Tuesday, 29 October 2019

MKURUGENZI WA TIC AFICHUA SIRI NZITO


Geofrey Mwambe Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) amesema TIC imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuwavutia wawekezaji na kuja kuwekeza hapa nchini ambako mpaka sasa kwanzia mwezi wa Kwanza hadi wa Tisa 2019 wamesajili makampuni 227 huku sekta ya viwanda inaongoza kwa uwekezaji ambako viwanda 128 vimesajiliwa, amesema siri kubwa ya mafanikio haya kutoa elimu ya uwekezaji, kuishauri serikali katika kuondoa vikwazo vya uwekezaji, kuondoa tozo za uwekezaji, kupatikana kwa TIN namba bure na upatikanaji wa vibali vya ujenzi kwa haraka pamoja na usajili wa makampuni kwa haraka kupitia brela hii ndio ambayo imefanya wawekezaji kuwa na imani na Raisi John Pombe Magufuli. Taasisi ya AFS group imeipongeza TIC kwa kukizi vigezo kumi na moja katika uwekezaji ambako Tanzania imeshika nafasi ya 105 mwaka huu kati ya nchi 190 ukilinganisha na mwaka jana ambako ilikua nafasi ya 131 kwa wafanyabiashara kuwa na sauti pia imeshika nafasi ya 165 mwaka huu kati ya nchi 190 ukilinganisha na mwaka jana katika kuondoa vikwazo vya kodi ambako mwaka jana imeshika nafasi ya 167 kwa upande wake EFC group imeipongeza Tanzania kwa kushika nafasi ya 7 kati ya nchi 20 ukilinganisha na mwaka jana ilishika nafasi ya 15 katika kuwavutia wawekezaji hapa nchini, mikoa inayoongoza katika uwekezaji hapa nchini ni Dar es Salaam na Pwani.
Geofrey Mwambe ametoa wito kwa watanzania kuwekeza hapa nchini, Makampuni 227 yaliyosajiliwa ya thamani ya dora za kimarekani Bilioni 2.0093 ambako ajira zilizo tengenezwa kwa watanzania kupitia TIC ni 38856.

Habari picha na Ally Thabith

Saturday, 26 October 2019

TBS YAWAFUNGULIA MILANGO WAJASILIAMALI WADOGO KATIKA KUELEKEA MASOKO YA KIMATAIFA.


Afsa mwandamizi wa shirika la viwango Tanzania TBS Joseph Ismail amesema wameamua kuwapa Elimu na mafunzo wajasiliamali wadogo kwenye Sekta ya usindikaji mazao ya kilimo na vipodozi lengo waweze kukizi viwango za bidhaa zao ili waweze kuuza hapa nchini na nje ya nchi amesema hawa wajasilia mali wadogo ni kundi ambalo limesaulika katika swala la kupewa Elimu juu ya bidhaa zao ndiyo maana tbs tumechukua maamuzi ya kuwafikia ili wakue kiuchumi na wawe na hali ya kutambua nao wanahusika kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza viwango za bidhaa zao za usindikaji na vipodozi na tbs inawatambua wajasilia mali wadogo kwa kuwapa elimu bule na huduma za viwango bila malipo.


Nae kwa upande wake Afsa viwango wa tbs kutoka idara ya kilimo na chakula Sanjo Noely Stephano amewataka wajasiliamali wadogo wa sekta ya mazao na vipodozi wazingatie matumizi ya viwango kwenye bidhaa zao kwani ni muhimu pia amefanua kuwa kunahaina mbili za viwango viwango vya lazima na si vyalazima ambako viwango vya lazima vinahasili mazingira,Afya ya mtumiaji na maswalaya uchumi ndiyo maana shilika la viwango bts linawataka wajasilia mali wadogo ili wazingatie viwango kwa maslahi ya biashara zao na Taifa.

