Wednesday, 10 January 2024

MKURUGENZI MKUU WA BANDARI AINISHA MIKAKATI MIZITO

 




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mr. Plasduce M. Mbossa amesema wameanza kazi za kutanua Bandari ya Dar es Salaam kwa kujenga Magati kuanzia namba 12 hadi 15 magati haya yanauwezo wa kupakia Meri kubwa pia watajenga vituo viwili vya mafuta pamoja na kujenga Mapipa ya kupakulia mafuta Mr. Plasduce M. Mbossa amesema eneo la kulasini EPZA itakuwa bandari kavu kwa ajili ya kuweka Contena kwa wingi, pia kutakuwa na maboya ya kuongozea Meri uku wakiongeza kina kwenye magati.

Huku ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo unaanza hivi karibu ambako wataanza kujenga magati mawili ambako gati moja gharama yake Bilioni Moja Mia Tatu Siti kila gati litakuwa na ulefu wa Mt 500 ambako gati moja linauwezo wa kupokea meri moja yenye uwezo wa kubeba Makontena elfu 25 bandari hii ya Bagamoyo inatarajiwa kujengwa gati 9 huku kina cha Bandari ya Bagamoyo kwenda chini Mita 18.

Mr. Plasduce M. Mbossa amesema lengo la kupanua hizi Bandari ni kuweza kupokea meri kubwa, kuwavutia wawekezaji kwa wingi, kuondoa mlundikano wa mizigo bandarini na kuiwezesha serikali kupata kodi kwa wingi na kupatikana kwa ajira kwa Watanzania na kuwepo kwa usalama kwa kiwango kikubwa,

Mr. Plasduce M. Mbossa amewataka wanahabari pamoja na walili wa vyombo vya habari waendelee kushilikiana na TPA kwa ajili ya Maslahi mapana ya Taifa na waache kuandika habari za upotoshaji kwa jamii.

Habari Picha na Ally Thabiti


WAWEKEZAJI 58 KUTOKA NJE YA NCHI WAONYESHA NIA KUWEKEZA KATIKA KONGANI YA KAMAKA ILIYOPO MKOANI PWANI- KABENGULA


Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.

WAWEKEZAJI 58 kutoka nje ya nchi wameonyesha nia ya kuwekeza katika kongani ya kisasa ya Modern Industrial Park -KAMAKA co.ltd iliyopo Disunyara, Mlandizi Kibaha mkoani Pwani .



Licha ya nia hiyo ya wawekezaji ,Kongani hiyo inaiomba Serikali kutupia macho changamoto ya barabara kwa kiwango cha lami kutokea Mlandizi ,huduma ya maji na umeme wa uhakika ili kuendelea kuvutia wawekezaji ndani na nje ya nchi ambao wakwenda kuomba kuweka ndani ya Kongani hiyo.

Hayo aliyaeleza Afisa Fedha na Masoko wa Turnkey Real Estate Tumaini Kabengula, kampuni ambayo inahusika na mauzo na masoko,na kuingia mkataba wa kutafuta wawekezaji kuwekeza viwanda kwenye viwanja 202 vilivyoko ndani ya Kongani ,kwa Waziri wa Viwanda ambae alifika kwenye eneo hilo kujionea changamoto zinazowakabili.

Alieleza, hadi sasa wawekezaji 58 wametembelea kongani na kuonyesha nia ya kuwekeza wakitokea nchi ya India, China ,Uturuki,Sudan ya Kusini ,Afrika ya Kusini ,Rwanda ,Somalia ,Tanzania , Pakistan,Yemen ,Zambia ,Falme za kiarabu ,Misri,Uganda ,Kenya na Canada.

"Mikataba iliyopo ni kumi ya ununuzi wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, pamoja na viwanja 24 vilivyoshikiliwa vikisubiri kusainiwa kwa mikataba."

Kabengula alieleza, wawekezaji watatu wamekwishaanza hatua za awali za ujenzi za ujenzi zinazohusisha michakato ya vibali vya mazingira (EIA) na michoro kwa ajili ya ujenzi na wanatarajia wengine watano waliosaini mikataba wataanza hatua za ujenzi mwaka huu.

Afisa huyo alifafanua kuwa, wawekezaji wengi ambao wameshaingia mikataba ya ununuzi wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda wangependa watakapoanza ujenzi changamoto hasa ya maji na umeme iwe imetatuliwa.

Hata hivyo ,alieleza miundombinu rafiki na wezeshi ndio kiungo pekee cha kuvutia wawekezaji zaidi.

