Monday, 22 May 2023

DIWANI BUSORO PAZI ANDAA MASHINDANO YA QUR AN

 Busoro Pazi diwani wa kata ya buguruni amesema lengo la kuandaa mashindano ya Qur An watu wamjue Mwenyezi Mungu.

Habari kamili na Ally Thabith

Tuesday, 9 May 2023

Kiongozi wa zamani wa Pakistan Imran Khan akamatwa

 

Maafisa wa usalama wa Pakistani walimkamata Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan siku ya Jumanne alipokuwa akifikishwa mahakamani katika mji mkuu, Islamabad, kujibu mashtaka ya kesi nyingi za ufisadi, maafisa wa chama chake walisema.

Khan alitolewa nje na kuwekwa ndani ya gari la polisi na maajenti kutoka taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo, Ofisi ya Kitaifa ya Uwajibikaji, kulingana na Fawad Chaudhry, afisa mkuu wa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf.

Televisheni huru ya GEO ya Pakistan ilitangaza picha za Khan mwenye umri wa miaka 72 akivutwa na vikosi vya usalama kuelekea kwenye gari la kivita, ambalo lilimchukua.

Khan aliangushwa kwa kura ya kutokuwa na imani naye Aprili 2022. Amedai kuondolewa kwake kulikuwa kinyume cha sheria na njama ya Magharibi na amefanya kampeni dhidi ya serikali ya mrithi wake, Waziri Mkuu Shahbaz Sharif, akitaka uchaguzi wa mapema.


Chama cha Khan kililalamika mara moja kwa Mahakama Kuu ya Islamabad, ambayo iliomba ripoti ya polisi kuelezea mashtaka ya kukamatwa kwa Khan.

Maafisa wa shirika la kupambana na ufisadi walisema kuwa Ofisi ya Kitaifa ya Uwajibikaji ya Pakistan ilitoa hati za kukamatwa kwa Khan wiki iliyopita katika kesi tofauti ya ufisadi, ambayo hakupata dhamana  jambo ambalo litamlinda dhidi ya kukamatwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Maafisa hao, ambao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina, walisema Khan atafikishwa mbele ya mahakama ya kupinga ufisadi baadaye Jumanne.

Hakukuwa na taarifa nyingine rasmi kutoka kwa serikali kuhusu kukamatwa kwa Khan.


Habari Picha na Ally Thabiti

Expedia Group Kushirikiana Na Tanzania Kutangaza Utalii


 

Seattle, Marekani

Kampuni kubwa ya biashara ya utalii duniani kupitia mtandao, Expedia Group, imeahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Bodi ya Utalii (TTB), kutangaza na kuleta watalii wengi zaidi nchini Tanzania.

Kauli hiyo inayounga mkono pia juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuitangaza Tanzania kimataifa, imetolewa jana Mei 8, 2023, na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masoko ya Kimataifa wa kampuni hiyo, Bw. Andrew Van Der Feltz, alipokutana na kufanya mazungumzo kwenye makao makuu yao mjini Seattle na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi.

Expedia ni kampuni inayotumia teknolojia za kisasa kutangaza na kuhudumia watu zaidi ya milioni 400 kwa mwezi duniani na ikiwa inatumia muunganiko wa zaidi ya tovuti 200 na ikifanya kazi na mashirika ya ndege na wabia wengine zaidi ya 509 ikishika nafasi ya pili duniani na wakati fulani namba moja Marekani kwa kuaminiwa na watalii katika sekta ya usafiri na utalii.

Awali, ujumbe wa Tanzania pia ulipata wasaa wa kusalimiana na Rais wa Expedia Group anayeshughulikia Biashara ya Kimataifa, Bi. Ariane Gorin, ambaye aliueleza ujumbe huo kuwa Tanzania ambako alipata kutembelea mwaka 2016 Tarangire, Serengeti na Ngorongoro Kreta kuwa ni nchi yenye vivutio vya kipekee na anatarajia kuitembelea tena.

Kwa upande wake Dkt. Abbasi aliyeambatana na Mtendaji Mkuu wa TTB, Damasi Mfugale, aliwahakikishia watendaji hao wa Expedia kuwa Tanzania kwa sasa imeamua kuja na mtazamo mpya katika kutangaza utalii.

