Tuesday, 27 February 2024

WATU WENYE ULEMAVU WAPONGEZA TRENI YA UMEME

 Ally Thabiti ni kijana mlemavu wa kuona amesema mladi w reli ya mwendo kasi ya treni ya umeme (SGR) umezingatia maitaji ya watu wenye ulemavu wa aina zote kuanzia miundo mbinu kwenye kituo cha kupandia hiyo treni pamoja na ndani mabehewa yenyewe. hivyo kwaniaba ya watu wenye ulemavu wameishukuru serikali ya Tanzania chinu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani uku wakimpongeza mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika la Reli Tanzania Mwandisi Masanja Kadogosa kwa kuweza kusimamia mradi wa SGR na kuzingatia maitaji ya watu wenye ulemavu.


Habari Picha na Victilia Stanslaus

Saturday, 24 February 2024

TTCL KUSAINI MKATABA WA MIAKA MITANO NA BBS

Waziri NAPE NAUYE amesema TTCL kusaini mkataba wa miaka 5 na nchi ya Buruni utakao dumu kwa miaka 5 wenye thaman ya shilingi Milioni Tatu nukta tatu (3.3) sawa na Shilingi Bilioni 8.3 ambapo kutaenda kudumisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi mbili (2). Amewaagiza TTCL kuakikisha BBS inapata huduma bora ili wapate kuendesha shughuli zao kwa uraisi, amewaomba Burundi kujitaidi hili kusaini mkataba wa kituo cha kutunzia data na kuimarisha sekta ya mawasiliano kwani Tanzania ipo tayari kuwahudumia Burundi na nchi zingine.

Mwandishi Peter Lwanga amemshukuru Rais kwa kutufunguria fursa katika ukanda wa Afrika Mashariki pia amewapongeza BBS kwa kukubari kushirikiana na Tanzania kupitia shirika la mawasiliano Tanzania kwa kutumia huduma za mkongo wa Taifa ambakko leo wamesaini mkataba wa Dola za Kimarekani Milioni 3.3 sawa na Bilioni 8.3 za Kitanzania ambapo mktaba huu utadumu ndani ya miaka mitano (5) ameahidi TTCL watawapa huduma bora. Kwani wanajivunia kuwa na uhusiano mzuri tangu mwaka 2019.

Shirika la mawasiliano Tanzania lipo tayali kutoa huduma bora na iliyo kamilika ambapo wanaamini ushirikiano huu utaimarisha uhusiano wa kindugu kati ya nchi zetu na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Tanzania na Burundi. TTCL itaendelea kutoa huduma bora na kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukuza sekta ya mawasiliano nchini Tanzania. Haya yamesemwa na mwandishi Peter Luanga kutoka TTCL.

Bw. Jeremie Diomende hageringwe mtendaji mkuu wa Burundi Backbone System – BBS na viongozi wa BBS kutoka Burundi mtendaji mkuu amewashukuru Marais wan chi mbili kwa ushirikiano uliopelekea kusaini mkataba wa miaka mitano (5) kwa Dolla za Kimarekani 3.3 sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 8.5 kwani itasaidia kufanya shughuri zao kwa wapesi na ufanisi kwani Burundi inafurahia kuunganishwa na mkongo wa Taifa wa Tanzania ambao utaenda kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano na Tecknolojia kuongeza ushirikiano wa kibiashara kwani hili tukio ni la kiistoria katika sekta ya mawasiliano.

Habari na Victoria Stanslaus

Thursday, 22 February 2024

TMA YATOA TAADHARI KWA WANANCHI JUU YA MVUA YA MASIKA


 


MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA MASIKA

MACHI – MEI, 2024

 

Kielelezo 1: Mwelekeo wa mvua za Machi hadi Mei, 2024.

 

Dondoo muhimu za msimu wa mvua za Masika; Machi - Mei 2024

 

Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Masika katika kipindi cha Machi – Mei, 2024, ushauri kwa wadau wa sekta na mamlaka mbalimbali kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Utalii na Wanyamapori, Uchukuzi, Mamlaka za miji, Nishati, Maji na Madini, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa. Baadhi ya mambo muhimu katika taarifa hii ni: -

 

          i.    Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani kwa msimu wa Masika, 2024 zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

 

         ii.    Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Machi, 2024.

        iii.    Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Februari, 2024 katika maeneo mengi na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2024 katika maeneo mengi.