"Tunaiomba Serikali kutatua hasa changamoto ya maji na umeme "alisisitiza Kabengula.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni utoaji wa vivutio vya kodi kwa kongani jirani na kutokuwepo vivutio hivyo katika kongani ya modern industrial park licha ya uwekezaji mkubwa uliofanyika na unaoendelea kufanyika kuna haribu ushindani wa haki wa kibiashara.

"Baadhi ya wawekezaji wanaamua kutokuchukua viwanja ndani ya Kongani kwa sababu ya kukosekana kwa vivutio vya kikodi kama ambavyo vinapatikana katika kongani jirani."

Kabengula alieleza, wawekezaji wengi wanakiri kuvutiwa na uzuri wa kongani ya modern industrial park lakini wanakwazwa na kutokuwepo kwa vivutio hivyo vya kikodi kama ambavyo vinapatikana kwenye kongani jirani.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alieleza ,kuhusu Changamoto ya maji alishaongea na waziri wa maji Jumaa Aweso na ameahidi kufika kwenye kongani hiyo kujionea uhalisia wa tatizo.

"Tunajivunia kuifungua Mkoa wa Pwani kwa ujenzi wa viwanda ,tuna kongani tatu na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Kongani 23 ,ambapo tunaishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuvutia wawekezaji na kuboresha na kuweka mazingira wezeshi hatua kwa hatua ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili "alieleza Kunenge.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji alieleza miundombinu wezeshi ni suala muhimu kwenye uwekezaji.

Kuhusu masuala ya kikodi alisema, watafuatilia ili kuona namna ya kuliweka sawa tatizo hilo.

"Ninashauri upande huo wa masoko ,waongeze taarifa ambazo hazipo kwenye taarifa ya mradi,wekeni wazi kila kitu hatua itakayosaidia ili ziwafikie wawekezaji kwa urahisi"alieleza Kijaji.

Nae Mkurugenzi Mtendaji, Mkandarasi Mkuu Afriq Engineering and Construction Co.Ltd mhandisi Charles Bilinga , alisema wamefikia asilimia 93 katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa miundombinu ambao utakamilika mwezi Februari mwaka huu .

Kongani ya KAMAKA ni mradi ambao ukikamilika utagharimu trilioni 3.5 kati ya fedha hizo bilioni 122.4 zitajenga miundombinu ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo hadi sasa sh .bilioni 35 zimetumika kwa ujenzi wa miundombinu na gharama zinazohusiana na uwekezaji huo.

CMSA YATINGA ZANZIBAR KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI

 


MWANDISHI WETU.


KATIKA kuadhimisha Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya dhamana (CMSA) imetinga visiwani humo kutoa elimu juu ya masuala ya Uwekezaji katika Masoko ya mitaji.

Maonyesho hayo ya 10 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar ambayo yanafanyika Dimani Fumba visiwani humo yameanza rasmi Januari 7, mwaka huu ambapo
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ally Mwinyi, atakuwa mgeni rasmi.

Akizungumza na wanahabari, Afisa uhusiano na elimu kwa umma, Stella Anastazi amesema, lengo kuu la kuja katika maonyesho hayo ni kutoa elimu juu ya masoko ya mitaji.

Stella amesema amefurahi kuona muitikio mzuri na mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali waliotembelea banda la CMSA ili kujifunza.

 
"Nia na madhumuni ni kuleta elimu hii kwa wananchi wa Zanzibar, na pia kuwajuza maendeleo makubwa ambayo mamlaka imekuwa nayo mpaka sasa,"
Amesema imekuwa fursa kubwa kukutana na watu ambao wanaelimu juu ya mitaji hivyo hata kuwapa madini ya uwekezaji imekuwa rahisi tofauti na kukutana na mtu asiye na elimu ya masoko hayo.


Aidha Stella amesema ni wakati muafaka kwa wawekezaji kuwekeza kwani wao wanatoa ushauri zaidi na kujibu sintofahamu ambazo wananchi wamekuwa wakizipitia katika uwekezaji.


"Tumekuja na vipeperushi vingi vitazidi kumpa elimu muhusika ili kujua mambo mengi yanayohusu mitaji na masoko kupitia hivi vipeperushi pia vinampa mwongozo wa namna gani ya kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja na mambo mengi yanayofanyika CMSA,"amesema.

Aidha amewataka Watanzania kuwekeza ili kupata ongezeko la thamani ambayo ni faida kubwa sana kwao.

"Tuna kipeperushi kinacho toa elimu ya kujiepusha na uwekezaji wa upatu haramu ambao sio mzuri kwao maana akikosea anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria maana kuvunja sheria ya nchi ni kosa la jinai kufanya kosa hilo"amesema Stella.