Amemalizia kwa kusema faida ya matumizi ya viwango ikiwemo kuongezeka kwa masoko,kuleta imani kwa wateja na kukuza kipato cha mjasiliamali. amesema haya kwenye ofisi za Sido ambako shirika la viwango tanzania tbs lilipowafikia wajasilia mali wadogo wanaosindika mazao na anaotengeneza vipodozi vingunguti jijini Dar es Salaam.


Pichani wajasilia mali wadogo wakisikiliza kwa makini maada zinazo tolewa na wawezeshaji kutoka shirika la viwango Tanzania tbs kuhusu jinsi ya wajasiriamali hao wadogo kwenye sekta ya usindikaji wa mazao na bidhaa za vipodozi jinsi ya kuzingatia matumizi ya viwango ili wapate masoko makubwa semina hii imefanyika kwenye ukumbi wa sido jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na 
Ally Thabiti

MKURUGENZI WA GLOBAL LINK EDUCATION ATETA NA WADAU


Abdulmariki mkurugenzi wa Global Link Education amewataka wadau wa sekta ya Elimu waendelee kuunga mkono tuzo zinazotolewa kwenye sekta ya Elimu hapa nchini.


Nae kwa upande Mwalimu Raurenti Ndoje anayefundisha shule ya sekondary ya Garanose ambayo ipo jijini Dar es Salaam Tegeta, Amewashukuru Global Link Education kwa kushirikiana na wizara ya Rais tamisemi na Serikali za mitaa kwa yeye kupewa tuzo ya kuwa mwalimu alikuwa amefanya vizuri katika kufundisha somo la Biology.


Suzan Hassani Bahati ni mwana aliyemaliza kidato cha sita Hasa Secondary School ambaye ni mshindi wa somo la History amewataka Global Link Education, Serikali na wadau wengine waendelee kutoa tuzo hizi za Elimu kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya ufaulu Nchini na kuwapa moyo na molali kufundisha zaidi Walimu.


Pichani waziri wa Ofisi ya Raisi na serikali za mitaa Selemani Jafu akimpa tuzo Mwalimu wa shule ya secondary ya Fedha kwa kufundisha vizuri kwa somo la Physics kitaifa kwenye tuzo za Global Link Education kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam huku Selemani Jafu akiwataka watunga miongozo wabadili mitaala ya Elimu kwani imekuwa ya kuwakomoa wanafunzi.

Pia akitaka tuzo hizi ziwe endelevu zi siwe za zima moto.

Habari Picha na 
Ally Thabiti 

Thursday, 24 October 2019

MSANII NGULI KALA JEREMAYA AWAFUTA MACHOZI VIJANA WALIOKATA TAMAA

Msanii wa kizazi kipya Kala Jeremaya amezindua taasisi inayoitwa ndotolengo ni kuwasaidia vijana ambao wameshindwa kukamilisha ndoto zao ambao wamekata tamaa za kimaisha taasisi hi itafika Tanzania nzima, ametoa wito kwa jamii, vijana taasisi mbalimbali na serikali wa muunge mkono.

Habari Picha na Ally Thabith

HASHIMU RUNGWE MWENYEKITI WA CHAMA CHA UMMA AFUNGUA MILANGO

HashimuRungwe amewataka watanzania waende kwenye ofisi za chama cha Chauma ili wapewe kadi lengo wawe na sifa zakugombea nafasi za uwenyekiti kwenye uchaguzi wa Serikali za mtaa utakao fanyika tarehe 24/11/2019 pia amekiasa chama cha mapinduzi ccm waache tabia ya kubeza vyama vingine pia amewataka wote watakao chaguliwa kuongoza serikai za mtaa waache ubazazi kwakununuliwa na ccm na ametoa rai watu waache ukuadi wa siasa amesema haya kwenye ofisi zake makumbusho Jijini Dar es Salaam