 

Athari zinazotarajiwa:

          i.    Vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo.

 

        ii.    Kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka.

       iii.    Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji.

 

 

 

1.     MWENENDO WA MVUA ZA MSIMU (NOVEMBA, 2023 HADI APRILI, 2024) NA MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA (MACHI – MEI), 2024

1.1     Mwenendo wa mvua za Msimu (Novemba, 2023 hadi Aprili, 2024)

Mvua za Msimu zilizoanza mwezi Novemba, 2023 zimenyesha kwa kiwango cha Juu ya Wastani katika mikoa ya Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Katavi, Iringa, Ruvuma, Lindi, Mtwara na kusini mwa mkoa wa Morogoro na Wastani katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe na Njombe katika kipindi cha Novemba, 2023 hadi Januari, 2024. Mvua hizi zilianza mapema wiki ya kwanza na ya pili mwezi Novemba, 2023 na zilitawaliwa na vipindi vya mvua nyingi zilizochangiwa na uwepo wa El NiƱo. Katika kipindi kilichosalia cha msimu (Februari hadi Aprili, 2024) mvua zinatarajiwa kuendelea kama ilivyotabiriwa mwezi Oktoba, 2023, ambapo kwa ujumla mvua zilitabiriwa kuwa za Wastani hadi Juu ya Wastani.

 

1.2       Mwelekeo wa mvua za Masika (Machi hadi Mei), 2024

Msimu wa mvua za Masika ni mahususi kwa maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), pwani ya kaskazini (kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. 

 

Kutokana na mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa katika kipindi cha Masika (kama inavyoelezwa katika kipengele Na. 2 cha taarifa hii), kwa ujumla mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Ongezeko la mvua linatarajiwa mwezi Machi, 2024 katika maeneo hayo. Maelezo ya kina juu ya mwelekeo wa mvua hizo za msimu ni kama ifuatavyo:

 

i.   Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, na Mara) pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma (wilaya za Kakonko na Kibondo):

 

Mvua za Masika zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Juu ya Wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mvua za nje ya msimu zinazoendelea kunyesha zinatarajiwa kuungana na mvua za Masika 2024. Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei, 2024.

 

 

 

 

 

 

 

ii.   Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mkoa wa Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba):

 

Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya kaskazini.

 

Mvua hizo zinatarajiwa kuanza mapema wiki ya nne ya mwezi Februari, 2024 na kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei, 2024.

 

iii.   Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro):

 

Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Juu ya Wastani na zinatarajiwa kuanza mapema wiki ya nne ya mwezi Februari, 2024. Mvua hizo zinatarajiwa kuisha wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Mei, 2024.

 


Kielelezo 2:  Kushoto: Mwelekeo wa mvua za Masika (Machi –Mei), 2024 na Kulia: Wastani wa muda mrefu (miaka 30) wa mvua za Masika (1991-2020).

 

Angalizo 1: Izingatiwe kuwa matukio ya vipindi vya mvua kubwa yanaweza kujitokeza katika Msimu wa Masika, 2024.

 

Angalizo 2: Mwelekeo wa mvua uliotolewa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya mvua na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika

 

 

uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi. Watumiaji wa taarifa hii wanashauriwa kufuatilia taarifa za utabiri wa saa 24, siku 10, mwezi na tahadhari kama zinavyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

 

2.      MIFUMO YA HALI YA HEWA 

Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la magharibi mwa Bahari ya Hindi (pwani ya Afrika Mashariki) ikilinganishwa na upande wa mashariki mwa Bahari ya Hindi. Vilevile, joto la bahari la chini kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo la kusini mwa kisiwa cha Madagaska. Hali hii kwa pamoja inatarajiwa kuimarisha mifumo isababishayo mvua nchini kwa kuimarisha kasi na nguvu ya msukumo wa unyevu nyevu kutoka baharini kuelekea katika maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini-mashariki. Katika eneo la mashariki mwa bahari ya Atlantiki (pwani ya Angola), joto la bahari la chini kidogo ya wastani linatarajiwa. Hali hii inatarajiwa kuimarisha msukumo wa unyevu nyevu kutoka misitu ya Kongo kuelekea nchini hususan katika maeneo yanayozunguka ziwa Viktoria, kaskazini mwa mkoa wa Kigoma na nyanda za juu kaskazini mashariki. Hata hivyo, hali ya El-NiƱo inayoendelea katika Bahari ya Pasifiki inatarajiwa kupungua nguvu hususan tunapoelekea mwishoni mwa msimu wa mvua wa MAM, 2024.

