Fidelis John Kutoka Chuo Kikuu SUA amemshukuru taasisi ya Utafiti wa Afya NIMR Kwa kufanya Kongamano la 31 kuanzia tarehe 17 na mwisho tarehe 19/2022 kwani Chuo Kikuu SUA kimepata fursa ya kuelimisha watu namna Panya Buku anavyoweza kutambuwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu Kwa haraka zaidi .
Fidelis John amesema kupitia Panya Buku Tanzania inaweza kutibu wagonjwa wa Kifua Kikuu Kwa wakati na haraka tena Kwa gharama nafuu ambako itapelekea pesa nyingi za serikali kuokolewa na vifo vyingi kupunguwa na kutokomeza Kifua Kikuu.
Fidelis John amesema nchi ya Marawi na Ethiopia Wamechukuwa Panya Buku Kutoka Tanzania kupitia Chuo Kikuu SUA kwaajili ya Kupambana na kutokomeza Kifua Kikuu kwenye nchi zao.
Habari na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment