Thursday, 30 November 2023

AFRICAN CONTEXT OF WOMEN'S LAND RIGHTS

 


WIZARA YA ARDHI YAIPONGEZA LIBERTY SPARKS

 Naibu katibu mkuu wa wizara ya Ardhi, nyumba maendeleo na makazi Dr. Pendo Makokolo amesema Liberty Sparks utafiti walioufanya ni mzuri kwani serikali itatumia report hii walioizindua kwaajili ya kuboresha sera, sheria, kanuni na taratibu ambazo zinamnyima mwanamke haki ya kumiliki ardhi.

Dr. Pendo amepongeza kwa kusema kuwa watafanya maboresho na kwenye mabaraza ya ardhi lengo kuweza kuweka mifumo thabit ili mwanamke aondokane na manyanyaso na matesho anapodai haki ya kumiliki ardhi.

Habari kamili na Ally Thabit

MWENYEKITI WA BODI WA LIBERTY SPARKS

 Mwenyekit i wa Liberty Sparks ni vyema Serikali kuwapa elimu na uelewa wanawake waweze kumliki ardhi pia bunge litenge bajeti ya kutosha nakuweka mifumo rafiki kwenye mabaraza ya ardhi pamoja na mahakamaza. Yote haya yatafanyika migogoro ya Ardhi itapungua kwa kiasi kikubwa na wanawake watapa fursa yakuweza kumiliki ardhi

Mwenyekiti wa bodi wa taasisi ya LIBERTY SPAERK Dr Tumsifu amesema utafiti unaonesha kwenye ripoti yao asilimia 10% ya watanzania wanahati za Ardhi.

habari kamili na Ally Thabit

MKURUGENZI WA LIBERY SPARKS ATOA NENO JUU YA REPORT WALIOITOA

 Evans ni mkurugenzi wa Liberty Sparks amesema wamefanya utafiti na kugundua kuwa wanawake wanakosa haki ya kumiliki ardhi nchini Tanzania hii yote kutokana na mila na desturi dhidi ya wanawake pia sheria ya mwaka 1967 haimpi haki mwanamke kumiliki ardhi hivyo upitia utafiti yaiomba serikali kuweka mazingira wezeshi ili mwanamke kumiliki ardhi ambapo mwanamke huyu itamsaidia kwa kiasi kikubwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi ikiwemo kulima na shughuli zinginezo.

habari kamili na Victoria Stanslaus 

LIBERTY SPARKS YAJA NA RIPOTI YA UMILIKI WA ARDHI KWA WANAWAKE

 Dr. Samwel ni mshauri na mtafiti wa taasisi Liberty Sparks amesema wameamua kufanya utafiti kwa namna wanawake wanavyopata changamoto kwenye kumiliki Ardhi nchini Tanzania ambako kwa vijijini imekuwa ni tatizo kubwa sana ndio maana wameamua kufanya utafiti huu lengo serikali iweze kubadili sela, sheria, kanuni na taratibu kandamizi dhidi ya wanawake katika kumiliki ardhi.

Habari kamili na Ally Thabith

UGANDA YAIPONGEZA TEMINATE KWA MKUTANO WA ELIMU

 Mwakirishi kutoka Uganda John Samwel amesema mkutano ulioandaliwa na mtandao wa elimu nchini Tanzania utasaidia kwa kiasi kikubwa kukua kwa elimu Tanzania na Africa kiujumla.

Habari picha na Ally Thabith




TBA YAANZA KUWAONDOA WADAIWA SUGU DAR ES SALAAM

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Dar es Salaam umeanza zoezi la kuwaondoa wapangaji waliolimbikiza madeni ya kodi ya pango.


Akizungumza na wandishi wa habari Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam Arch. Bernard Mayemba amesema zoezi la kuwaondoa wapangaji hao linafata taratibu zote za kisheria.

"Utaratibu wa huu kuwandoa wadaiwa sugu wa kodi ya pango unaongozwa na dalali ya makahama ambaye ni Twins Auction Mart, kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wapangaji wetu kutolipa kodi ya pango na kuwa na malimbikizo makubwa ya madeni wengi wakiamini kwa kuwa ni nyumba za Serikali hawawezi kutolewa licha ya kuwa na madeni hayo" amesema Mayemba

Pamoja na hatua wa kuwaondoa kwa nguvu kwenye nyumba hizo Mayemba amesema TBA imeazima kuwafikisha Mahakamani wadaiwa wote lengo likiwa ni kuhakikisha wanalipa madeni yao yote.

"Wadaiwa hao wenye madeni makubwa, wameifanya TBA kushindwa kutekeleza mipango ya ukarabati wa nyumba zilizopo na kujenga nyumba mpya zitakazopangishwa au kuuzwa kwa watumishi wa umma na wananchi wanaokabiliwa na changamoto ya makazi" amesisitiza Mayemba.

Vile vile ameeleza juu ya maboresho yaliyofanywa na TBA kupitia mfumo mpya wa kielektroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) ambapo mfumo huo utakuwa unatoza riba ya 20% kwa mpangaji atakae kaa zaidi ya miezi 3 bila kulipa kodi ya pango. Riba hiyo itaendelea kila mwezi kwa kiwango mfuto ( automatically) cha 20% mpaka deni litakapokamilika kulipwa.

Zoezi ya kuwaondoa wadaiwa sugu katika mkoa wa Dar es Salaam litadumu kwa muda wiki tatu ambapo litafanyika katika nyumba na majengo yote yanayosimamiwa na TBA