 

3.      ATHARI NA USHAURI

Athari za kisekta na ushauri uliotolewa hapa chini umeandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kushirikiana na wataalam wa sekta husika katika mkutano wa wadau wa hali ya hewa uliofanyika tarehe 19 Februari, 2024. Wadau wa sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii wanashauriwa kupanga na kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia taarifa mahususi za hali ya hewa zinazotolewa na TMA.

 

a)        Kilimo na Usalama wa Chakula

Vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo. Magonjwa kama vile ukungu (Fungus) yanatajariwa kuongezeka na kuathiri mazao kama nyanya, ufuta, maharage na mazao jamii ya mizizi. Hata hivyo, shughuli za kilimo zinatarajiwa kuendelea kama ilivyo kawaida katika maeneo mengi.

 

Wakulima wanashauriwa kuandaa mashamba, kupanda, kupalilia na kutumia pembejeo husika kwa wakati, kutumia mbinu bora na teknolojia za kuzuia maji kutuama shambani, mmomonyoko na upotevu wa rutuba, na kuchagua mbegu na mazao sahihi kwa ajili ya msimu huu wa Masika. Pia, wanashauriwa kuimarisha miundombinu ya kilimo hususan maeneo ya mabondeni pamoja na kudhibiti visumbufu vya mimea ili kupunguza athari

 

zinazoweza kujitokeza. Aidha, wauzaji na wasambazaji wa pembejeo za kilimo wanashauriwa kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wakati.

 

b)        Mifugo na Uvuvi

Wafugaji na wavuvi wanatarajiwa kunufaika na upatikanaji wa malisho na chakula cha samaki. Hata hivyo, mlipuko wa magonjwa ya mifugo kama vile ugonjwa wa homa ya bonde la ufa na kuzaliana kwa wadudu wanaosambaza magojwa vinaweza kujitokeza.  Vilevile, matukio ya kuongezeka kwa magonjwa ya mwani baharini na kupungua kwa uzalishaji wa mwani kutokana na kupungua kwa kiwango cha chumvi ya maji ya bahari vinatarajiwa.

 

Wafugaji wanashauriwa kutumia mbinu bora za ufugaji ili kutunza malisho na kuvuna maji ya mvua kwa matumizi ya baadae. Jamii inashauriwa kuweka mipango mizuri ya matumizi bora ya maji na malisho. Wakulima wa mwani wanashauriwa kulima mwani kwenye maji ya kina kirefu ili kuondokana na athari za maji ya mvua yanayokuwa yanaingia baharini. Vilevile, wafugaji na wavuvi wanashauriwa kufuatilia mirejeo ya tabiri za hali ya hewa na ushauri kutoka kwa maafisa ugani ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza na kuongeza tija katika msimu huu wa mvua.

 

c)        Utalii na Wanyamapori

Hali ya malisho na maji kwa ajili ya wanyamapori katika mbuga na hifadhi inatarajiwa kuwa nzuri. Hata hivyo, mvua za wastani hadi juu ya wastani zinazotarajiwa katika maeneo mengi zinaweza kusababisha kutuama na kusambaa kwa maji na kupelekea kuhama kwa wanyamapori. Hali hii inaweza kupelekea magonjwa ya wanyamapori kusambaa kwa wanyama wanaofugwa na binadamu kutokana na wanyamapori kuingia katika makazi ya jamii zinazozunguka hifadhi na mbuga. Pia, hali hii inaweza kusababisha hatari kwa binadamu na wanyama wanaofugwa kutokana na kushambuliwa na wanyamapori.