Mmoja wa wananchi kisiwani Zanzibar Hamis Shaibu Hamad,amesema alikuwa akisikia mamlaka ya masoko ya mitaji lakini hakufahamu ni vitu gani vizuri vinapatikana huko ila baada ya kutembelea banda amefarijika kufahamu mengi.

"Unajua ukiwa haujapata elimu ya kitu husika unaweza kujikosesha fursa lakini mimi nimepata vitu vizuri kabisa kutika katika hili banda la CMSA nitakuwa balozi mzuri kwa wenzangu huko ili na wao waweze kuwekeza zaidi,"alisema Hamad.

Afisa uhusiano na elimu kwa umma kutoka CMSA, Stella Anastazi,akitoa elimu ya uwekezaji kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya biashara Zanzibar ( Zanzibar International Trade Fair)


Monday, 8 January 2024

MKURUGENZI MKUU MTENDAJI WA TRC AELEZA SGR ILIVYOKUWA NI RAFIKI KWA WENYE ULEMAVU


Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema mradi wa wa Treni ya Umeme (SGR) umezingatia maitaji ya msingi kwa watu wenye Ulemavu mfano kwa wasiona kuna alama maalumu kwa wenyeulemavu wa viungo miundo mbinu yao pia ni rafiki hivyo amewatoa hofu watu wenye ulemavu na wasiokuwa na ulemavu kwa usalama ni mkubwa katika mradi huu ukikamilika ametoa wito kwa jamii kuendelee kumuunga mkono Mh. Rais Samia Suluhu Hassani pia kumuombea kwa Mungu aendelee kuwa na hekma na afya tele huku Masanja Kadogosa akimpongeza Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuutekeleza mradi huu wa SGR.

Habri Picha na Ally Thabiti
 

WAZIRI WA UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI AWAFUNGULIA MILANGO WAJAPANI KUJA KUWEKEZA TANZANIA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mnyaa Mbarawa amewataka wajapani kuja kuwekeza Tanzania kwani Miundombinu ni rafiki kwa upande wa Bandari Barabara na Reli ambako kwa sasa mradi wa Treini ya Umeme umefikia Hatua Mzuri hivyo amewataka wajapani wajitokeze kwa wingi kuwekeza nae kwa upande wake waziri wa maliasili wa Japan amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani namna alivyotengeneza mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji.

Habari na Ally Thabiti

MKUU WA WILAYA WA DODOMA MJINI ATEKELEZA KWA VITENDO MAAGIZO YA RAIS SAMIA

Mh. Jabiri Shekimweri  Mkuu wa wilaya Dodoma Mjini amesema wanaendeleza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato, ujenzi wa Barabara za Tarula, Miradi ya Maji Madarasa na Barabara za Mzunguko Mh. Jabiri Shekimweri amesema pia wamejenga jengo la Machinga Complex ambako wamewezesha vijana kujiajili na kuwajili watu wengine, pia wanatoa pesa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ametoa wito kwa jamii waendelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani.

Habari na Ally Thabiti

Monday, 1 January 2024

HOSPITAL YA MKOA WA DODOMA YAMPONGEZA RAISI SAMIA

 Mganga mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Dodoma Dk. Ibezi Ernest amempongeza Raisi Dr. Samia Suluhu Hassani kwa kuweza kutengeneza miundombinu ya hospital ya mkoa wa Dodoma na kuweka vitanda vitatu na vitanda 28 vya wagonjwa mahututi nakufunga mtambo mkubwa wa kuzalisha gesi mitungi 300 kwa siku moja na kuweka vitanda 300 vya wagonjwa wanaotumia gesi pia Rais Samia aweza kununua mashine ya city scan ambayo inauwezo wa kuhudumia wagonjwa 3018 na kuweza kutengeneza maabara na kununua vitenganishi 86 na kununua gari la usimamizi moja pia kuna mpango wa m-mama lengo la mpango wa M-MAMA nikuweza kuwasaidia mama wajawazito pindi wanapoitahi kwenda kujifunngua magari yanawafuata walipo, Pia Rais Samia ameoa Ambulance Tatu kwaajili ya wagonjwa.

Dr. Ibenzi amesema hospital mkoa wa Dodoma inawahudumia watu wenye ulemavu pamoja na wazee bure pia inawataalamu wa lugha za alama kwenye watu wenye uziwi.

Ametoa wito kwa jamii wamuunge mkono Dr. Samia Suluhu Hassani















Habari picha na Ally Thabith