Habari Picha na Aly Thabit

SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) YAONDOA HOFU NA MKANGANYIKO DHIDI YA MAZAO YA KILIMO


Mwandisi Joaness Maganga Mkurugenzi wa upimaji na ugezi ubora shirika la viwango nchini Tanzania (tbs) amesema kutokana na mabadiriko ya sheria ya mwaka 2019 ambako tbs imepewa mamlaka ya kusimamia usalama na ubora wa chakula kutoka kwenye mamlaka iliyokuwa TFDA imeamua kuitisha semina kwa wasafirishaji wa mazao ya kilimo katika kuwa elekeza na kuwafahamisha kwa ubora wa mazao yao na usalama watapata kutoka tbs, tangu tbs ipewe mamlaka haya imepita ni miezi mitatu na mwitikio kwa watanzania mwitikio umekuwa wa kuridhisha hii inatokana na semina wanazo zitoa.
mwandisi Joaness Maganga amesema wanamipango yakwenda kutoa semina mkoani Katavi na kwenye kanda zingine inchini Tanzania juu ya wasafirishaji wa mazao ya kilimo ili biashara zao ziwe zenye ubora na ufanisi mkubwa na ziweze kupata masoko nchi nyingine, Mwandisi Joaness Maganga amesema tbs imeshakamilisha jengo lenye ghorofa ambalo litakuwa linahusika katika upimaji ubora na viwango kwa bidhaa mbalimbali.

Ametoa wito kwa watanzania kuunga mkono na kutoa taarifa zozote zile juu ya bizaa zisizo kuwa na ubora kupitia tbs ameongezea kwa kusema kuwa kupitia online.
Amesema haya kwenye ukumbi wa anatogo Jijini Dar es Salaam

amesema tbs wameamua kutoa hizi semina bure bila gharama yoyote ili watu waweze kusafirisha biashara zao za kilimo zikiwa safi, ubora na usalama kwani wakifanya hivi wataepukana na usumbufu na bidhaa zao zitakuwa za ushindani kwao na Taifa na hatimaye itapelekea kukua kwa uchumi wetu Tanzania na ameahidi kutoa Elimu na Mafnzo inchi nzima

Habari picha na Ally Thabith

KUEREKEA SIKU YA VIWANGO DUNIANI TBS YAWEKA HAZARANI

Meneja wa mafunzo na utafiti Hamisi Sudi amesema katika viwango duniani, Shirika la viwangoo vya ubora nchini Tanzania tbs wameweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kutoa semina za bure nchi nzima kuhusu kufuata utaratibu wa bizaa kuwa na ubora pia wameweza kuzuia bidhaa feki zisizo kuwa na ubora kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi ya Tanzania ambako kila mwaka tarehe 14-10 ni siku ya ubora wa viwango duaniani ambako amesema tagu mwaka 2015 biadha zilizokuwa zikitoka Tanzania kwenda nje ya nchi ni Tilioni 4 na kufikia mwaka 2018 zimeongezeka kufikia Tilioni 5 na bidhaa za inport kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania zimepungua kutoka Tilioni 29 mwaka 2015 na kufikia Tilioni 19 mwaka 2018 hii inatokana na kazi nzuri inayofanywa na tbs katika kuhamasisha wa matumizi ya bidhaa za ndani.
Amesema haya kwenye semina ya wafanya biashara wa mazao ya kilimo ukumbi wa Anatogo Jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na Ally Thabith

Wasafirishaji wa mazao ya kilimo wapongeza mikakati ya mizito ya tbs

Nosiata Mwakilagi kutoka mkoani shinyaga amesema tbs wameamua kuwakomboa wasafirishaji wa mazao ya kilimo kwa kuwapa mafunzo ya mazao ya kilimo katika kufanya biashara yao ya kitaifa na yakimataifa kwani hapo mwanzo hawakuwa na uelewa wowote katika kufuata viwango vya ubora katika biashara zao za kilimo nakupelekea kupata hasara kubwa ameahidi Elimu na Mafunzo aliyoyapata kutoka tbs ameahidi atawafikishia na wengine.
amesema haya kwenye ukumbi wa anatogo Jijini Dar es Salaam