 

Mamlaka husika zinashauriwa kuboresha miundombinu mbalimbali katika hifadhi za wanyamapori na kujenga uelewa kwa jamii ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza. Hivyo basi, jamii inashauriwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo wanyamapori wataingia katika makazi ya watu.

 

d)        Usafiri na Usafirishaji

Kutokana na mvua zinazotarajiwa, sekta ya usafiri na usafirishaji inatarajiwa kuathirika na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya barabara na reli, ongezeko la ajali barabarani katika usafiri wa nchi kavu, kuchelewa au kusitishwa kwa safari za nchi kavu, ndege, majini,

 

mawasiliano hafifu angani na kwenye maji na kupelekea kuongezeka kwa gharama za uendeshaji katika usafiri wa anga, nchi kavu na majini. Mamlaka husika na wadau wanashauriwa kuchukua hatua stahiki katika utekelezaji wa matengenezo na ujenzi wa miundombinu mbalimbali pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara wa miundombinu ya usafiri na usafirishaji ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

 

e)        Nishati, Maji na Madini

Mvua zinazotarajiwa zitachangia kuongezeka kwa kina cha maji katika mito, maziwa na mabwawa hivyo matumizi sahihi ya maji majumbani na uzalishaji wa umeme ni muhimu kupewa kipaumbele. Hata hivyo, kupungua kwa ubora wa maji, kuongezeka kwa kifusi cha mchanga maji na uharibifu wa kingo za mito na mtandao wa usambazaji maji pia unatarajiwa.

 

Sekta ya Madini hususan shughuli za uchimbaji mdogo wa madini, huenda zikaathirika, hivyo tahadhari za kiusalama ni muhimu kuchukuliwa ili kukabiliana na maporomoko ya ardhi na miamba. Mvua zinazotarajiwa huenda zikaathiri mtandao wa usafirishaji na usambazaji wa nishati ya umeme na kupelekea kukosekana kwa umeme. Hivyo, mamlaka husika na wadau zinashauriwa kuzingatia usimamizi endelevu wa rasilimali maji na mgawanyo wake kwa maeneo mbalimbali kama vile shughuli za uchakataji madini, uzalishaji umeme, matumizi ya viwandani na majumbani.

 

f)         Mamlaka za Miji na Wilaya

Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kusababisha kutuama kwa maji na mafuriko. Hali hii inaweza kusababisha uharibifu wa miundombinu na upotevu wa maisha na mali. Mamlaka za Miji na Kamati za Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana na athari zinazohusiana na mafuriko ikiwa ni pamoja na shughuli za utafutaji, uokoaji na msaada wa kitabibu.

 

g)        Sekta ya Afya

 

Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji unaoweza kusababishwa na maji ya mvua kutuama na kutiririka. Mamlaka za Afya na jamii zinashauriwa kuchukua tahadhari stahiki ili kupunguza athari za kiafya zinazotarajiwa kwa kuharibu mazalia ya mbu, kutibu maji kabla ya kuyatumia, kunywa maji safi na salama pamoja na kuhakikisha uwepo wa dawa na vifaa tiba vya kutosha katika vituo vya Afya.

 

 

 

h)        Sekta Binafsi

Sekta binafsi inatarajiwa kunufaika na mvua zinazotarajiwa katika msimu huu wa Masika hususan katika shughuli za kilimo, uzalishaji viwandani, n.k. Hata hivyo, wingi wa mvua unaweza kupelekea athari katika shughuli za ujenzi wa miundombinu, uhifadhi na usafirishaji wa mazao tete na bidhaa.

 

Sekta binafsi zinashauriwa kushirikiana na wataalam mbalimbali ikiwemo wataalam wa hali ya hewa ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza. Taasisi mbalimbali zikiwemo Benki na Bima zinashauriwa kuandaa na kutoa huduma mahususi kwa wadau ili kujenga ustahamilivu katika biashara.

 

i)          Menejimenti za Maafa

Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kujitokeza na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi na kupelekea uharibifu wa miundombinu, mazingira, upotevu wa mali na maisha. Hivyo, mamlaka husika katika idara mbalimbali na idara ya Menejimenti ya Maafa nchini zinashauriwa kuendelea kuratibu utekelezaji wa mipango itakayosaidia kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza. Aidha, sekta, mamlaka husika na Kamati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji/Mitaa zinashauriwa kushirikiana na kuchukua hatua stahiki ikiwemo kutoa elimu na miongozo itakayohamasisha kuzuia au kupunguza madhara, kujiandaa, kukabiliana na maafa na kurejesha hali endapo maafa yatatokea.

