Friday, 25 November 2022

MRATIBU WA MRADI WA MAISHA BORA ATOA NENO

 Mratibu Agness Sameja amewataka wazazi na walezi nchini Tanzania kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu pia ametoa wito kwa watoto wenye ulemavu waliopo mashuleni kusoma kwa bidii na watoe taarifa pindi wanapotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Amesema haya wakati wa kukabidhi pea 30 za uniform kwa wanafunzi wasio ona shule ya msingi Toangoma kupitia mradi wa Maisha Bora chini ya kanisa la FCPT.


Habari picha na Ally Thabit

MCHUNGAJI WA FCPT AHAIDI MAZITO

 Mchungaji wa kanisa la FCPT lililopo Toangoma Henry Katamba amesema mradi wao wa maisha bora ambao unatekelezwa kwenye mikoa saba Tanzania utaendelea kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu amesema haya wakati wa kukabidhi Pair 30 za uniform kwa wanafunzi wasioona shule ya msingi Toangoma Dar es  Salaam.



Habari Picha na Ally Thabit

WIZARA YA MARIASILI NA UTALII WAJA KUZIBITI WA UOTO WA ASILI




 




Habari picha na Ally Thabith

Monday, 21 November 2022

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KIGAMBONI AMPONGEZA SAMIA

 SIKU NJEMA YAHAYA SHABANI mwenyekiti wa ccm wilaya ya kigamboni amesema rais Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa kwenye nchi ya Tanzania pia ameweza kufungua miradi mikubwa wilaya ya kigamboni nakutoa fedha nyingi katika wilaya hii.


habari kamili 

Ally Thabith

AZAM TV YAFUNGUA DUKA JIPYA KARIAKOO


 

HABARI PICHA NA ALLY THABITH

Sunday, 20 November 2022

MBUNGE WA SEGEREA KUIBUWA VIPAJI

 Mbunge Bona wa jimbo la segerea ameamua kuja na michuano wa mpira wa miguu ambako tarehe 03 December uzinduzi unafanyika jumla ya timu 64 zitashirki ambako mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni tano. mshindi wa pili milioni tatu amesema lengo hili la michuano hii nikuibua na kukuza vipaji vya vijana ili waweze kuajiliwa huku akijipanga kuanzisha michuano ya watu wenye ulemavu.

Habari na Ally Thabith

WAZIRI NAPE AIPONGEZA TBC

NAPE MOSES NAUYE waziri wa habari technologia na habari amelipongeza shirika la habari nchini Tanzania TBC kwa kupata haki za kuonesha michuano ya kombe la dunia inayofanyika nchini Qatar nae kwa upande wake msemaje mkuu wa serikali Gereson Msigwa amevitaka vyombo vya habari nchini Tanzania kutoa habari zenye uweredi kama TBC ambako ameahidi kutoa ushirikiano kwenye kuonesha na kutangaza michuano ya Kombe la michuano nchini Qatari uku mwenyekiti wa bodi ya TBC anaitwa STEVEN KAGAIGAI amewataka watu kujitokeza kwa wingi kutangaza nakuonyesha bidhaa zao kupitia TBC pia Mkurugenzi mkuu wa TBC Dr. Ayubu Ryoba amesema TBC itaonesha mechi 28 kwenye kombe la Dunia kwa lugha ya kiswahili na kwa muonekano wa HD na upande wa radio TBC itatangaza mechi 24.

Meneja masoko wa TBC ametoa wito kwa makampuni viwanda kuweza kutangaza na TBC kwenye kombe la dunia.

Habari 

Ally Thabith