Habari picha na Ally Thabith

WASAFIRISHAJI WA BIDHAA ZA KILIMO WAFURAHIA MAFUNZO YA TBS


Witness Joseph Kutoka kampuni ya green gold ameipongeza shirika la viwango nchini Tanzania (tbs) kwakuwapa mafunzo kuhusu jinsi ya kufunga bidhaa zao za kilimo pia namna ya kuweza kufuata utaratibu wakuwa na bidhaa bora na amewapongeza TRA, wizara ya kilimo na watoa mada wengine ametoa wito kwa tbs waendelee kutoa elimu na mafunzo haya kwa nchi nzima. Semina hii imefanyika ukumbi wa anatogo Jijini Dar es Salaam.
Habari Picha na Ally Thabith

HAMFREY POLEPOLE AWAPONGEZA VYUO UIN


Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (ccm) Hamfrey Polepole amewapongeza UIN kwa kumuenzi mwalimu nyerere kwakuwakutanisha vijana mbalimbali kwenye kongamano ambalo limeelezea mchango mkubwa aliofanya mwalimu nyerere na alivyotengeneza ujamaa nchini Tanzania.

Habari picha Ally Thabith

Wednesday, 23 October 2019

MTAALAM WA MIFUMO YA AFYA ATOA YA MOYONI



Manyirizo mtaalamu wa mifumo ya Afya kutoka global health Supply Change amesema yeye amenufaika kwa kupata mbinu mbadara jinsi ya kukwepa vikwazo katika maswala ya ugavi wa manunuzi wa bidhaa za afya pia amewata UNFPA wasikate tamaa katika elimu na mafunzo kwenye sekta ya Afya. nao washiriki kama wanavyoonekana pichani wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na UNFPA pamoja na Serikali katika kuondoa urasimu katika bidhaa za afya.
Habari picha na Ally Thabith

MSHIRIKU WA MASWALA YA UGAVI AFURAHIA FURSA


John Samwel amesema mkutano huu kwakuondoa mnyororo wa thamani wa ugavi wa manunuzi ya dawa, Vifaa tiba na vitenganishi vya maabara vimemsadia kwa kiasi kikubwa wa vitu hivi, elimu hii ataenda kuipeleka kwa watu wengine.

Amesema anaipongeza UNFPA kuja na jambo hili zuri kwani wananusuru maisha ya watanzania na watu wengine.

Habari picha na Ally Thabith

MPHAMASIA MKUU WA SERIKALI ATETA MAZITO


Daudi Msasi Mphamarcia Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa huduma za dawa wizara ya Afya amewapongeza UNFPA kwa kuweza kuwaunganisha na wadau mbalimbali kutoka nchi tofauti kujadili maswala ya mnyororo wa thamani katika maswala ya ugavi kwa upande wa manunuzi ya dawa, vifaa tiba na vitenganishi vya maabara. Hii itaisaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto za ununuzi wa Vitu hivi pia itaondoa maswala ya Rushwa na Urasimu katika manunuzi na usambazaji wa dawa, Vifaa tiba na vitenganishi.

Amewaomba UNFPA waendelee kutoa mafunzo kama haya Daudi Masasi Amesema wanaunga mkono juhudi na jitihada zinazofanywa na UNFPA kwenye Sekta ya Afya kwani wanaokoa maisha ya watu wengi inchini Tanzania na kuunga mkono Juhudi za Rais Magufuli kwa asilimia Mia kuerekea Tanzania ya viwanda.

Habari picha na Alli Thabith

Monday, 21 October 2019

BODI YA UTALII NCHINI TANZANIA (TTB) YAJA NA MBINU MPYA

Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Bi.Devota Mdachi akimpatia zawadi Mwandishi Sanghoon Ryu kutoka Haedan Media na Kituo cha Televishioni cha KBS mara baada ya Mkutano na Waandishi wa Habari  leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari Bi, Devota mdachi amesema kuwa bodi ya utalii wamezindua rasmi swahili tourism ili kuwezesha sekta ya utalii kuenea zaidi na kuwafikia wadau mbalimbali ulimwinguni kote. 


Waziri wa mambo ya nje Profesa Palamagamba John Aidan kabudi 
Ameipongeza sana bodi ya utalii Nchini kwa kuweza kuzindua swahili tourism kwani kufanya Hivyo kutawezesha kupanua sekta yetu ya utalii na kutuongezea mapato mengi zaidi 
Ndug Tumain pia ameunga mkono juhudi zinazofanywa na Bodi ya utalii TTB kwan wameweza kupiga hatua kubwa sana na kudai kuongeza ushirikiano zaidi ili kuleta tija katika maendeleo ya sekta ya utalii 
Habari picha na Ally Thabiti 


Friday, 4 October 2019

CCBRT YAWATOA HOFU NA WASIWASI WAZAZI WENYE WATOTO


DR. Zainabu wa kitengo cha mifupa na upasuaji Hospital ya CCBRT amesema wanatoa matibabu bure kwa watoto wenye midomo sungura pia wanagharamia gaharama za usafili na malazi kwa wazazi na walezi kwa watoto wenye midomo sungura ametoa lai kwa watanzania ususani kwa wamama wajawazito kutotumia sigara wakati wa ujauzito wao pia uzito na kisukali ni miongoni mwa vyanzo vya kumpata mtoto mwenye mdomo sungura.

Amesema haya jijini Dar es salaam kwenye Hospital ya CCBRT.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

CCBRT YAPONGEZWA KWA KUREJESHA MATUMAINI KWA WATOTO WENYE MIDOMO SUNGURA


Rehema Benito mkazi wa Temeke amesema kitendo cha Hospitali CCBRT kutoa huduma bure kwa watoto wenye midomo sungura ni jambo zuri kwani matibabu yake ni ya gharama sana Rehema Benito ametoa wito kwa wazazi na walezi kutowaficha watoto wenye midomo osungura.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye hospital ya CCBRT.

Habari picha na
Ally Thabiti

Thursday, 3 October 2019

WAZIRI WA KILIMO KUBURUTA MAHAKAMANI WATAKAO HUSIKA KUHUJUMU MBOLEA


Waziri wa Kilimo Japhet Asunga amsema bei elekezi za mbolea ni shilingi 45,000/= kwa mkoa wa Dar es Salaam na shilingi 58,000/= kwa Mkoa wa Rukwa amewataka wauzaji na wasambazaji wa mbolea wauze mbole zao nchini Tanzania kwa bei elekezi pia ni malufuku kuuza mbolea feki na wale watakao tolosha mbolea kupeleka nje ya nchi watachukuliwa hatua kali hikiwemo kupokonywa leseni zao na kufunguliwa mashtaka ya kuhujumu uchumi.

Amesema kifungu cha 4 sheria namba 9 ya mwaka 2009 na kanuni ya 56 ya mwaka 2011 inawataka makampuni ya mbolea kuhuza mbolea kutokana na bei elekezi iliyopangwa na serikali ametoa wito kwa watanzania kutumia vyama vya ushirika na TFRA katika kununua mbole na ametoa rai kwa mtu yeyote anaehitaji kuja kuwekeza ujenzi wa viwanda vya mbolea milango ipo wazi. Hata hivyo Japhet Asunga waziri wa Kilimo amewataka wakulima kutumia fursa za kpongua bei ya mbolea walime kwa wingi na watumie wataaramu kwa matumizi ya mbole.

Amesema haya jijini Dar es Salaam kwenye wizara ya kilimo wakatika akizungumza na wana habari.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

FAMILIA YA MWALIMU NYERERE YANG'AKA NA KUTOA MANENO MAZITO KWA SERIKALI


Magori Sophia Nyerere amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa uhuru kuanzia tarehe 08-14 October 2019 kwaajili ya kumuenzi baba wa Taifa amesema kuwa serikali isiwe na hofu kwani hii ni kumbukizi imepangwa na famili ya Mwalimu Nyerere hivyo serikali nayo itaendelea na kumbukizi yake amesema haya jijini Dar es Salaam kwenye hostel ya New Afrika.

Habari picha na
Ally Thabiti

Tuesday, 1 October 2019

JOSEPH BUTIKU AWAFUNDA WATANZANIA


Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation amewataka watanzania kutoa lugha za matusi, Uzalilishaji, Kebei, Unafki, Umbea na ukuwaji kwani hivi vitu vinaleta uchonganishi zidi ya serikali na wananchi huku akizipongeza azaki za kiraia kuja na ilani za uchaguzi kwani huu ni mwongozo mzuri katika kuelekea chaguzi mbalimbali.

Hamesema haya kwenye ukulmbi wa Kisenga jijini Dar es Salaam.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA THRDC ATEMA CHECHE ZA MOTO


Vick Mtetema mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa THRDC amesema azaki za kiraia wamekuja na mwalubaini wa kuwasulutisha vyama vya siasa kuwa fursa na nafasi wanawake kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa azaki za kirai kuzindua ilani yenye matumaini mapya kwa wanawake pia ilani hii itasaidia serikali kutekeleza kwa vitendo maswala ambayo ayajatekelezwa yenye mlengo wa kijinsia.

Amesema haya kwenye Ukumbi wa Kisenga jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Ilani ya Azaki za kiraia.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

CCM KUTEKELEZA KWA VITENDO IRANI YA ASASI ZA KIRAIA


Katibu mwenezi wa CCM Ndg hamphrey polepole amesema irani iliyotolewa na asasi za kiraia chini ya mtandao wa utetezi wa haki za biandamu (THRDC) wameipokea na wataifanyia kazi kuanzia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi wa mwaka 2020.

Amesema haya kwenye ukumbi wa kisenga jijini Dar es Salaam.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

THRDC KUTINGA UMOJA WA MATAIFA NA RIPOTI NZITO


Mratibu wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) Onesmo Elengulumo amesema wameamua kuwakutanisha wanaharakiti kutoka asasi mbalimbali kwa ajili ya kukusanya ripoti ya utekelezaji ya maswala ya haki za binadamu na kupeleka umoja wa mataifa
.
Amesema swala la kukosekana kwa uhuru wa habari, uhuru wa kukusanyika kwa vyama vya siasa ni vitu ambavyo havitekelezwi pia swala kupatikana kwa katiba mpya ni jambo ambalo halijatekelezwa hadi sasa na kuuwawa kwa wandishi wa habari pamoja na kutekwa mfano Azori Gwanda wa gazeti la mwananchi na kufungiwa kwa vyombo vya habari Mfano wa kwanza TV na kupigwa faini ya 5,000,000/= kwa watetezi Tv huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu na maswala ya utawala bora ni tatizo wamesema watawasilisha umoja wa Mataifa.

Habari Picha na
Victori Stanslaus

SHIVIAWATA YATOA NENO KWA THRDC


Brandina Sembu katibu wa jumuhia ya wanawake na watoto shirikisho la vyama la watu wenye ulemavu (SHIVIAWATA) amesema kitendo cha THRDC kukusanya ripoti za maswala ya watu wenye ulemavu katika utekelezaji kupeleka umoja wa Mataifa ni jambo la kishujaa tena linatakiwa kuungwa mkono kwani serikali ya Tanzania kwa upande wa watu wenye ulemavu wanawake aiwatendei haki hata kidogo mfano walemavu wa kutosikia wakienda kujifungua mahospitalini hakuna wataaramu wa lugha za alama hivyo upelekea vifo vya watoto na mama wajawazito.
pia ni tatizo kwa vitanda vya kujifungulia kwa wanawake walemavu wa viungo vya miguu ambako vitanda hivi vipo juu zaidi hivyo amewataka THRDC kuwasilisha maswala haya ili yatendewe kazi huko umoja wa Mataifa ili serikali ya Tanzania iwajibishwe.

