Tuesday, 23 May 2023

BAJETI YA TRIL. 3.554 KUBORESHA MIUNDOMBINU NCHINI



Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha zaidi ya shilingi Trilioni 3.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege, reli, meli, vivuko, majengo ya Serikali na ununuzi wa ndege.

Fedha hizo zimeombwa ili kuimarisha huduma za usafiri na usafirishaji kote nchini na hivyo kuimarisha ukuaji wa uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Akiwasilisha mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema pamoja na mambo mengine fedha hizo zinatarajiwa kujenga miradi ya kihistoria yenye urefu wa kilometa 2,035 nchini ikiwemo barabara za Kidatu - Ifakara - Lupilo - Malinyi - Kilosa kwa Mpepo - Londo - Lumecha hadi Songea KM 435.

Miradi mingine ni barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago - Maswa hadi simiyu KM 339 na barabara ya Handeni – Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijochini – Dalai – Chambalo – Chemba – Kwa mtoro hadi Singida KM 460.

Aidha, Prof. Mbarawa amefafanua kuwa Serikali itaendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam – Mwanza KM 1,219 katika vipande vitano vya awamu ya kwanza ya ujenzi ili kuhakikisha vinakamilika kwa wakati na kwa thamani halisi ya fedha.

“Mheshimiwa Spika vipande hivyo ni Dar es Salaam – Morogoro KM 300, Morogoro – Makutupora KM 422, Mwanza – Isaka KM 341,  Makutupora – Tabora KM 368 na Tabora – Isaka KM 165 ambavyo ujenzi wake uko katika hatua mbalimbali za utekelezaji”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Serikali itaendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa SGR sehemu ya Tabora – Kigoma KM 506 ambapo mkataba wake umesainiwa na kwa sasa mkandarasi anakamilisha maandalizi ya ujenzi.

Awali akitaja vipaumbele vya Sekta ya Ujenzi Prof. Mbarawa amesema ni pamoja na kuanza ujenzi wa barabara ya Express way kutoka Kibaha-Chalinze-Morogoro yenye urefu wa KM 205 kwa mfumo wa PPP na  kuendeleza  ujenzi wa barabara kuu zenye urefu wa KM 350 ambapo kilometa 282 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na kilometa 68 ni miradi mipya.

“Wizara imepanga kufanya matengenezo ya kilometa 38,384.90 za barabara kuu na barabara za mikoa pamoja na matengenezo ya madaraja 3,129”, amesisitiza Prof. Mbarawa.  

Kuhusu vipaumbele vya Sekta ya Uchukuzi, Prof. Mbarawa ameeleza kuwa Serikali inakusudia kutekeleza miradi ya miundombinu ya reli ambapo ujenzi wa reli mpya ya SGR na ukarabati wa reli ya zamani ya MGR na TAZARA.

Waziri Mbarawa amesema katika kuimarisha bandari nchini Serikali imepanga kuboresha bandari zilizomo katika maziwa makuu ikiwemo bandari ya Bukoba, Kemondo bay, Mwanza South, Mwanza North, Kibirizi na Ujiji.

Serikali itaendelea na ununuzi wa mitambo ya kuongozea ndege na uendelezaji wa Chuo cha mafunzo ya usafiri wa anga ikiwa ni pamoja na mradi wa ununuzi wa rada mpya, na vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya hali ya hewa.

Kati ya zaidi ya shilingi Trilioni 3.5 zinazoombwa katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu takriban shilingi Trilioni 1.5 ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi na shilingi Trilioni 2.086 kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi.

Habari picha na Ally Thabiti

HANDRY SAMKY AIPONGEZA BANK YA NBC

Maneja program wa taasisi ya Mkapa Foundation aipongeza bank ya NBC kwa kuja na NBC Marathoni ambapo mbio hizi zitafanyika tarehe 23/07/2023 jijini  Dodoma ambako kiasi cha fedha kinachotarajiwa kukusanywa ni Millioni mia Tatu lengo kuweza kusaidi Hospitali ya Ocea Road kwa ajili ya wagonjwa wanaoumwa salatani ya shingo ya kizazi na fedha zingine itapewa taasisi ya Mkapa Foundation kwa ajili ya kuweza kuwafadhili kimasomo wakunga.

Hendry Samky amesema fedha hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa kunusuru vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua na wakunga watakuwa na taaluma pamoja na weredi kwenye kazi zao, kwani idadi ya akina mama kwenda kujifungua hospitali itaongezeka ambako mwaka 2016, 63% ya wanawake walikuwa wanajifungulia vituo vya afya na 85% wanajifungulia vituo vya afya na Hospitalini huku kukiwepo na huaba wa watumishi kwenye sekta ya afya kwa  52%  pia Hendry Samky amesema nivyema serikali kwa sasa kuweka wataaramu wa lugha za arama kwenye sekta ya afya pamoja na vyuoni. 

Kwa upande wake mkurugenzi wa benki ya NBC amesema taasisi ya Mkapa Foundation itapewa fedha itakayokusanywa na benki yao kwenye marathoni kwa ajili ya wakunga hapa nchini.

Habari picha na Ally Thabiti





Monday, 22 May 2023

Wadau walioalikwa katika uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma

 





RASI DKT. SAMIA ATEUA VIONGOZI NANE WAKIWEMO MABALOZI

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mabalozi kama ifuatavyo:


  1. Amemteua Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (JWTZ).


  1. Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).


  1. Amemteua Bw. Mohamed Awesu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Awesu alikuwa Konseli Mkuu, Konseli ya Tanzania, Jeddah Saudia Arabia.


  1. Amemteua Bw. Gelasius Byakanwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Byakanwa alikuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.


  1. Amemteua Dkt. Mohamed Juma Abdallah kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja. 


  1. Amemteua Bw. Hassan Mwamweta kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwamweta alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania, Uturuki.


  1. Amemteua Bw. Imani Salum Njalikai kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Njalikai alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu – Hotuba


  1. Amemteua Bw. Khamis Mussa Omar kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mussa alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.


Uteuzi huu wa Mabalozi umeanza tarehe 10 Mei, 2023 na wataapishwa kwa tarehe        itakayopangwa baadae. 


Zuhura Yunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

SILENT OCEAN WAFUNGUA OFISI INDIA KIBABE


Mohamed Kamilagwa Meneja Masoko wa Silent Ocean amesema wameamua kufungua Ofisi yao nchini India eneo la Mumbai lengo kuweza kuwasafirishia bidhaa zao wafanya biashara.

Mohamed Kamilagwa amewatoa hofu na Mashaka wafanyabiashara wote kuwa mizigo yao itasafirishwa kwa gharama nafuu na usalama wakutosha kwani kilio cha wafanyabiashara kilikuwa cha muda mrefu kwani walikuwa wanasafirisha mizigo yao miezi mitatu hadi sita. Hivyo Silent Ocean wameamua kufungua Ofisi India ambako Silent Ocean watasafrisha mizigo kuanzia siku 17 hadi 25.


Habari Kamili na Ally Thabiti

WHO KUWATHAMINI WAKUNGA

Meneja wa masuala ya MATENITE bwana Emmanuel amesema WHO inatahamini na kuwajali wakunga nchini Tanzania.

Habari kamili na Ally Thabith

TMDA KANDA YA ZIWA YAKAMATA VIFAA TIBA NA DAWA BANDIA

 Meneja wa kanda ya ziwa wa TMDA Sophia Mzilai amekamata madawa na vifaa tiba vilivyoingizwa kanda ya ziwa bila kufuata utaratibu na walivyovikamata wadai ni feki na badala yake wameviteteketeza na wahusika kupelekwa mahakaamani ambavyo vifaa tiba na hizo dawa thamani yake milioni therathini.

Habari kamili na Ally Thabiti