 

j)          Vyombo vya Habari

Vyombo vya Habari vinashauriwa kupata, kufuatilia na kusambaza taarifa za utabiri na tahadhari, pindi tu zinapotoka ili jamii iweze kuzipata kwa wakati. Vilevile, vinashauriwa kutafuta ushauri wa kitaalamu kutoka katika sekta husika wakati wa kuandaa, kutayarisha na kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa watumiaji. Pia, inapendekezwa kutumia lugha nyepesi wakati wa kuhabarisha jamii.

 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawashauri watumiaji wote wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima, wafugaji, mamlaka za wanyamapori, wasafirishaji, mamlaka za maji, afya, shughuli za ujenzi (Makandarasi), uchimbaji madini, upakuaji na ushushaji mizigo Bandarini kuendelea kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalam katika sekta husika.

 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mirejesho ya mwelekeo wa mvua na hali ya hewa kwa ujumla nchini kadri

 

 

inavyohitajika. Aidha, wadau wanashauriwa kuwasiliana na Mamlaka ili kupata taarifa mahsusi za mwelekeo na utabiri wa hali ya hewa ili kukidhi mahitaji maalum katika sekta zao.

 

 

 

 

Imetolewa: Tarehe 22 Februari, 2024.

Na: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania:


Bahari Picha na Ally Thabiti

Wednesday, 21 February 2024

 BALOZI MINDU AHIDI MAFANIKIO KWENYE KUMBI LA MIKUTANO ZA ARUSHA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE NA MWL NYERERE INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE.

Balozi mindu amesema katika semina ya siku mbili wanaopewa maafisa wanaofanya katika ukumbi AICC ARUSHA ,utasidia kwa kiasi kikubwa ufanisi ulio mzuri kwa wateja wanaohudumia pia utawaongezea chachu ya utendaji kazi na kupata mbinu mpya za kuvutia wateja na kutafuta fulsa za kimasoko ambapo itapelekea ongezeko kubwa la mikutano ya kitaifa na kimataifa kufanyika katika ukumbi huo.

kwa upende wao washiriki wamepongeza uwongozi kwa kuwapa semina hii kwani watapata mbinu mpya na zenye Tija ambapo itapelekea kukua uchumi wa Tanzania kwa kupata fedha za kigeni

Hbari Picha Ally Thabiti.




Tuesday, 20 February 2024

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AKABIZI MAGARI NA PIKIPIKI KWA TFS

Angera Kailuki Waziri wa Maliasili na Utalii amewataka TFS kuweza kuyatumia vizuri Magari aina ya Maroli mawili pamoja na magari mawili ya Randcuser pamoja na Pikipiki 39 kwaajili ya kuimalisha na kukuza sekta ya misitu nchini Tanzania uku akitaka hatua kari zichukuliwe kwa watumishi wasiokuwa na maadili.

Habari na Ally Thabiti

TANROADS, TBA, NA TEMESA KUKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA EGYPT

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuleta wawekezaji kutoka Egypt wa usafirishaji na miundombinu pamoja na wajumbe wake. Waziri Bashungwa amefuraishwa na mradi wa kutoka Cairo kwenda Captaon Afrika ya Kusini ambao njia yake itapita kwenye nchi 9 na Tanzania ikiwemo nchi itakayo nufaika na mradi huu ambao utakamilika ifikapo mwaka 2060 pia amewakaribisha kwenye sekta binafsi kwaajili ya project mbalimbali moja ya fursa ya kupata wawekezaji wa viwango vya juu.

Waziri bashungwa amewaambia Tanroads kutekeleza ahadi ya Rais kuwa na mkakati wa waandisi kuwa sehemu ya kusaidia wakandarasi wa zawa ambako kila kilometa 20 kutakuwa na vijana wawili. Kubadilishana uzoefu wa majenzi na kujifunza amewaomba Temesa kuwa na mitambo ya kisasa kwaajili ya kusaidia Wakandarasi wa ndani hii ndio mikakati ya Rais kuleta ubunifu na kuongeza wigo.

