Mratibu wa Asasi za Kiraia amesema wanamatumaini makubwa ya Utendaji kazi wa rais Samia Suluhu Hassani na wasaidizi wake wa Wizara akiwemo Waziri Dorith Ngwajima na Katibu Mkuu Zainabu Chakula.
Tuesday, 17 May 2022
ASASI ZA KIRAIA ZINAMATUMAINI MAKUBWA
Mratibu wa Asasi za Kiraia amesema wanamatumaini makubwa ya Utendaji kazi wa rais Samia Suluhu Hassani na wasaidizi wake wa Wizara akiwemo Waziri Dorith Ngwajima na Katibu Mkuu Zainabu Chakula.
MWENYEKITI WA ASASI ZA KIRAIA AIPONGEZA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII ,JINSIA,WATOTO,WAZEE NA MAKUNDI MAALUM
Liliani Mwenyekiti wa Asasi za Kiraia amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii imefanya kazi kubwa ya kuziunganisha Asasi zote za Kiraia nchini Tanzania, ambako Asasi hizi zimekuwa na Uhuru mkubwa wa kufanya kazi nchini.
amemshukuru Waziri Dorith Ngwajima na Katibu Mkuu Zainabu Chakula Kwa Ushirikiano na utendaji kazi wao mzuri na ulio tukuka Kwa Asasi za Kiraia za Kitaifa na kimataifa .
Habari picha na Ally Thabiti
MRATIBU WA THRDC ATOA NENO
Abdalla Abedi Mratibu wa THRDC Zanzibar amesema katika kufikisha Miaka 10 ya THRDC wameweza kunufaika Kwa kiasi kikubwa Kwa majaji na mahakimu wa Zanzibar Kwa kujengewa uwezo wa Uendeshaji wa kesi ambako imepelekea kupunguwa Kwa mrundikano wa kesi Zanzibar.
Pia wameweza Kutoa magodoro na elimu kwenye chuo cha Mafunzo .
Nae Kwa upande wake Waziri wa Latina na Sheria Dr Damasi Ndumbalo amempongeza rais Samia Suluhu Hassani Kwa kuwa mtetezi namba moja wa haki za binadamu kwenye sekta zote .
Huku Mratibu wa THRDC Onesmo Ole Ngurumo amemongeza rais Samia Suluhu Hassani Kwa Juhudi na jitihada anazofanya katika uongozi wake Kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu .
Habari picha na Ally Thabiti
JAJI MSTAAFU TOMASI MIHAYO APONGEZA JUHUDI ZA RAIS SAMIA SULUHU HASSANI
Jaji Mstaafu Tomasi Mihayo amesema Kitendo cha rais Samia Suluhu Hassani kuzinduwa Loyo Tuwa itasaidia Kwa kiasi kikubwa kuongezeka Kwa Ajira,kukuwa Kwa uchumi na kuimarika na kukuwa sekta ya Utalii Tanzania .
Jaji Mstaafu Tomasi Mihayo amewataka watu kumuunga mkono rais Samia Suluhu Hassani Kwa vitendo.
Habari picha na Ally Thabiti
MKURUGENZI MTENDAJI WA BODI YA UNUNUZI NA UGAVI ATANGAZA VITA KALI
Godfred Mbanyi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) amewataka Waajiri nchini Waajili wataalam wa Ununuzi na Ugavi wenye sifa na waliosajiliwa na PSPTB lengo kuwa na wataalam wenye uweredi zaidi.
Ambako itasaidia kuondokana na upotevu wa fedha mpaka kupelekea serikali kupoteza mapato na hatinaye kukosa kukusanya Kodi, Godfred Mbanyi amewataka wataalam wa Ununuzi na Ugavi kujisajili kwenye PSPTB .
Yeyote atakae puuza maagizo haya hatuwa Kali za kisheria zitatumika Ikiwemo kutozwa faini milioni mbili na kwenda jera miakamiwili.
Mkurugenzi wa PSPTB amesema wameamuwa kuja na kampeni kwenye vyombo vya habari lengo Kutoa elimu Kwa Jamii umuhimu wa kuwaajili maafisa Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na PSPTB.
Habari na Ally Thabiti
Sunday, 1 May 2022
COSOTA YAGUSWA NA WATU WENYE ULEMAVU
Mkurenzi mtendaji wa COSOTA, DORIS SINALE amesema kupitia mkataba wa MARA CASH utasaidia kiasi kikubwa watu wenye ulemavu kuweza kupata haki ya kuchapisha vitabu mbalimbali na majalida kupitia maandishi ya Nukta nundu kwaaajili wasioona lengo la COSOTA ni kuyafikia makundi yote.
Habari picha na Ally Thabit
WILAYA YA MKURANGA YAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA.
KHADIJA NASRI ALI Mkuu wa Wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani amesema katika mbio za mwenge ambako wilaya ya mkuranga itatembekewa na mwenge tarehe 03/05/2022 ambapo jumla ya miradi saba itazinduliwa na mingine itawekewa mawe ya msingi thamani ya miradi hii ni kiasi cha Bilioni saba nukta sita (7.6) Bi. Khadija Nasri Ali amesema wanapongeza juhudi na jitihada za utendaji kazi za Raisi Samia Suruh Hassan ndio maana wilaya yake ya mkuranga itakeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo ya Rais Samia Suruh Hassan ikiwemo uzinduzi wa msitu wa vikindu ambao watalii zaidi ya mia tano (500) hutembelea kila mwezi na ujenzi wa miundo mbinu sehemu za kihistoria. Bi Khadija Nasri Ali ametoa wito kwa watu wote kumuombea Rais Samia Suruh Hassan na kumuunga mkono kwa moyo na vitendo pia ametoa rai kwa wanamkuranga na watanzania kwa ujumla kulinda na kudumisha amani iliyopo nchini Tanzania.







