Friday, 27 May 2022

BRELA KUSHUSHA RUNGU LA KUYAFUTA MAKAMPUNI 5676


 
Afisa Mtenadaji Mkuu wa Brela Godfrey Nyaisa Amesema Tangu uteuzi wangu wa BRELA mojawapo ya changamoto niliyokutana nayo ni uwepo wa makampuni mengi ambayo hayafanyi kazi au shughuli yoyote ya kibiashara katika Daftari la Kampuni. Yapo makampuni yenye miaka zaidi ya 50 na hayana uthibitisho kuwa yanafanya biashara na hayawasilishi taarifa za mwaka (Annual Return) kwa kampuni zilizosajiliwa hapa nchini au mizania ya Mwaka (Financial Statement) kwa kampuni zilizosajiliwa nje ya nchi. 

kifungu cha 128 cha Sheria ya makampuni, sura 212 kinazitaka kampuni zilizosajiliwa hapa nchini kuwasilisha Taarifa za mwaka " Annual Return" ambapo kutofanya hivyo kunatupa tafsiri kuwa huenda kampuni hii haifanyi biashara kulingana na lengo la uanziliashwaji wake.

Kifungu cha 438 cha sheria ya makampuni kinazitaka kampuni zilizosajiliwa nje ya nchi ambazo zina ofisi za biashara nchini kuwasilisha Mizani ya Mwaka (Financial Statement) ambazo kutofanya hivyo pia kunatoa tafsiri kuwa kampuni hizo hazifanyi biashara hapa nchini.

Vifungu vya 400 na 441 vya sheria ya makampuni vinanipa mamlaka mimi kama msajili wa makampuni kufuta makampuni ambayo hayafanyi biashara. uwepo wa makampuni mengi yasiyofanya biashara ni kinyume na sheria na ni mzigo kwa wakala kwa kutunza kumbukumbu za makampuni. Mengi ambayo hayafanyi biashara au yameshikilia majina kinyume cha sheria kwaajili ya kuwauzia watu wengine wenye uhitaji wa majina hayo.

Habari picha na Ally Thabith






habari picha Ally Tabith

No comments:

Post a Comment