Kipande cha kutoka Zambia unapoingia nchini pale Songwe ni kilometa 1600 ni moja ya barabara ya mikakati Dar es Slaam na Morogoro Tanroads kujenga barabara za Express Morogoro kwenda Dodoma ambako itafungua uchumi na kutengeneza ajira kwa watanzania. 

Nae waziri wa Egypt amewaarika viongozi wa Tanzania kutembelea nchini mwao ili wajionee ujenzi wa Barabara zinavyopendeza . Chakwanza kudizaini njia za kawaida zote wanaweza kuzitengeneza katika ubora pia wanauwezo wa kutengeneza madaraja ya aina zote amewaomba watu wa Tanroads waende wakajionee ubunifu wa hali ya juu. Ujenzi wa barabara za Cement ya kawaida na hata barabara za rami pamoja na njia za juu njia za mwendokasi.

Habari na Victoria Stanslaus

Monday, 19 February 2024

WADAU WA SEKTA YA USAFILISHAJI WAPATA WAWEKEZAJI KUTOKA EGYPT

Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji Prof Makame Mbawara amefurahi kutembelewa na wageni na kuangalia fursa kwenye uwekezaji  kama mradi wa Bandari wa kujenga gati namba 13 na 15 ni mradi utakaoenda kuondoa changamoto pia litajengwa gati kubwa kwaajili ya kupokelea mafuta ambako mtwara itajengwa bandari kwaajili ya kusushia mizigo. Tanga kuna mradi wa reri, Mtwara kuna mradi wa reri ambao utaanzia Uvinza kwenda Mbambabei kilomita 1000.

Maboresho gati namba 8 hadi 11 ambako meri zinakaa wiki mbili mpaka 3 ambako itasaidia kuondoa msongamano waziri ameshukuru Rais kwa kupambania maswala ya miundombinu ya bandari, viwanja vyandege pamoja na reri na serikali itaendelea kuwekeza kwenye miundo mbinu.

Kwa upande wake Waziri wa EGYPT Hon Amb. Sherif Abdelhamid Ismail ametoa shukrani kwa nchi yao kuwa ya pili wa urafiki na Tanzania kisiasa ambako utaenda kufafanua ushirikiano mkubwa wakufanya biashara.

Misri na Tanzania ilikuwa na urafiki kwenye utalii na bara zima la Afrika katika kusapoti kazi za maendeleo mpaka sasa mausiano yameendelea kwenye kitengo cha uchukuzi ambako itapelekea wizara mbalimbali na sekta ya uchukuzi kusonga mbele amesema nchi ya Misri itafanya kila kitu kwaajili ya afrika na kujitoa katika uwekezaji kwenye njia za anga na miundombinu mingine kitengo cha usafirishaji ndio kitengo muhimu na kinategemewa na nchi ilikiweze kutoa mitandao mbalimbali mabadilishano ya biashara kati ya nchi na nchi nyingine ili kuwaraisishia wananchi na watu kuja kuwekeza mambo ya kitalii na kidini.

amesema kupata miradi ya nchi hivyo kuna umuhimu wa kuongelea njia za bandari kavu kwa sababu Tanzania ndio mlango unao tumika na nchi zingine. angependa bandari ya Dar es Salaam kushirikiana na bandari ya misri na kubandilisha na uzoefu pia itapelekea mausihano kuongezeka kitu kitapelekea misri kusadirisha biashara zao kutoka mto Nail na kuamasisha biashara nchi za maretenia na ziwa Victoria ili kutanua utalii. Projecti ya kuwekeza Tanzania ni fursa ya kuzifikia nchi zingine ambako ajenda yao itakamilika ifikapo mwaka 2060 ambako wanataka kuetenegenza njia kilometa 200 kutokan Kairo ambako nchi 9 njia iyo itapita miongoni mwao Tanzania ambako itapelekea kuongeza wigo baadhi ya uzoefu wa kampuni kufanya kazi mbalimbali miongoni mwa makampuni ni Arabic na Asweedi katika ushirikiano wa kujenga bwawa la mwalimu Nyerere hii imekuwa alama tosha kwa Misri litakapo kamilika.

Pia alizungumzia miji mipya ya viwanda Tanzania ina mraba mlioni moja uwekezaji wake milino mia moja na nafasi za kazi 50. Hakuna viwanda zao makampuni ya madawa vifaa vya ujenzi viwanda vya vinywaji na vyakula na wapo tayali kutekeleza mala moja, Kampuni ya Aweedi kufundisha watu ili kufanya kazi kwa weredi na ameaidi kufanya kazi vizuri ili kuacha alama iliyo bora. Uhusianio wa kisiasa Tanzania na Misri kuongezeka zaidi na kuyalaisisha Makampuni ya Misri nchini Tanzania ambako kampuni zipo tayari kuwekeza soko la Tanzania ambako Tanzania inaweza kutumia Kampuni hizi ili kuweza kubadilishana uzoefu katika kitengo cha uchukuzi.

amemshukuru Prof. Mbarawa na kumkribisha Misri kuwatembelea haya yamesemwa na waziri wa uchukuzi wa Egypt kwenye kikao muhimu.

Habari na Victoria Stanslaus

CRDB YAKUTANA NA WANAHABARI


 
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Benki ya CRDB ABDUL MAJJID MSEKELA amesema lengo la kukutana na wanahabari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari ni kuendeleza mahusiano na ushirikiano katika kazi pia amesema CRDB inafanya kazi kubwa sana katika sekta ya kifedha na imeweza kupata mafanikio makubwa kwaajili ya kupita wanahabari ambako CRDB Bank inatoa taarifa zake kwa uma kupitia vyomboa vya habari.

Nae MASOUD KIPANYA mwanahabari wa Clouds Fm amesema CRDB lipoti wanazotoa za kifedha ni jumuishi ambako mwaka 2006 walitoa lipoti yao kwa mara ya kwanza uku ikionesha 10% za huduma zao kuwafikia wananchi na lipo hii ya tano huduma jumuishi ilikuwa 76%.

Habari picha na Ally Thabiti 

WAZIRI NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAAHIDI MAMBO MAZITO ZAO LA MIANZI

Waziri wa Maliasili na Utalii Angera Kailuki amesema mkakati aliouzindua wa zao la mianzi serikali itasimamia na kutekeleza kwa vitendo kwa kutega bajeti ya kutosha ili kutoa elimu kwa jamii namna bora ya kupanda mianzi kwani faida zitakazopatikana ajira, kodi, fedha za kigeni, malisho kwa mifugo na kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. 

Waziri Kailuki ameitaka taasisi ya utafiti kutafiti mbegu bora na ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kupanda zao la mianzi.

Nae kwa upande wake katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dr. Hassan Abbas amesema zao la mianzi litasaidia kuondoa mmomonyoko wa ardhi huku akiahidi mpango kazi na mkakati uliozinduliwa wa kupanda zao la mianzi atasimamia kikamilifu.

Nae kwa Ubapande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema tukipanda mianzi tutabusulu kumomonyoka kw ardhi hekta milioni 5 huku, akisisitiza kuwa zao la mianzi litaleta faida kubwa nchini Tanzania ambako mikoa kumi na nne 14 litapanda zao la mianzi.

Habari na Ally Thabiti

Friday, 16 February 2024

MAJIMBO KUMI YANUFAIKA NA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA DAR ES SALAAM

Mganga Mkuu Daktali Mang'ura amesema Magari yapatayo 14 yamepatikana Serikalini kupitia mradi wa UVIKO ambapo kila jimbo litapata gari moja kwaajili ya kuwabebea wamam wajawazito pamoja na wagonjwa wengine.

Vituo 25 vya upasuaji wanatakiwa kufika salama Magari yamepelekwa vituo maalumu kwaajili ya huduma ya Afya.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala alikuwa na haya, ameongea kwaniaba ya wakuu wa wilaya wote amemshukuru mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kukabidhi magari ya wagonjwa hasa kwa Mama wajawazito na wataendelea kumuunga mkono kwenye afya na maeneo mengine.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Arbeti Charamira amesema magari ya kubebea wagonjwa 10 na magari 4 kwaajili ya ufuatiliaji. Ambako amesema gari moja ina gharimu shilingi milioni 10 ameimiza kuyatunza magari haya na kutumia vizuri. Katika majimbo 10 Dar es Salaam kila jimbo litapata gari moja aya ni zaidi ya magari 500 haya ni maoni ya Rais wakati akitafuta fedha kwaajili ya maji kujenga madarasa pamoja na afya bila kusaau miundombinu bilioni nyingi zilienda kwenye maji.

