Thursday, 21 October 2021

MWENYEKITI WA NCCR MAGEUZI ATANGAZA VITA


 James Mbatia Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi amewataka Viongozi wa Serikali ya Tanzania,wanasiasa, Viongozi wa Kidini, Viongozi wa kimira na kijadi na watu wote wawapige Vita na wawapige watu wote wanaoalibu UTU wa Watu. 

kwani kutowapiga Vita watasababisha kuvunjika Kwa Amani na utulivu wa nchi yetu ya Tanzania .

Habari picha na Victoria Stanslaus

MENEJA WA TANROAD AHAIDI MAZITO


 Japhet Kivuyo Meneja wa TANROAD wa Mizani amesema Kwa sasa wanafanya makongamano na semina mbalimbali Kwa wadau mbalimbali wa Usafirishaji namna ya kutumia Mizani ambako wameanza elimu Kwa Mkoa wa Dsm na Pwani na wamefurahishwa na mwitikio mkubwa wa wadau wa Usafirishaji na jinsi walivyopokea Mafunzo haya.

Mikoa mingine watakayoenda Lindi ,Mtwara,Dodoma,Singida ,Morogoro,Tanga Iringa,Mbeya Ruvuma,Katavi,Geita,Mwanza,Arusha na Mikoa mingine. Lengo la semina hizi ni kuwaongezea uwelewa na ufahamu  na umuhimu wa kuzingatia Sheria,kanuni na Taratibu za Mizani.

Ametoa wito Kwa wadau wa Usafirishaji wazingatie Uzito unaotakiwa kwenye magari Yao kwaajili ya kutunza na kulinda barabara na madaraja hili yaweze kudumu Kwa muda mrefu.

Kwani wakizingatia haya tutapunguza gharama za ujenzi wa barabara na madaraja ambako Fedha hizi zitasaidia katika kutatuwa Changamoto ya Afya, Elimu,maji na maeneo mengineyo.

Japhet Kivuyo Meneja wa TANROAD amesema haya wakati wa semina na wadau wa Usafirishaji jijini Dsm.

Habari picha  Victoria Stanslaus

TANROAD YAJIVUNIA


 Mkurugenzi wa Matengenezo ya Mizani TANROAD amesema mpaka sasa wameweza kuiboresha na kuimarisha Mizani ya kupinga Nagari .amewataka wadau wa Usafirishaji wazingatie sheria ,kanuni na Taratibu za Mizani .

Lengo la TANROAD kuweka Mizani ya kupinga magari hili kudhibiti Uzito uliopitiliza ,ambako kutaepusha uhalibifu wa barabara na madaraja.

Amesema moja ya jitihada anazofanya kutoa elimu na kufanya semina mbalimbali Kwa wadau wa Usafirishaji.

Habari picha Ally Thabit

MCHUNGAJI ATAKA WATU KUZINGATIA UTU


 Mchungaji Masanja anawataka Watu Wote Kuzingatia UTU kwani Ndio msingi wa Amani pia amekipongeza Chama cha NCCR Mageuzi Kwa kuzinduwa Kampuni ya UTU .

Ivyo amevitaka Vyama vingine kuunga mkono .

Habari picha na Victoria Stanslaus

ZANZIBAR YAIPA TANO TAFFA


 Kiongozi wa ZAFFA Othumani Musa amempongeza raisi wa TAFFA Edwardi Urio Kwa kazi nzuri anayoifanya za kutatuwa Changamoto za wanachama wake na kuwaunganisha ZAFFA na TAFFA kuwa kitu kimoja.

Habari picha na Ally Thabiti

NIC YAFUNGUWA MILANGO


 Kafiti Kafiti , Principal Business Development Officer anawataka watu kuchangamkia huduma ya bima inayotolewa na NIC kwani bei zao ni nafuu .

NIC ina bima mbalimbali ambako mtu yeyote akijiunga atojutia na bima zao ni nafuu ukilinganisha na Kampuni zingine za bima na NIC Awana ubabaishaji kwenye malipo Kwa wateja wao.

Pia NIC wanawaakikishia wanachama wa TAFFA watapata hudhuma Bora .

Habari picha na Victoria Stanslaus

TAFFA YAJA KIVINGINE


 Mwenyekiti wa TAFFA  Edwardi Urio amewataka wanachama wake kujitaidi kutoa michango na amewaaidi kuwa watapata KAZI nyingi, pia amewataka  wanachama wa TAFFA wafanye KAZI Kwa Uweredi.

Habari picha na Victoria Stanslaus