalii zaidi ya mia tano (500) hutembelea kila mwezi na ujenzi wa miundo mbinu sehemu za kihistoria. Bi Khadija Nasri Ali ametoa wito kwa watu wote kumuombea Rais Samia Suruh Hassan na kumuunga mkono kwa moyo na vitendo pia ametoa rai kwa wanamkuranga na watanzania kwa ujumla kulinda na kudumisha amani iliyopo nchini Tanzania.

Habari Picha na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment