Hali ya Taharuki imewakumba wakazi wa kata za Lukobe,Kihonda na Mkundi Manispaa ya Morogoro baada ya mvua Kubwa kunyesha usiku wa kuamkia Leo na kusababisha mafuriko katika maeneo hayo.
habari kamili
Hali ya Taharuki imewakumba wakazi wa kata za Lukobe,Kihonda na Mkundi Manispaa ya Morogoro baada ya mvua Kubwa kunyesha usiku wa kuamkia Leo na kusababisha mafuriko katika maeneo hayo.
Ni January 13, 2023 ambapo Bondia Kareem Mandonga amezungumza kuhusu pambano lake dhidi ya mpinzani wake Daniel Wanyonyi huko nchini Kenya linalotarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa KICC nchini Kenya.
Kupitia ukurasa wake mtandao wa kijamii wa Instagram, Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), wametangaza nauli mpya za mabasi ya mwendo wa haraka zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia Jumatatu, Januari 16, 2023 huku nauli kwa Wanafunzi zikibaki kama zilivyo.
Katika ukurasa huo, DART imeandika kuwa, “Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), unapenda kuwaarifu watumiaji wa mabasi yaendayo haraka kuwa kuanzia Jumatatu, Januari 16, 2023 nauli mpya zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) zitaanza kutumika.”
Taarifa hiyo imeonyesha kuwa nauli katika njia kuu ya Kimara-Kivukoni, Kimara-Gerezani na Kimara-Morocco itakuwa Shilingi 750 wakati Kimara-Mbezi nauli itakuwa Shilingi 500 na njia ya Kimara – Kibaha na Kimara-Mlongazila itakuwa Shilingi 700, huku Gerezani –Muhimbili ikiwa Shilingi 750.
Mkuu wa wilaya ya ilala yaikabidhi vishikwambi kwa walimu wa mkoa wa Dar es salaam 3782 lengo walimu watumie katika kufundishia nae afisa takwimu wa elimu mkoa wa Dar es Salaam Asha Mapunda amemshukuru Rais Dr. Suuhu Hassani kwakutoa vishikwambi kwa walimu pia amesema wanafunzi wenye ulemavu watafundishwa bila shida amesema haya kwenye shule ya msingi ya Diamond Dar es Salaam wakati akikabidhiwa vishikwambi.
Habari picha na Ally Thabit
Takriban watu wanne wamefariki Dunia, baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha magari mawili aina ya Toyota Spacio na Lori kugongana uso kwa uso katika eneo la Kwambe Wilayani Kilosa lililopo Barabara kuu Morogoro – Dodoma.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mukama amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari dogo kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.
Habari picha na Ally Thabit
Wajumbe saba kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wametangazwa hii leo baada ya kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ameteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, akichukua nafasi ya Shaka Hamdu Shaka.
Katika Kikao hicho kilichofanyika hii leo Januari 14, 2023 na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati kuu ya CCM iliketi na vikao vyote vilihitimishwa chini ya mwenyekiti wake kwa kutangaza safu mpya za wajumbe wa NEC na kuidhinisha sekretarieti.
habari picha na Ally Thabith
Angelina Mabula waziri wa ardhi nyumba na makazi amezifungia kampuni saba na zingine kumi na tano za upimaji ardhi kushindwa kutekelezwa mikataba.
Habari kamili na Ally Thabith