“Tunaamini utaalamu wenu na uzoefu wenu katika masoko na biashara ya utalii kimtandao utasaidia kuongezea juhudi za Rais wetu wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya juhudi kubwa kupitia filamu ya “Tanzania; The Royal Tour” kuiweka Tanzania katikataswira pana zaidi kimataifa katika utalii na uwekezaji,” alisema Dkt. Abbasi. 

UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO MKOANI MANYARA


 Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Manyara  watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Manyara. Upimaji huo utaenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani yatakayofanyika  tarehe 17/05/2023.

Upimaji huo utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 15/05/2023  hadi tarehe 19/05/2023  saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Manyara.

 

Kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

 

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.


Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayebainika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0768408984 Vailine Osward na 0714956529 Abubakar Mjaka.


        • “Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.


Habari Picha na Ally Thabiti

 


WADAU WAKUTANA NA KUWEKA MIKAKATI YA KUENDELEZA KILIMO BIASHARA

 


SEKTA ya kilimo bado inazo fursa mbalimbali ambazo zikitumika ipasavyo zitawezesha uchumi wa nchi kukua sambamba na kuzalisha ajira nyingi kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, wakati akifungua kongamano kuwajengea uwezo wakulima kuhusu kilimo biashara lililoandaliwa na ubalozi wa Uholanzi nchini na kufanyika mjini Dodoma, likiwa linawashirikisha wakulima na wadau mbalimbali katika sekta hiyo.

Kwa upande wake,Balozi wa Uholanzi nchini,Mh. Wiebe De Boer, alisema Serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania hasa katika sekta hiyo ili izidi kukua na kuongeza uchumi.


Balozi wa Uholanzi nchini, Mh.Wiebe De Boer, akibadilishana mawazo na Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe ,muda mfupi kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.

Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe. akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa wa Uholanzi nchini,Mh.Wiebe De Boer baada ya kufungua kongamano la kuendeleza kilimo biashara nchini.

Habari Picha na Ally Thabiti

Kanisa Lahukumiwa Kulipa Milioni 70 Kwa Kosa La Gari Kugonga Na Kusababisha Kifo

 


Njombe

MAHAKAMA ya hakimu Mkazi Njombe imelihukumu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini kulipa fidia ya shilingi Milioni 70 baada ya gari mali ya kanisa hilo kugonga na kusababisha kifo cha marehemu Kaselida Mlowe wa mjini Njombe.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Njombe Lihad Chamshama amesema mdaiwa namba mbili ambaye ni kanisa anahukumumiwa kulipa fidia ya milioni 70 kutokana na uzembe uliofanywa na mdaiwa namba moja bwana Rajab Kitwana ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo wakati ikitoka mjini Makambako kwenye matengenezo na kusababisha kifo cha Marehemu Kaselida.

Aidha Mahakama hiyo imetoa jukumu kwa kanisa kulipa ghalama zote za uendeshaji wa kesi iliyoendeshwa kwa zaidi ya miaka miwili mpaka sasa huku ikitoa haki ya kukata rufaa kwa kanisa dhidi ya hukumu hiyo.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama kutokana na kesi No 2 ya mwaka 2022 ya madai ya fidia ya Milioni 100 dhidi ya kanisa la KKKT iliyofunguliwa na Siglada Mligo msimamizi ambaye ni msimamizi wa mirathi wa marehemu Kaselida Mlowe baada ya kifo kilichotokana na ajali ambapo marehemu aliacha wategemezi wakiwemo watoto wake watatu.

Kesi ilifunguliwa baada ya msimamizi wa mirathi kushinda kesi No 6,2021 ya makosa ya usalama barabarani kutokana na ajali iliyotokea eneo la Kibena Mlima wa Ichunilo mjini Njombe hapo September 25,2020 baina ya Hiace Namba T 298 DNE na gari NO T 210 - AHU Mercedes Benz Track mali ya kanisa na kupelekea kifo cha Kaseleida Mlowe.

Kesi hiyo imeendeshwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe Lihad Chamshama huku upande wa madai ukiwakilishwa na mawakili watatu akiwemo Emmanuel Chengula,Frank Ngafumika na Gervas Semgabo huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Marco Kisakali.

Habari na Ally Thabiti

DAWASA AWATAKA WATEJA WAAO KULIPA BILLS

 Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa Dawasa Kiula Kingu amewataka wateja wa Dawasa kulipa bills kwa wakati na kulinda miundo mbinu ya maji.

Habari na Ally Thabiti