Habari picha na
Victoria Stanslaus 

WATU WENYE ULEMAVU WAIPA TANO THRDC


Mwanasherisa Maduu Cosmas William kutoka under the same sun  amesema maswala ya watu wenye ulemavu bado ayajatekelezwa kwa kiwango kikubwa licha ya serikali kulizia mikataba ya kimataifa na kuwepo kwa sheria mfano kuwajiliwa kwa watu wenye ulemavu bado aijatekelezwa kwa kiwango kikubwa hivyo amewapongeza THRDC kwakuwakutanisha kufanya tasmini hii huku akiwaomba THRDC wasisite kuwasilisha maswala yanayowasibu watu wenye ulemavu umoja kwa mataifa.

Hamesema haya kwenye ukumbi wa LAP  mkumbusho jijini Dar es Salaam.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO WATAKIWA KUFIKISHWA MARA MOJA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE JKCI


Na Mwandishi wetu
1/10/2019 Madaktari nchini wameshauriwa kuwatuma watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mapema iwezekanavyo mara baada ya kuwagundua kuwa na matatizo hayo ili waweze kupata matibabu kwa wakati.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto (JKCI) Naiz Majani wakati akizungumzia kuhusu kambi ya matibabu ya magonjwa ya moyo ya ya kuzaliwa nayo kwa watoto ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Taasisi hiyo.
Dkt. Naiz ambaye pia ni msimamizi wa kambi za matibabu ya moyo zinazofanyika katika Taasisi hiyo alizitaja dalili za mtoto mwenye magonjwa ya moyo kuwa ni  pamoja na  kutokwa na jasho kwa wingi wakati wa kunyonya, kutoongezeka uzito, kupata nimonia, kikohozi cha mara kwa mara , kushindwa kucheza , kuvimba miguu na kubadilika rangi kwenye midomo na kucha kuwa rangi ya bluu.
“Ninawaomba madaktari wanapoona dalili kama hizi kwa mtoto wawalete katika Taasisi yetu kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi kwani kuna  baadhi ya matatizo ya moyo ya kuzalliwa nayo mtoto hatakiwi  kuzidi umri wa miezi sita hadi mwaka mmoja bila ya kupata matibabu. Mtoto mwenye matatizo hayo akichelewa  kupata   matibabu akiwa na umri huo hawezi kufanyiwa upasuaji tena”, alisisitiza Dkt. Naiz.
“Katika kambi ya matibabu ya pamoja tuliyoyafanya na wenzetu wa Shirika la Mending Kids International lenye wataalamu wa afya  kutoka nchini Italia na Marekani watoto wanne walishindwa kufanyiwa upasuaji   kutokana na umri wao kuwa mkubwa  zaidi ya mwaka mmoja na nusu hivyo wataendelea na matibabu ya kawaida”, alisema Dkt. Naiz.
Akizungumzia kuhusu kambi hiyo Dkt. Naiz alisema watoto 40 walifanyiwa upasuaji kati ya hao watoto waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua 17 na upasuaji wa bila kufungua kifua  23 ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wamesharuhusiwa kurudi nyumbani.
Dkt. Naiz alisema, “Kambi hii imeenda vizuri, kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama, wakati huduma za upasuaji zinaendelea kwa watoto  walijitokeza wasamaria wema wawili na kuchangia  matibabu ya watoto wawili ambao wazazi wao hawakuwa na uwezo  wa kuwagharamia matibabu. Watoto hao wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri”, alisema Dkt. Naiz.
Kwa upande wa wazazi ambao watoto wao walipata wafadhili wa kulipiwa gharama za matibabu walishukuru kwa huduma ya matibabu ambayo watoto wameipata na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia gharama za matibabu ya moyo kwa watoto.
“Namshukuru mfadhili wa mtoto wangu ambaye amelipa gharama za matibabu ya mtoto ambaye amefanyiwa  upasuaji na hali yake inaendelea vizuri. Mara kwa mara amekuwa akinipigia simu na jana amekuja kumuangalia mtoto kujuwa maendeleo yake”, alisema Eva Jacob