Magari haya yataenda kusaidia wagonjwa kuongeza nguvu kiteknolojia kwa wahudumu wa afya, zaidi ya watu Milioni 6 wanahitaji huduma mzuri ya afya.

Wito kwa madereva kuendesha magari vizuri kwa wale watakao endesha magari huku wamelewa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao hamesema haya wakati akikabidhi magari 10 kwa kila jimbo gari moja (1) kwaajili ya kubebea wagonjwa na wamama wajawazito.

Habari na Victoria Stanslaus 


Thursday, 15 February 2024

SUPA JACKPOT YAZIDI KUACHILIA MABILIONI KWA WASHINDI

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas amemtangaza David Mwenge Nyantora kuwa mshindi wa Super Jackpot ya mechi 13 akiwa amejishindia shilingi 265,780,681. ikiwa ni takribani miezi 11 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Supa Jackpot mechi hizihizi 13 ambapo hii ni awamu ya pili kupata mshindi wa Supa Jackpot tangu ianzishwe rasmi.

hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashri kupata zaidi ya washindi wa Jackpot 10 na kuwatangaza kwa miaka 6 mfululizo. Supa Jackpot ya wiki hii imeweza kutoa washindi wa bonasi jumla ya 8708 huku jumla ya bonasi zilizotolewa ikiwa ni zaidi ya milioni 756.

Naye mshindi alikuwa na haya ya kuongea, Akizungumza katika hafla hiyo maalumu iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, Dar es Salaam, David anasema alianza kucheza na SportPesa mwaka 2018, baada ya kuifahamu kupitia usomaji wa magazeti, amewashauli Watanzania waendelee kucheza na SportPesa.

Naye Mkuu wa kitengo cha Uhusiani na Mawasiliano wa SportPesa Sabrina H. Msuya alimpongeza mshindi na kumhimiza kuwa balozi kwa wengine. Anawakumbusha Watanzania Supa Jackpot ipo na itaendelea kuwepo kutegemeaa na matokeo ya kila wiki. endeleeni kutuamini kama ambavyo, David ametuamini na matokeo ya ushindi mtayapata. amesema haya wakati wa kumtangaza mshindi wa Supa Jackpot David Mwenge Nyantora.

Habari Picha na Victoria Stanslaus

Thursday, 8 February 2024

UZINDUZI MAALUMU WA KADI ZA WANACHAMA WA YANGA HII NI YAKIMATAIFA

Mkurugenzi wa Biashara na Wateja Binafsi wa benki ya NMB, Filbert Mponzi amesema wamefungua tawi Sengerema kwa ajili ya kuwaudumia wanachama wa Yanga hivyo amewataka kujisajili kwa wingi kwa kulipa Ada NMB watanufaika na Yanga watanufaika, ameongezea kwa kusema ukiona NMB umeliona tawi la YANGA

Habari na Victoria Stanslaus

UZINDUZI WA KADI MAALUMU ZA WANANACHAMA WA YANGA

 


Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amewataka wanachama kujisajili kwenye Benki ya NMB na kufungua Akaunti zao ambapo amesema Ada yake ni shiringi 1,000,000/= ya Kitanzania na mwaka mmoja ukiisha unaweza kuirenew kwa shilingi 25000/= ambapo ameelezea faida zake, kwanza Taasisi zote mbili zitanufaika

1) Jezi sita (6) kila msimu /na VIP Tiket 10 mechi ya nyumbani.

2) Punguzo hadi asilimia kumi ukifanya malipo ya kadi kwa QR.

3) VIP Lounge viwanja vya ndege vya kimataifa bure.

Hizi ndiyo faida ya kadi maalumu za wanachama wa Yanga.

Habari Picha na Victoria Stanslaus