Thursday, 31 March 2022

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII YAMPONGEZA RAISI SAMIA SULUHU HASSAN


Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia watoto na makundi maalum Dr. Doris Ngwajima amesema kipindi cha uongozi wa Raisi Samia Suluh Hassan kwa Mwaka Mmoja ameweza kuanzisha wizara ya maendeleo ya jamii ambako imeweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kutatua changamoto zilizo kuwa zinawakabili watoto waishio mitaani, wanawake na watoto pia pamoja na makundi maalum yameweza kufikiwa kwa kiasi kikubwa Waziri Doris Gwajima amewataka watu kumuunga mkono Rais Samia Suluh Hassan 




Nae katibu mkuu Dr. Zainabu Chaula amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kuyainua makundi mbalimbali hivyo ni vyema watu waendelee kumuunga mkono na kuwanao sambamba.

Habari picha na Ally Thabith

KAMPUNI YA PUMA YA MAFUTA YATOA ZAWADI

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Puma Energy Dr. Suleiman Madige lengo la kutoa zawadi nikuongeza ufanisi kwa Ma_meneja na wadau wa kampuni ya Puma. Ameutaka uongozi wa kampuni hii ifikapo mwaka 2025 Puma iwe na vituo vitavyo 150 ambavyo kwasasa vipo vituo 80 

Naye kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Puma amemuhakikishia mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya PUMA kuwa ifikapo mwaka 2025 watahakikisha watajenga vituo zaidi ya 150 pia mkurugenzi amepongeza serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan namna inavyoweka nguvu kwenye kampuni ya PUMA. Kwa upande wake VANESA meneja wa kampuni ya PUMA energy ametoa wito wa watu wote waendelee kutumia bidhaa ya kampuni ya PUMA pia kampuni ya PUMA inakuja na bidhaa ya gesi ambako gesi hiyo itapatikana kwenye vitu vyote vya PUMA, VANESSA amewaahidi watu waishio vijijini watajengewa vituo vya PUMA.

Habari  na Ally Thabith

 

Friday, 4 March 2022

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AWAFUNDA VIONGOZI WA DINI


 Hamadi Suleimani Chande  Naibu Waziri wa Fedha na Mpango amewataka viongozi WA dini Kutoa elimu Kwa jamii ,pia Watumie nafasi zao vizuri na waache kujikweza .

Habari picha na Ally Thabiti

WAZIRI APONGEZA KONGAMANO LA AFRICA MEDIA

 Waziri wa Ardhi Anjerina Mabura ameipongeza Kampuni ya Africa Media Group Kwa kufanya kongamano la Wanawake ambako umesaidia kutolewa Kwa madam mbalimbali za kuwawezesha Wanawake kuwainua kiuchumi na kutiwa moyo.

Habari na Ally Thabiti

TAASISI YA SAFINA YABAINISHA MIKAKATI


 Mkurugenzi wa Taasisi ya Safina amesema watashirikiana na serikali katika kuwajengea mazingira wezeshi watoto waishio mitaani Kwa kuwaweka pamoja na kuwapa ujuzi mbalimbali .

Mkurugenzi wa Safina amesema Taasisi yao wanawapokeana kuwapa Mafunzo watoto wa mitaani wenye Ulemavu wa Aina mbalimbali.

Habari picha na Ally Thabiti

SOS YAUNGA MKONO JUHUDI ZA DORITH NGWAJIMA


 Mkurugenzi wa SOS David amesema wanamuunga mkono juhudi na jitihada za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee,Watoto, Wanawake na Makundi Maalum katika kuwatengenezea mazingira wezeshi watoto waishio mitaani kwani vipaji vyao vitaonekana na wataweza kujikwamuwa kiuchumi.

Habari picha na Ally Thabiti

JAMES YUSTA AMEPATA TUMAINI KWA WAZIRI DORITH NGWAJIMA


 James Yusta amemshukuru na kumpongeza Waziri Dorith Ngwajima na viongozi wote wa wizarani Kwa kuja na Mpango Mkakati kwaajili ya kunusulu Maisha ya watoto waishio mitaani, pia James amemshukuru rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuguswa na kuwa na uluma na watoto waishio mitaani.

Habari picha na Ally Thabiti