MSANII NGULI APINGA VIKALI UZALILISHAJI WA WANAWAKE


Kalajeremaya ni msanii wa mziki wa kizazi kipya amewataka wasanii hapa nchini kuacha kuwatumia wanawake na watoto wa kike hapa nchini kuwazalilisha kwa kuwaweka kwenye video zao huku maongo yao ya sili yakiwa yanaoneka kwani yeye amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwatumia watoto wakike bila maungo yao ya mwili kuonekana.

Hamesema haya kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

SANAA YA MZIKI NA FILAM YAINGIZA WATOTO KATIKA VISHAWISHI


Mkurugenzi wa program kwenye tasaisi ya Bright Jamii Inshetiave Godwin Mungi amesema wameweza kufanya tafiti katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Aruha wamebaini kuwa sanaa ya muziki imesababisha watoto wengi kujihusisha na maswala ya unywaji pombe, uvutaji wa bangi na kuacha masomo kwa upande wa filam umesababisha wanawake pamoja na watoto wakike kujihusisha kwenye maswala ya ngono zembe amehiasa jamii, wazazi, walezi,serikali na viongozi wa dini waakikishe  wasanii sanaa wanayotoa ilinde utu wa mwanamke na mtoto pamoja na maadili na destuli ya nchi yetu ya Tanzania.

Amesema haya kwenye uzinduzi wa ripoti ya maswala ya sanaa na filam katika hoteli ya Selena jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

RUSHWA YA NGONO YAWATAFUNA WASANII WA KIKE NCHINIAAA


Anna Sangai amesema asasi za kiraia zimeamua kutoa elimu kwa wasanii kuacha kuwazalilisha wanawake na watoto katika kazi zao za sanaa kwani wanawake wengi wanatumika kutoa rushwa ya ngono katika filam na nyimbo .
Hivyo asasi za kiraia zitatoa elimu na pia wameitaka serikali kuweza kutumia sheria katika matumizi ya filam oambazo azina maadili na nyimbo lengo kunsulu watoto waweze kusoma kwa bidii.

amesema haya kwenye uzinduzi wa ripoti ya namna ya sanaa na filam zinavyo wazalilisha wanawake na watoto kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.

Habari picha na
Victoria Stanslaus

VIONGOZI WA KIDINI WALALAMA JUU YA FILAM


Sheikh Abdallah Kundecha amesema nyimbo zinazoimbwa na wasanii wa kitanzania pamoja na Filam zinamzalilisha mwanamke pamoja na watoto kwani lugha zinazotumika kwenye nyimbo ni zamatusi pia wanawake katika filam wanatumika katika kuonesha maungo yao ya mwili ususani ni sehemu za sili huu ni udhalilishaji.

Nae mkurugenzi wa Bright Jamii Inshetive bibi Irene ambaye yupo kushoto wa Sheikh Abdallah Kundecha amevitaka vyombo vya habari na wasanii kupigavita maswala ya uzalilishaji wa wanawake na watoto kwa wandishi wa habari wasipige nyimbo za matusi na uzalilishaji na wasanii waache kutoa filam za kufedhehesha wanawake na watoto amesema haya Serena Hotel jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti inayohusu wasanii pamoja filam zipozalilisha wanawake na watoto.

habari picha na
Ally Thabiti